Vipimo
Mchele basmati, pishori - 3 vikombe
Vitunguu katakata - 2
Nyanya/tungule katakata - 5 takriban
Viazi/mbatata menya katakata - 3 kiasi
Thomu (saumu/garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha kulia
Hiliki ya unga - ½ kijiko cha chai
Kidonge cha supu - 2
Chumvi - kisia
Mafuta - ½ kikombe
Maji ya moto au supu - 5 takriban
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha na roweka mchele
Katika sufuria weka mafuta yashike moto, tia viazi, vitunguu ukaange.
Vikianza tu kugeuka rangi tia thomu na bizari, hiliki, endelea kukaanga kidogo.
Tia nyanya kaanga lakini usiache zikavurugika sana.
Tia mchele ukaange chini ya dakika moja.
Tia maji ya moto, na kidonge cha supu au supu yoyote kiasi cha kufunika mchele yazidi kidogo.
Koroga vichanganyike vitu, kisha funika upike kama pilau.
Pakua ikiwa tayari, tolea kwa samaki wa kukaanga au kitoweo chochote kile
No comments yet. Be the first to share your thoughts!