Mara nyingi utunguaji mimba nje ya mfuko wa uzazi hutokea kwa sababu ya maradhi kwenye via vya uzazi. Maradhi hayo huharibu mirija ya kupitisha mayai. Uharibifu huo hufanya yai lisiweze kufika kwenye mfuko wa mimba na mara nyingi unasababishwa na magonjwa ya zinaa. Kama mwanamke alikuwa na magonjwa ya zinaa uwezekano wa kutunga mimba kwenye mrija wa kupitia mayai unaongezeka.
Ikiwa unafikiri una mimba au iwapo una maumivu chini ya tumbo, unashauriwa uende kliniki kwa ajili ya uchunguzi.
Yai lililorutubishwa linapokaa kwenye mrija wa kupitisha mayai tunasema mimba i imetungwa nje ya mji wa mimbaβectopic pregnancyβ. Kwa maana hiyo basi,, ukuta mwembamba wa mrija utashindwa kutanuka kikamilifu i ili kubeba mimba i inayokua. Mrija hupasuka na damu kutoka. Ikitokea hali hii , lazima mwanamke aende hospitali kwa ajili ya kupasuliwa na pengine kuongezwa damu.

Kwa nini mara nyingine mimba inatungwa kwenye mrija wa kupitisha mayai badala ya kwenye tumbo la uzazi?

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!