Sidebar with Floating Button
AckySHINE Katoliki
☰
AckyShine

Jinsi ya kutumia kondomu ya kike

Featured Image

Kondomu ya kike inafahamika kwa jina la β€žcareβ€œ na β€œLady Peteta”. Hapa Tanzania hazipatikani sehemu zote na bei yake ni kubwa kidogo.
Kondomu ya kike huingizwa ukeni kabla ya kujamiiana. Kama unatumia kondomu ya kike, chana kwa uangalifu pembezoni mwa pakiti. Kondomu ina pete mbili za plastiki na uwazi upande wa juu. Pete moja imelegea ni ndogo na iko kwa ndani, upande usio na uwazi. Pete ya pili ni kubwa zaidi, imeshikiliwa na iko upande wa tundu. Shikilia kondomu upande uliozibwa na minya pete ya ndani kwa dole gumba na kidole cha pili na cha kati. Mara nyingine inaweza ikakuponyoka, (kuteleza) lakini endelea kujaribu hadi umeiminya vizuri. Tafuta mkao mzuri na ingiza kondomu ya kike. Huku bado unaminya kwa vidole vyako iongoze kondomu ndani ya uke wako. Ukiiachia pete ya ndani itashikilia kondomu ndani ya uke. Sasa ingiza kidole chako kwenye kondomu, sukuma pete mpaka inapogota kwenye mlango wa uzazi.
Kondomu ya kike inaweza kuvaliwa saa kadhaa kabla ya kufanya ngono na pia inaweza kuvuliwa baada ya muda wa kufanyika ngono kupita. Ili kuhakikisha kuwa uume umeingia sehemu husika, msaidie mwenzi wako kuongoza uume kuingia kwenye uke ili usipenye pembeni.
Baada ya kujamiiana, vua kondomu kwa uangalifu. Tupa kondomu iliyotumika kwenye choo cha shimo au uichome. Usitupe kondomu iliyotumika ovyo.
Kama ilivyo kwa kondomu ya kiume, kondomu ya kike itatumika kwa mafanikio zaidi pale ambapo wahusikia wanakuwa na makubaliano na maelewano juu ya matumizi yake.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Ukubwa wa kondomu

Ukubwa wa kondomu

Kuna aina kondomu za ukubwa mbalimbali. Kwa wastani ukubwa wa kondomu unafaa kwa wanaume watu waz... Read More

Je, kuna umuhimu wa kuzungumzia kuhusu ngono/kufanya mapenzi ya salama na kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa?

Je, kuna umuhimu wa kuzungumzia kuhusu ngono/kufanya mapenzi ya salama na kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa?

Je, kuna umuhimu wa kuzungumzia kuhusu ngono/kufanya mapenzi ya salama na kinga dhidi ya magonjwa... Read More

Nimwambie nini mtu anayejaribu kunishawishi nijihusishe na makundi ya watu wanaokunywa pombe na wavutaji sigara?

Nimwambie nini mtu anayejaribu kunishawishi nijihusishe na makundi ya watu wanaokunywa pombe na wavutaji sigara?

Kama umeamua kutovuta sigara wala kunywa pombe ni uamuzi
mzuri sana na wa kiafya. Ni haki ya... Read More

Je, umewahi kujaribu njia mpya za kufurahisha katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, umewahi kujaribu njia mpya za kufurahisha katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, umewahi kujaribu njia mpya za kufurahisha katika ngono/kufanya mapenzi?

Kama wewe ni m... Read More

Je, kisimi cha mwanamke kikisuguliwa kwa vidole atafikia mshindo? Na kuna madhara yoyote ?

Je, kisimi cha mwanamke kikisuguliwa kwa vidole atafikia mshindo? Na kuna madhara yoyote ?

Ni kweli kwamba kuna sehemu za mwili ambazo zikiguswa huleta msisimko mwilini.

Kisimi (au k... Read More

Njia za Kupata Msichana Anayeshiriki Maslahi yako na Malengo

Njia za Kupata Msichana Anayeshiriki Maslahi yako na Malengo

Kupata msichana ambaye anashiriki malengo yako na ana maslahi sawa nawe ni muhimu sana kwa mafani... Read More

Njia za Kujenga Urafiki Mzuri na Msichana Kabla ya Kuwa na Uhusiano

Njia za Kujenga Urafiki Mzuri na Msichana Kabla ya Kuwa na Uhusiano

Karibu ndugu yangu kwenye makala hii ambao inazungumzia njia mbalimbali ambazo utaweza kutumia ku... Read More

Kuna fikra kuwa Albino ni watu wa kawaida je, kisayansi hii ni kweli?

Kuna fikra kuwa Albino ni watu wa kawaida je, kisayansi hii ni kweli?

Hii ni kweli kabisa. Watu wanaoishi na ualbino ni watu wa
kawaida kama binadamu wengine wote... Read More

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Leo tutazungumzia njia za kujenga ushawishi na msichana katika uhusiano. Kujenga ushawishi kunama... Read More

Njia za Kujenga Ukaribu wa Kiroho na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Ukaribu wa Kiroho na Msichana katika Uhusiano

Kujenga ukaribu wa kiroho na msichana katika uhusiano ni jambo muhimu sana. Uhusiano wa kimapenzi... Read More

Je, mwanaume ambaye ana uwezo wa kumwaga shahawa bila shida, inawezekana kwamba ni mgumba?

Je, mwanaume ambaye ana uwezo wa kumwaga shahawa bila shida, inawezekana kwamba ni mgumba?

Ndiyo, mwanaume ambaye ana uwezo wa kumwaga mbegu bila shida anaweza kuwa mgumba. Kutokuwa mgumba... Read More

Jinsi ya kujikinga na ubakaji

Jinsi ya kujikinga na ubakaji

Hata kama utafanya kila kitu usibakwe bado inaweza ikatokea. Ubakaji na unyanyasaji wa ujinsia unawe... Read More
πŸ“˜ About πŸ”’ Login πŸ“ Register πŸ“ž Contact