Sidebar with Floating Button
AckySHINE Katoliki
AckyShine

Ushauri kwa mtu aliyebakwa

Featured Image

Jambo la kwanza jaribu kumwondoa hofu mwathiriwa na
muliwaze maana amepata jambo la kutisha. Na iwapo mtu
amejeruhiwa sana mpeleke katika kituo cha huduma za afya
kilicho karibu mara moja. Vinginevyo ongozana na rafiki
yako kwenda kituo cha Polisi na kutoa taarifa kuhusu jambo
lililotokea. Polisi watampa fomu ambayo ataipeleka kwa mtoa
huduma. Ni muhimu usijioshe kwa maji kabla hujachunguzwa na
mtaalamu wa afya kwani kufanya hivyo kutaondoa ushahidi wa
kubakwa.
Kwa kuwa kupitia utaratibu huu
inakuwa vigumu mwathiriwa
anahitaji msaada wa karibu
na uangalizi. Mzazi au rafiki
anahitajiwa aongozane naye
na kumsaidia, kwa mfano
kuhakikisha kuwa katika kituo
cha polisi msichana ahojiwe na
polisi wa kike.
Mtu aliyebakwa anahitaji
kusaidiwa kihisia ili aweze
kusahau mawazo na jambo
liliomtokea. Kwa mwathirika, ni
muhimu apewe ushauri nasaha
ili aendelee kujihisi kwamba yeye bado yupo kama mtu wa
kawaida. Ni muhimu pia kuzishughulikia habari za mwathiriwa
kwa siri. Usimweleze kila mtu kilichotokea. Waeleze wale tu
ambao unafikiri wanaweza kusaidia kama daktari, mwalimu au
mzazi. Usiulize maswali ya kwa nini maana inaweza ikaonekana
ni kosa la mwathiriwa. Badala yake zungumza na huyo mtu kwa
utaratibu, polepole, peke yake na mpe uangalifu wa kutosha.
Hakikisha kwamba hutoi lawama yoyote kwa mwathiriwa.
Kubakwa kamwe siyo kosa la mwathiriwa.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Msaada juu ya ukeketaji

Msaada juu ya ukeketaji

Unaweza ukajaribu kuzungumza na wazazi wako kwamba
ukeketaji ni desturi mbaya, na pia unawez... Read More

Je, madhara gani yatawapata wasichana na wavulana wanaojamiiana kwa kutumia sehemu ya haja kubwa?

Je, madhara gani yatawapata wasichana na wavulana wanaojamiiana kwa kutumia sehemu ya haja kubwa?

Tunasema ngono kutumia njia ya haja kubwa pale ambapo uume uliodinda unaingizwa kwenye njia ya haja ... Read More
Njia za Kujua Kama Msichana Anavutiwa na Wewe

Njia za Kujua Kama Msichana Anavutiwa na Wewe

  1. Macho ya msichana Macho ya msichana ni njia moja wapo ya kujua iwapo msichana anavutiwa... Read More

Njia za Kusuluhisha Mazungumzo ya Mgawanyiko katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kusuluhisha Mazungumzo ya Mgawanyiko katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kusuluhisha Mazungumzo ya Mgawanyiko katika Uhusiano wako na Msichana

Kila uhusian... Read More

Jinsi ya kumfanya mpenzi au rafiki yako asiwe na mwingine

Jinsi ya kumfanya mpenzi au rafiki yako asiwe na mwingine

Jambo la muhimu ni kuwasiliana kwa karibu i ili kuelewa mawazo na matatizo ya rafiki yako. Hakiki... Read More

Jinsi ya Kuwa na Siku ya Kumbukumbu ya Kipekee na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Siku ya Kumbukumbu ya Kipekee na Msichana

Kumbukumbu zetu ni muhimu sana katika maisha yetu. Siku ya kumbukumbu ni siku muhimu sana kwa sab... Read More

Je, ni kweli matumizi ya dawa za kulevya ni mojawapo ya sababu zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU)

Je, ni kweli matumizi ya dawa za kulevya ni mojawapo ya sababu zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU)

Dawa za kulevya zenyewe hazisababishi UKIMWI na magonjwa ya zinaa. Lakini utumiaji wa dawa za kul... Read More

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Kusisimua na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Kusisimua na Msichana Wako

Tarehe ya kusisimua inaweza kuwa ngumu kupanga, hasa ikiwa unataka kumpendeza mpenzi wako. Lakini... Read More

Je, ni wanadamu tu ndiyo wameathirika na ualbino?

Je, ni wanadamu tu ndiyo wameathirika na ualbino?

Hapana. Ualbino ni hali
inayoweza kutokea kwa
wanadamu na wanyama wa
kundi la mama... Read More

Jinsi ya Kujikinga na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende

Jinsi ya Kujikinga na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende

Jinsi ya Kujikinga na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende 🌟

Karibu sana kwenye makala hi... Read More

Magonjwa ya zinaa na dalili zake

Magonjwa ya zinaa na dalili zake

Kuna magonjwa mengi tofauti ya zinaa, lakini yale ambayo yameenea sana ni kisonono, kaswende, klamdi... Read More
Jinsi ya Kuanza Mazungumzo na Msichana Unayempenda

Jinsi ya Kuanza Mazungumzo na Msichana Unayempenda

Kuanza mazungumzo na msichana unayempenda inaweza kuwa vigumu, lakini pia inaweza kuwa jambo la k... Read More

📘 About 🔒 Login 📝 Register 📞 Contact