Serikali inatakiwa iamue kuwepo kwa matangazo ya biashara
ya pombe na sigara au la? Serikali ina wakati mgumu katika
kuamua kati ya kulinda afya za watu na shinikizo litokalo
kwa wakulima pamoja na makampuni yanayotengeneza pombe
na sigara. Wenye viwanda na wauzaji wanataka bidhaa hizi
zitangazwe kibiashara kwa sababu wanapata pato kutokana na
kuzalishwa na kuuzwa kwa bidhaa hizi. Serikali yenyewe pia
inapata faida kutokana na kutangazwa kwa tumbaku na pombe
kwa sababu uuzaji wake unaipatia serikali ushuru kupitia kodi.
Nchini Tanzania serikali imeamua kuwa matangazo ya biashara
ya sigara yawe na onyo lisemalo,βUvutaji wa sigara ni hatari kwa
afya yakoβ. Hii inawajulisha wavutaji wa sigara kuhusu hatari
za uvutaji wa sigara na kuacha kila mtu ajiamulie mwenyewe.

Kwa nini pombe na sigara bado zinatangazwa wakati zina madhara?

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!