Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu. Zab 95:7-8
Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya.
Dawa ya dhambi ni kutubu na kusamehewa.
Kutubu sio kusema tuu "Ninatubu" au "Ninaomba msamaha". Kutubu ni kuona uchungu kweli rohoni kwa dhambi tulizotenda, tukizikataa na kunuia kutokuzitenda tena.
12βLakini hata sasa,β
nasema mimi Mwenyezi-Mungu,
βNirudieni kwa moyo wote,
kwa kufunga, kulia na kuomboleza.
13Msirarue mavazi yenu kuonesha huzuni
bali nirudieni kwa moyo wa toba.β
Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu;
yeye amejaa neema na huruma;
hakasiriki upesi, ni mwingi wa fadhili;
daima yu tayari kuacha kuadhibu.
14Huenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atabadili nia
na kuwapeni baraka ya mazao,
mkamtolea sadaka za nafaka na kinywaji.
15Pigeni tarumbeta huko Siyoni!
Toeni amri watu wafunge;
itisheni mkutano wa kidini.
16Wakusanyeni watu wote,
wawekeni watu wakfu.
Waleteni wazee,
wakusanyeni watoto,
hata watoto wanyonyao.
Bwana arusi na bibi arusi
na watoke vyumbani mwao.
17Kati ya madhabahu na lango la hekalu,
makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu,
walie na kuomba wakisema:
βWahurumie watu wako, ee Mwenyezi-Mungu.
Usiyaache mataifa mengine yatudharau
na kutudhihaki yakisema,
βYuko wapi basi Mungu wao?ββ Yoeli 2:12-17
Uzuri wa Mungu ni kwamba anasamehe na kusahau, tunapotubu dhambi zetu Mungu anatufutia makosa yetu, anaponya majeraha au madhara yaliyoletwa na dhambi hiyo na kisha antubariki kwa Neema na Vipawa vya kusonga Mbele.
Maana nitawasamehe makosa yao, wala sitazikumbuka tena dhambi zao.β Yeremia 31:34
Mungu anatambua kwamba Binadamu ni dhaifu na anaweza kuanguka dhambini ndio maana anatupa nafasi ya Kutubu na Kumrudia yeye.
13Afichaye makosa yake hatafanikiwa;
lakini anayeungama na kuyaacha atapata rehema. Methali 28:13
Mungu anazifahamu juhudi zetu katika kutafuta kutenda mema ndio maana anakubali toba ya kweli na anatupa matumaini ya kusonga mbele.
"Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu". Isaya 1:18
Biblia inatuambia kuwa anaheri yule atubuye na kusamehewa kosa lake kwa sababu hana hatia mbele ya Mungu.
1 Heri yake mtu aliyesamehewa kosa lake,
mtu ambaye dhambi yake imeondolewa kabisa.
2Heri mtu ambaye Mwenyezi-Mungu hamwekei hatia,
mtu ambaye hana hila moyoni mwake. Zaburi 32:1-2
Tunapaswa kukumbuka kuwa toba ya kweli ya kutupa msamamaha inaambatana na kuwasamehe wengine na kuondoa kinyongo kwa wengine waliotukosea. Yesu anatufundisha kuwa inatupasa tusamehe ili na sisi tusamehewe.
14βMaana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nyinyi pia. 15Lakini msipowasamehe watu makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe nyinyi makosa yenu. Mathayo 6:14-15
Tena, Mungu anatusamehe Makosa Yetu bila kujali tunakosea Mara nagpi na tunarudi kwake mara ngapi. Ndio maana Yesu alitufundisha kuwa tunapokosewa na wenzetu ni lazima tuwasamehe haijalishi wametukosea mara ngapi.
3Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, muonye; akitubu, msamehe. 4Na kama akikukosea mara saba kwa siku, na kila mara akarudi kwako akisema, βNimetubu,β lazima umsamehe.β Luka 17:3-4
Unapotubu na kuomba msamaha ni sharti uwasamehe pia wale waliokukosea ili na wewe usamehewe. Kusameheana na wenzetu ndio tabia ya Kimungu ambayo yatupasa kujifunza na kuiishi ili na sisi tuwe watoto wema wa Mungu.
12Nyinyi ni watu wake Mungu; yeye aliwapenda na kuwateua. Kwa hiyo, basi, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe nyinyi. Wakolosai 3:12-13
Tumuombe Mungu atujalie Moyo wa toba na kujirudi kwake Kila tunapokosea. Na tumuombe pia atupe nguvu na uwezo wa kuwasamehe wale wanaotukosea.
KUMBUKA:Β Unapotubu dhambi zako na kusamehewa ndipo inapokuwa rahisi kwa sala zako kujibiwa. Mungu ni rafiki ya waliosafi Moyoni, na ndio anaowasikiliza na kuwaonyesha nguvu na uwezo wake.
Nakualika kwa Sala ya Toba, uweze kurudi kwa Mungu. Sali kutoka moyoni, kwa kujua kuwa unapendwa na Mungu, Kwa Imani na Matumaini Kwake.
Sala ya Toba
Mungu wangu, Baba wa mbinguni, nakuja mbele zako nikiwa na moyo uliovunjika na toba ya kweli. Nakiri kuwa mimi ni mwenye dhambi, na nimekosa mbele zako kwa njia nyingi. Nimefanya mambo ambayo hayakupendeza, na nimeshindwa kutenda yale uliyoniagiza. Kwa kuwa Neno lako linasema, "Kwa maana wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23).
