Je, kuharibika mimba kunasababishwa na nini?

Asimilia kumi hadi i i ishirini ya mimba huharibika. Mimba nyingi zinaharibika katika kipindi cha wiki 12 za mwanzo wa ujauzito. Sababu kuu hutokana na kuharibika kwa yai lililotungwa mimba. Iwapo yai lingeendelea kukua katika hali hii matokeo ni mtoto kuzaliwa na kasoro mwilini au kiakili. Kwa hiyo mimba kuharibika inaweza kuwa ni njia ya asili ya mwili kukabiliana na matatizo hayo ya kimaumbile.
Vilevile kuharibika kwa mimba huweza kutokea kama mama ana magonjwa kama malaria au kaswende, kama ameanguka chini kwa nguvu au kama ana matatizo kwenye via vya uzazi. Dalili za mimba kuharibika ni damu kutoka ukeni na maumivu makali ya tumbo kwa chini.

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!