Unywaji wa pombe ni sehemu ya utamaduni wa Tanzania na nchi
nyinginezo duniani.
Watu hupendelea kunywa pombe katika
sherehe za kidini, kijamii, nyumbani na vilabuni. Wanakunywa
pombe ili kujiburudisha, lakini pia kuongeza ujasiri, kuondoa
aibu au kusahau matatizo yao kwa kipindi fulani au kwa muda
mfupi.
Vijana wengi, hasa wavulana, hudhani kwamba kunywa
pombe ni ishara ya kujionyesha kuwa wamekuwa watu wazima.
Kimsingi, unywaji pombe kidogo hukubalika kijamii na hauna
madhara, lakini ulevi wa kupindukia ni hatari na huweza
kusababisha vifo na haukubaliki katika jamii zetu kwa sababu
hudhoofisha na kufanya watu kusahau majukumu yao, hupunguza
heshima na afya njema.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!