Ee Bwana, naomba unisamehe dhambi zangu zote. Nimetenda dhambi kwa mawazo, kwa maneno, na kwa matendo. Ninatubu kwa dhati na kwa kweli kutoka moyoni mwangu. Naomba unioshe kwa damu ya Yesu Kristo, Mwanao mpendwa, ambaye alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu. Kama unavyosema katika Neno lako, "Lakini ikiwa tutatembea katika nuru kama Yeye alivyo katika nuru, tu ushirika sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote" (1 Yohana 1:7).
Ninakiri kuwa mimi ni mnyonge bila wewe, na siwezi kufanya lolote bila msaada wako. Naomba unijaze na Roho Mtakatifu, aniongoze na kunipa nguvu ya kushinda majaribu na dhambi. Ee Mungu, niongoze katika njia zako za haki, na unisaidie kuishi maisha yanayokupendeza. Kwa kuwa Neno lako linasema, "Basi kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu" (Wakolosai 3:1).
Ninakuja mbele zako nikiwa na unyenyekevu na moyo wa toba. Naomba unirehemu na unifanye kuwa kiumbe kipya ndani ya Kristo. Kama unavyosema katika Neno lako, "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! yamekuwa mapya" (2 Wakorintho 5:17). Asante kwa upendo wako usio na kikomo, na kwa neema yako inayotosha kila siku. Naomba haya yote kwa jina la Yesu Kristo, aliye Mwokozi wangu.
Bwana, naomba unifundishe kuwa mtiifu na kuwa na moyo wa shukrani kwa kila jambo. Acha neno lako likae kwa wingi ndani yangu, na linibadilishe kutoka ndani hadi nje. Nisaidie kuacha njia zote za dhambi, na kuwa mwaminifu kwako katika kila hali. Kwa kuwa Neno lako linasema, "Neno lako nimeliweka moyoni mwangu, nisije nikakutenda dhambi" (Zaburi 119:11).
Ninakubali kuwa mimi ni mnyonge na ninahitaji msaada wako kila siku. Nakiri dhambi zangu na naomba unisamehe. Naomba unipatie moyo safi, na kunifufua kiroho. Kama unavyosema katika Neno lako, "Ee Mungu, uniumbie moyo safi, unirejeshee roho iliyotulia ndani yangu" (Zaburi 51:10). Naomba unifanye kuwa mwanga na chumvi duniani, ili niweze kuonyesha upendo wako kwa wengine. Kwa kuwa Neno lako linasema, "Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima" (Mathayo 5:14).
Asante, Bwana, kwa kusikia sala yangu. Naamini kuwa umesikia na kujibu ombi langu. Ninatangaza kuwa mimi ni wa Kristo, na ninakubaliana na mapenzi yako maishani mwangu. Kama unavyosema katika Neno lako, "Ninaweza kufanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu" (Wafilipi 4:13). Kwa jina la Yesu, Amina.
Stephen Mushi (Guest) on July 1, 2018
Baraka kwako na familia yako.
David Kawawa (Guest) on June 26, 2018
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Jackson Makori (Guest) on May 8, 2018
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Christopher Oloo (Guest) on January 31, 2018
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Miriam Mchome (Guest) on December 31, 2017
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Carol Nyakio (Guest) on December 25, 2017
Mungu akubariki!
Diana Mallya (Guest) on December 18, 2017
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Joy Wacera (Guest) on December 15, 2017
Neema ya Mungu inatosha kwako
John Mwangi (Guest) on December 6, 2017
Rehema hushinda hukumu
Ruth Mtangi (Guest) on October 26, 2017
Nguvu hutoka kwa Bwana
Margaret Anyango (Guest) on October 13, 2017
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Edward Lowassa (Guest) on October 11, 2017
Baraka kwako na familia yako.
Monica Nyalandu (Guest) on July 5, 2017
Mungu akubariki!
Rose Waithera (Guest) on July 3, 2017
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Sarah Mbise (Guest) on May 31, 2017
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Grace Minja (Guest) on April 3, 2017
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
John Malisa (Guest) on March 11, 2017
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Francis Mrope (Guest) on November 30, 2016
Rehema zake hudumu milele
Edward Chepkoech (Guest) on October 29, 2016
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Jane Muthui (Guest) on October 25, 2016
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Esther Nyambura (Guest) on October 1, 2016
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Jane Malecela (Guest) on September 15, 2016
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Ruth Wanjiku (Guest) on September 14, 2016
Tumaini ni nanga ya roho
Nora Kidata (Guest) on July 31, 2016
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Lydia Mutheu (Guest) on July 25, 2016
Rehema hushinda hukumu
Diana Mallya (Guest) on June 30, 2016
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Victor Mwalimu (Guest) on June 24, 2016
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Edwin Ndambuki (Guest) on April 18, 2016
Neema na amani iwe nawe.
Edward Chepkoech (Guest) on March 12, 2016
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Anna Mchome (Guest) on January 14, 2016
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Catherine Naliaka (Guest) on January 2, 2016
Imani inaweza kusogeza milima
Emily Chepngeno (Guest) on December 6, 2015
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Monica Lissu (Guest) on November 8, 2015
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Nicholas Wanjohi (Guest) on October 17, 2015
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Grace Wairimu (Guest) on September 23, 2015
Kwa Mungu, yote yanawezekana
James Kawawa (Guest) on September 21, 2015
Mwamini katika mpango wake.
Nora Lowassa (Guest) on August 12, 2015
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Agnes Lowassa (Guest) on August 12, 2015
Katika imani, yote yanawezekana
Mary Kidata (Guest) on June 29, 2015
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Alice Jebet (Guest) on June 14, 2015
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe