Sidebar with Floating Button
AckySHINE Katoliki
AckyShine

LITANIA YA KUWAOMBEA MAPADRE WOTE 1

Featured Image

Kwa ajili ya Baba Mtakatifu wetu ..(N); Bwana, umpe moyo wako wa uchungaji mwema
Kwa ajili ya warithi wa Mitume; Bwana, uwape wawe na uangalifu uliojaa upendo kwa mapadre wao
Kwa ajili ya Maaskofu wako waliochaguliwa na Roho Mtakatifu; Bwana, uwabakishe karibu na kondoo wako
Kwa ajili ya wachungaji wako; Bwana, uwafundishe kutumikia kuliko kutafuta kutumikiwa
Kwa ajili ya waungamishi na washauri wa kiroho; Bwana, uwafanye kuwa vyombo visikivu kwa Roho wako Mtakatifu
Kwa ajili ya mapadre wanaotangaza neno lako; Bwana, uwawezeshe kushirikisha Roho wako na Uzima wako
Kwa ajili ya mapadre wanaosaidia utume wa walei; Bwana, uwatie moyo wa kuwa mifano bora
Kwa ajili ya mapadre wanaofanya kazi na vijana; Bwana, uwajalie wawakabidhi vijana kwako
Kwa ajili ya mapadre wanaofanya kazi kati ya watu fukara; Bwana, uwajalie wakuone na wakutumikie kupitia hao
Kwa ajili ya mapadre wanaoangalia wagonjwa; Bwana, uwajalie wawafundishe thamani ya mateso
Kwa ajili ya mapadre fukara; - Uwasaidie ee Bwana
Kwa ajili ya mapade wagonjwa; - Uwaponye ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wazee; - Uwapatie tumaini la raha ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wenye huzuni na walioumizwa; -Uwafariji ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wanaohangaishwa na wale wanaosumbuliwa; - Uwape amani yako ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wanaodharauliwa na wanaonyanyaswa; - Uwatetee ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre waliokata tamaa; - Uwatie moyo ee Bwana
Kwa ajili ya wale wanaosomea upadre; - Uwape udumifu ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wote; - Uwape uaminifu kwako na kwa Kanisa lako ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wote; - Uwajalie utii na upendo kwa Baba Mtakatifu na kwa maaskofu wao ee Bwana
Kwa ajili ya mapadre wote; - Uwajalie waishi katika umoja na maaskofu wao ee Bwana
Tunawaombea mapadre wote; - Wawe wamoja kama Wewe na Baba mlivyo wamoja ee Bwana
Tunawaombea mapadre wote; - Waishi na kuendeleza haki yako ee Bwana
Tunawaombea mapadre wote; - Washirikiane katika umoja wa ukuhani wako ee Bwana
Tunawaombea mapadre wote, wakiwa wamejawa na uwepo wako; - Waishi maisha yao ya useja kwa furaha ee Bwana
Tunawaombea mapadre wote; - Wajalie ukamilifu wa Roho wako na uwageuze wafanane nawe ee Bwana
Kwa namna ya pekee, ninawaombea mapadre wale ambao kwa njia yao nimepokea neema zako. Ninamwombea padre aliyenibatiza na wale walioniondolea dhambi zangu, wakinipatanisha na Wewe na Kanisa lako.
Ninawaombea mapadre ambao nimeshiriki Misa walizoadhimisha, na walionipa Mwili wako kama chakula. Ninawaombea mapadre walionishirikisha Neno lako, na wale walionisaidia na kuniongoza kwako. Amina.


AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Diana Mallya (Guest) on June 5, 2017

Mungu akubariki!

Jane Muthui (Guest) on May 9, 2017

Mwamini katika mpango wake.

John Lissu (Guest) on April 29, 2017

Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia

Simon Kiprono (Guest) on April 12, 2017

Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako

Ann Wambui (Guest) on March 14, 2017

Upendo wa Mungu haukosei kamwe.

Lucy Wangui (Guest) on November 17, 2016

🙏❤️💖 Baraka za Mungu ziwe nawe

Jane Muthui (Guest) on October 29, 2016

Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha

Samson Tibaijuka (Guest) on August 28, 2016

🙏💖🙏 Mungu akufunike na upendo

Charles Mrope (Guest) on August 20, 2016

🙏✨ Mungu atakuinua

Patrick Mutua (Guest) on August 6, 2016

Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia

Lucy Mushi (Guest) on June 11, 2016

🙏🌟 Mungu akujalie amani

Nancy Akumu (Guest) on May 1, 2016

Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu

Peter Tibaijuka (Guest) on April 5, 2016

🙏❤️✨ Asante Mungu kwa kila kitu

Edward Chepkoech (Guest) on March 25, 2016

Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu

Agnes Njeri (Guest) on February 25, 2016

Sifa kwa Bwana!

