Sidebar with Floating Button
AckySHINE Katoliki
AckyShine

Je, kwa nini unasema kwamba wasichana vijana hawapo tayari kubeba mimba?

Featured Image

Ni kweli kwamba kupata hedhi ni dalili ya mwili wa msichana kuwa tayari kwa kubeba mimba, lakini kupata hedhi hakuna maana kwamba msichana yupo tayari kwa kuanza kujamii ana au kubeba mimba. Uke wa mwanamke ambaye ni mtu mzima ni madhubuti na unavutika, lakini uke wa msichana ni mwembamba na hauwezi kutanuka sana. Hivyo uke wa msichana unaweza kuchanika vibaya wakati wa kujifungua. Vilevile nyonga ya msichana huwa bado nyembamba sana kuweza kumpitisha mtoto wakati wa kujifungua.
Kwa kuongezea, kupata mtoto siyo suala tu la mwili kuwa tayari kubeba mimba na kujifungua. Inamaanisha pia kuwa tayari kuwa na mwenzio wa kushirikiana naye katika malezi ya mtoto, kuwa na kipato cha kutosha cha kutunza familia na kuwa na nyumba ya kuishi. Kwa vyovyote vile kubeba mimba mapema kunamkosesha msichana kuendelea na masomo na hivyo kumyima nafasi nyingi nzuri za mafanikio.
Hivyo kupata hedhi kila mwezi ni dalili tu ya kuelekea kwenye utu uzima. Haimaanishi kwamba mwili wake umekua vya kutosha kuweza kujifungua mtoto na haimaanishi kwamba amepanga maisha yake kikamilifu kuwa mzazi.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Magonjwa ya zinaa yanavyoenea

Magonjwa ya zinaa yanavyoenea

Magonjwa ya zinaa husababishwa na vijidudu vya magonjwa na huambukizwa kwa kukutana kimwili na mt... Read More

Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi?

Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi?

Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote ya kiafya ukikaa muda mrefu bila kujamii ana. Hakuna madha... Read More

Je, nifanye nini ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Je, nifanye nini ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Hakuna chanjo dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, Lakini kuna mienendo ya tabia a... Read More

Je, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI vinaambukiza kwa kujamiiana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni?

Je, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI vinaambukiza kwa kujamiiana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni?

Ndiyo, kuna hatari kubwa ya kuambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI wakati wa kujamii ana kwa nji... Read More

Vidokezo vya Kuepuka Mazungumzo ya Kuchosha na Msichana

Vidokezo vya Kuepuka Mazungumzo ya Kuchosha na Msichana

Mazungumzo ni sehemu muhimu katika uhusiano wowote wa kimapenzi. Lakini kuna wakati mazungumzo ya... Read More

Jinsi ya kujikinga na ubakaji

Jinsi ya kujikinga na ubakaji

Hata kama utafanya kila kitu usibakwe bado inaweza ikatokea. Ubakaji na unyanyasaji wa ujinsia unawe... Read More
Je, kuna tofauti kati ya mapenzi na ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti kati ya mapenzi na ngono/kufanya mapenzi?

Habari yako rafiki? Natumaini uko salama na unafurahia siku yako. Leo nitazungumzia suala linaloh... Read More

Iwapo msichana atajamiiana wakati wa siku salama anaweza kuepuka kupata mimba?

Iwapo msichana atajamiiana wakati wa siku salama anaweza kuepuka kupata mimba?

Siku salama ni siku ambazo hakuna yai ambalo lipo tayari kwa kurutubishwa. Iwapo mwanamke atajami... Read More

Jinsi ya Kujikinga na Mimba Pasipo Kuharibu Afya ya Mwili

Jinsi ya Kujikinga na Mimba Pasipo Kuharibu Afya ya Mwili

Jinsi ya Kujikinga na Mimba Pasipo Kuharibu Afya ya Mwili

Leo tutajadili jinsi ya kujiking... Read More

Je, kuna tofauti za kiutamaduni katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za kiutamaduni katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za kiutamaduni katika ngono/kufanya mapenzi? Swali hili linaweza kusababisha maj... Read More

Je, mvulana atajuaje kama msichana ni bikira? Na pia, msichana anaweza kujitambua vipi kama ni bikira?

Je, mvulana atajuaje kama msichana ni bikira? Na pia, msichana anaweza kujitambua vipi kama ni bikira?

Mvulana hawezi kuthibitisha ubikira wa msichana kwa njia ya kumwangalia wala kwa njia ya kumwingi... Read More

Nini imani ya watu katika ngono/kufanya mapenzi ya mara moja au watu wanapendelea uhusiano wa kudumu?

Nini imani ya watu katika ngono/kufanya mapenzi ya mara moja au watu wanapendelea uhusiano wa kudumu?

Kuna mjadala mkubwa kuhusu imani ya watu katika ngono au kufanya mapenzi ya mara moja ikilinganis... Read More

📘 About 🔒 Login 📝 Register 📞 Contact