Vijana wengi wanajikuta wanatumbukia katika matatizo mazito kama kupata mimba mapema, utoaji wa mimba, magonjwa ya zinaa pamoja na maambikizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI, kwa sababu wanapokea zawadi bila ya kujiuliza lengo la zawadi hizo.
Wanaume wengi wanatumia fedha kuwahadaa wasichana na wasichana wengine wamezoea kupata fedha hizo kukidhi mahitaji yao ya maisha. Jambo hili linaweza pia kuwapata wavulana kwani kwa maana kwamba wanawake watu wazima hujaribu kuwatongoza wavulana wadogo. Hivyo basi ni muhimu kwa wasichana na wavulana wote kwa pamoja kuwa waangalifu sana na zawadi zinazotolewa. Ni vema wakati wote ujiulize nini lengo la zawadi hiyo.
Pia fikiria kuhusu faida na hasara ya kujamiiana kila unapokutana na vishawishi mbalimbali. Ukikumbuka madhara ambayo unaweza kuyapata itakupa nguvu na msimamo wa kusema βhapanaβ na kujiepusha na vishawishi.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!