Hakuna kiwango cha umri kwa kutumia huduma za afya ya uzazi
na njia za uzazi wa mpango. Unatakiwa kuanza kutumia huduma
za afya ya uzazi pale unapoona unazihitaji. Na hasa iwapo
umeamua kujamiiana, unatakiwa uende kwanza kwenye huduma
za afya ya uzazi, na kupata ushauri juu ya ujinsia na masuala
ya afya ya uzazi pamoja na njia mbalimbali za uzazi wa mpango.
Vijana kisheria wamepewa haki ya kutumia njia za uzazi wa
mpango.
Nchini Tanzania kuna sera ya idadi ya watu ya mwaka 1992.2
ambapo kati ya mambo mengine inalenga katika kuandaa
vijana, kabla ya kuingia katika maisha ya ndoa wawe wazazi
wanaowajibika kwa kuinua kiwango cha elimu ya familia.
Sera hii inazungumzia uanzishwaji wa huduma za afya ya uzazi
ambayo itakidhi mahitaji ya vijana na inawahakikishia vijana
kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi bila pingamizi
katika umri wowote.
Baadhi ya watu wanafikiri kuwa huduma za uzazi wa mpango ni
kwa watu walio kwenye ndoa. Hii si kweli, mtu yoyote anaruhusiwa
kutumia huduma za uzazi wa mpango na kupata njia mbalimbali
za uzazi wa mpango. Vijana3 wanafaidika na kuwa na haki sawa
kama watu wazima walio kwenye ndoa. Huduma za kinga kama
vile ushauri juu ya mafunzo ya afya ya uzazi na vilevile kondomu
ni njia za kuzuia mimba zinapatikana bure katika vituo vya afya
vya serikali hapa Tanzania.

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kutumia huduma za afya ya uzazi na njia za uzazi wa mpango?

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!