Sidebar with Floating Button
AckySHINE Katoliki
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kuweka Kipaumbele cha Ukaribu na Kuunga Mkono Maendeleo ya Kila Mwanafamilia

Kuweka Kipaumbele cha Ukaribu na Kuunga Mkono Maendeleo ya Kila Mwanafamilia

Kuweka kipaumbele cha ukaribu na kuunga mkono maendeleo ya kila mwanafamilia ni jambo muhimu sana... Read More

Njia za Kujenga Ushirikiano wa Karibu na Kuweka Nafasi ya Mazungumzo katika Familia

Njia za Kujenga Ushirikiano wa Karibu na Kuweka Nafasi ya Mazungumzo katika Familia

Katika familia, ushirikiano wa karibu na mazungumzo ni muhimu sana kujenga uhusiano mzuri kati ya... Read More

Jinsi ya Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu mipango ya kujitolea na kusaidia wengine

Jinsi ya Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu mipango ya kujitolea na kusaidia wengine

Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu mipango ya kujitolea na kusaidia wengine ni njia nzuri ya kuimarish... Read More
Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipaka ya faragha

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipaka ya faragha

Kujenga na kudumisha mipaka ya faragha katika uhusiano ni muhimu kwa usalama, heshima, na ustawi wa ... Read More
Jinsi ya Kukabiliana na Changamoto za Kifedha katika Familia

Jinsi ya Kukabiliana na Changamoto za Kifedha katika Familia

Karibu katika makala hii ambayo inalenga kuzungumzia jinsi ya kukabiliana na changamoto za kifedh... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Kama kijana, kuna wakati unaweza kukutana na msichana na unataka kuzungumza naye kwa kina lakini ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kudumisha usawa wa kijinsia na haki za wanawake

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kudumisha usawa wa kijinsia na haki za wanawake

Jinsi ya Kusaidiana na Mpenzi Wako katika Kudumisha Usawa wa Kijinsia na Haki za Wanawake

... Read More

Jinsi ya Kupenda na Kuunga Mkono Watoto Walemavu: Kuunda Mazingira ya Ukuaji na Furaha

Jinsi ya Kupenda na Kuunga Mkono Watoto Walemavu: Kuunda Mazingira ya Ukuaji na Furaha

Siku zote, kama wazazi au watunzi wa watoto, tunapaswa kujifunza jinsi ya kupenda na kuunga mkono... Read More

Kukabiliana na Changamoto za Mahusiano: Mazoea Bora na Mbinu

Kukabiliana na Changamoto za Mahusiano: Mazoea Bora na Mbinu

Kukabiliana na Changamoto za Mahusiano: Mazoea Bora na Mbinu

Mahusiano ni sehemu muhimu sa... Read More

Jinsi ya kushirikiana na mke wako katika Kulea Watoto

Jinsi ya kushirikiana na mke wako katika Kulea Watoto

Kushirikiana na mke wako katika kulea watoto ni muhimu katika kujenga familia yenye nguvu na yenye u... Read More
Kuweka Kipaumbele cha Kuendeleza Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano

Kuweka Kipaumbele cha Kuendeleza Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano

Kuweka Kipaumbele cha Kuendeleza Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano

Kuwa na mahusiano... Read More

Upendo na Kufanya Mapenzi: Tofauti na Uhusiano wao

Upendo na Kufanya Mapenzi: Tofauti na Uhusiano wao

  1. Upendo na kufanya mapenzi ni vitu viwili tofauti katika uhusiano. Upendo ni hisia za ki... Read More

📘 About 🔒 Login 📝 Register 📞 Contact