Kujamiiana ni uamuzi wa mtu binafsi. Ni uamuzi wako na hakuna
mtu yeyote mwenye haki ya kukuamulia. Lakini unapoamua
kujamiiana hakikisha kwamba ni maamuzi uliojulishwa na kwamba
unaelewa matokeo ya kujamiiana. Usisahau kuchukua hadhari
muhimu. kumbuka kutumia kondomu kujikinga wewe na mwenzi
wako kutokana na mimba usizotarajia na magonjwa kama vile
Virusi vya UKIMWI. Madhari mwili wako unaendelea kukua,
kujamiiana bila ya kondomu ni hatari zaidi kuliko mtu mzima,
kwa sababu maambukizo mengine haswa kwa vijana yanaweza
kukuletea matatizo kama vile ugumba baadaye katika maisha.
Pia jiulize mwenyewe kwa uangalifu kama kweli unataka
kujamiiana. Ni muhimu pia kujadiliana na mwenzi wako na kuwa
na hakika kama wote wawili mnataka kujamiiana. Usijamiiane
kwa sababu tu unafikiria kwamba watu wengine wanajamiiana
au unajitosa kwa kuwa unashawishiwa na marafiki au watu
wazima.

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kujihusisha na mambo ya kujamiiana?

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!