Wakati wa kujifungua, uke wa mwanamke mzima hupanuka kuanzia kipenyo cha sentimeta kumi mpaka kumi na mbili i i ili kuruhusu kichwa cha mtoto kupita. Kwa kawaida, mwanamke anayejifungua, uke na mlango wa mfuko wa uzazi hupanuka vya kutosha.
Kwa wasichana wa umri mdogo, kuzaa mtoto kunaweza kukaleta matatizo, kwa sababu viungo vyake vya uzazi bado ni vidogo na havina nguvu ya kutosha. Mara kwa mara wasichana wanapata uchungu wa muda mrefu kwa sababu fupanyonga ni nyembamba hivyo kutoruhusu mtoto kupita kiurahisi na kwa haraka. Mara nyingine hata i inabidi kufanyiwa operesheni i i ili kumtoa mtoto.
Wasichana ambao hawapati huduma ya wataalamu ambao wanaweza kugundua matatizo ya msichana na mtoto haraka wakati wa kujifungua, mara nyingi wanapata ulemavu wa kudumu. Yaani ulemavu wa kuharibika ama njia ya mkojo au njia ya haja kubwa au hata njia zote mbili kwa pamoja. Uharibifu wa njia hizi unajulikana kana fistula, unamfanya mama kushindwa kuzuia haja kubwa au ndogo hivyo kuvuja ovyoovyo kwa kupitia ukeni.
Wakati mwingine msichana na mtoto ambaye hajazaliwa hufa wakati wa kujifungua, kwa sababu wanakuwa hawajapata huduma kutoka kwa mtu mwenye stadi za kutosha.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!