Hapana, mbu na wadudu wengine hawawezi i kukuambukiza virusi vya UKIMWI kutokana na mfumo wa mii li yao. Virusi vya UKIMWI haviwezi kuishi kwenye mii li yao, kwa sababu siyo mazingira vinavyoyapenda. Virusi vya UKIMWI vinajilisha na kuzaliana katika chembechembe nyeupe za damu, lakini chembechembe za aina hii hazipo katika mwili wa mbu. Kwa hiyo, virusi vya UKIMWI vinakufa mara baada ya mbu kufyonza damu na akingβata mtu mwingine baadaye hakuna hatari ya kuambukizwa.
Thibitisho jingine la ukweli huu ni kwamba sisi sote tungekuwa tumebeba virusi vya UKIMWI kama mbu angelikuwa anaambukiza kwa sababu sisi sote tunaishi katika mazingira yenye mbu na karibu na watu wengine.

Je, ninaweza kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa kuumwa na mbu?

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!