Lucy Kimotho (Guest) on January 29, 2016

Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote

John Mwangi (Guest) on January 10, 2016

🙏❤️✨ Mungu akujalie furaha

Francis Mrope (Guest) on December 28, 2015

Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni

Mary Njeri (Guest) on July 25, 2015

Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine

Frank Macha (Guest) on July 8, 2015

Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi

Stephen Malecela (Guest) on May 20, 2015

🙏💖 Asante kwa neema zako Mungu

James Malima (Guest) on April 11, 2015

🙏💖 Nakushukuru Mungu

Edith Cherotich (Guest) on April 5, 2015

Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao

Related Posts

SALA YA NOVENA KWA MOYO MTAKATIFU WA YESU

SALA YA NOVENA KWA MOYO MTAKATIFU WA YESU

Ee Moyo Mtakatifu sana wa Yesu, chemchemi ya kila baraka, ninakuabudu, ninakupenda, na kwa majuto... Read More

NOVENA KWA AJILI YA KUJIANDAA KWA SIKUKUU YA MOYO MTAKATIFU WA YESU

NOVENA KWA AJILI YA KUJIANDAA KWA SIKUKUU YA MOYO MTAKATIFU WA YESU

Inaweza kusemwa wakati wowote katika mwaka. Kwa ajili ya kujiandaa kwa Sikukuu ya Moyo Mtakatifu ... Read More

LITANIA YA KUWAOMBEA MAPADRE WOTE II

LITANIA YA KUWAOMBEA MAPADRE WOTE II

Kwa ajili ya Baba Mtakatifu wetu ..(N); Bwana, umpe moyo wako wa uchungaji ... Read More

SALA YA MTAKATIFU INYASI

SALA YA MTAKATIFU INYASI

Roho ya Kristo unitakase
Mwili wa Kristo uniokoe
Damu ya Kristo unifurahishe
Maji ... Read More

SALA KWA BIKIRA MARIA KATIKA UKIWA WAKE

SALA KWA BIKIRA MARIA KATIKA UKIWA WAKE

Nakusikitikia sana Mama Mtakatifu Maria kwa sababu ya ukiwa wako mkuu. Uchungu wako ulikuwa mkubw... Read More

Kumbuka ee Bikira Mwenye Rehema

Kumbuka ee Bikira Mwenye Rehema

Read More

SALA YA KUMWOMBA MTAKATIFU TERESIA WA MTOTO YESU

SALA YA KUMWOMBA MTAKATIFU TERESIA WA MTOTO YESU

Ee Mtakatifu Teresia wa mtoto Yesu, ulistahili kuitwa Msimamizi wa misioni katoliki za dunia yote... Read More

SALA ZA IBADA KWA BIKIRA MARIA WA MATESO

SALA ZA IBADA KWA BIKIRA MARIA WA MATESO

ROZARI YA MATESO SABA YA BIKIRA MARIA

Tumia Rozari ya Mateso Saba ya Bikira Maria iliyo ... Read More

AMRI ZA KANISA

AMRI ZA KANISA

1. HUDHURIA MISA TAKATIFU DOMINIKA NA SIKUKUU ZILZOAMRIWA

2. FUNGA SIKU YA JUMATANO YA MAJI... Read More

ROSARI YA BIKIRA MARIA MAMA WA MSAADA WA DAIMA

ROSARI YA BIKIRA MARIA MAMA WA MSAADA WA DAIMA

Namna ya kusali Rozari kwa Bikira Maria Mama wa Msaada wa Daima

(Tumia rosari ya kawaida... Read More

Kuweka nia njema

Kuweka nia njema

Kumheshimu Mungu wangu, Namtolea roho yangu, Nifanye kazi nipumzike, Amri zake tu nishike, Wazo n... Read More

Majitoleo ya Asubuhi

Majitoleo ya Asubuhi

Ee Baba yetu Mungu Mkuu, Umenilinda usiku huu, Ninakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho, Ni... Read More

📘 About 🔒 Login 📝 Register 📞 Contact