Miaka zaidi ya 3000 iliyopita katika mji wa Yeriko alikuwepo mwanamke mmoja kahaba, jina lake Rahabu. Huyu mwanamke aliwaokoa wapelelezi wa Israel waliotumwa kwenda kufanya uchunguzi ktk nchi yao.
Wakati wana wa Israel wanatoka Misri kuelekea nchi ya Kaanani, Mungu aliwaahidi kuwapa mji wa Yeriko. Kwahiyo walipofika ng'ambo ya mto Yordani, Yoshua akatuma wapelezi wawili kwenda kuipeleleza Yeriko kabla wana wa Israel kuivamia na kuitwaa. Wale wapelelezi walipofika mji wa Yeriko mfalme akapelekewa taarifa kuwa kuna watu wawili wameingia kuipeleleza nchi.
Kwahiyo mfalme akaagiza wakamatwe na wauawe. Wale wapelelezi wakaingia ktk nyumba ya mwanamke kahaba aitwaye Rahabu akawaficha darini. Akawafunika kwa mabua ya kitani. Wale askari walipofika na kumuuliza Rahabu kwamba wako wapi waisrael wawili walioingia humu ndani, Rahabu akajibu kuwa wameondoka.
Akasema ni kweli waliingia ktk nyumba yangu lakini walitoka kabla lango la mji halijafungwa. Akawaambia wafuateni haraka kabla hawajafika mbali. Wale askari wakatoka kuwafuata wale wapelelezi hadi katika vilima vya nje ya mji lakini wasiwaone. Ilipofika usiku Rahabu akawashusha darini wale wapelelezi na kuwaelekeza namna ya kutoroka mji wa Yeriko. Akawaelekeza wapite njia nyingine tofauti na ile waliyoiendea wale askari. Akawashusha kupitia dirishani ili watu wa mji ule wasiwaone.
Kwa ukarimu aliowatendea wale wapelelezi wakaweka agano nae kwamba siku wana wa Israel wakija kuiangamiza Yeriko, BWANA ataiponya nyumba ya Rahabu na ndugu zake wote. Ili kutimiza agano hilo wale wapelezi wakamwambia Rahabu weka kamba nyekundu katika dirisha lako kama alama, ili jeshi la Israel liltakapouteketeza mji nyumba yako isiangamizwe.
Yoshua 2:17 &18 "Wale wapelelezi wakamwambia Rahabu, Sisi tunataka tusiwe na hatia kwa ajili ya kiapo hiki ulichotuapisha. Angalia, tutakapoingia katika nchi hii, funga kamba hii nyekundu katika dirisha hili ulilotuteremshia; nawe uwakusanye nyumbani mwako, baba yako, mama yako, na ndugu zako, na watu wote wa nyumba ya baba yako."
Rahabu akafanya hivyo, na siku Jeshi la Israel lilipovamia Mji wa Yeriko ili kuuteketeza, Rahabu na ndugu zake walipona.
Yoshua 6:23 &24 "Basi wale vijana wapelelezi wakaingia, wakamtoa Rahabu, na baba yake, na mama yake, na ndugu zake, na vitu vyote walivyokuwa navyo, wakawatoa na jamaa zake wote pia; wakawaweka nje ya matuo ya Israeli. Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake…"
MORAL OF THE STORY.!
Habari hii ina mengi ya kutufundisha lakini leo nataka nikufundishe kuhusiana na siri ya kamba nyekundu ambayo Rahabu aliiweka katika dirisha lake na jinsi ilivyomuokoa.
Rahabu hakua mtakatifu, hakuwa mteule wa Mungu wala hakuwa kizazi cha Israel. Alikua mwanamke wa mataifa, tena kahaba. Hakuwa mwema sana machoni pa Mungu. Lakini aliokoka kwa sababu ya "kamba nyekundu" dirishani mwake. Pengine wapo maaskofu, wachungaji, mitume au manabii walioangamizwa, lakini kahaba Rahabu akaokolewa yeye na ndugu zake licha ya kwamba alikua kahaba. Siri ni "kamba nyekundu" dirishani mwake.
Jiulize je wewe unayo kamba nyekundu? Kuna watu katika maisha wanaonekana wenye dhambi, wachafu, dhaifu au wasiofaa, lakini Mungu huwanyanyua na kuwabariki na kuwaacha wale tunaodhani ni watakatifu au wenye haki. Mungu anaangalia "kamba nyekundu". Unaweza kuwa mtakatifu lakini huna "kamba nyekundu" itakayomfanya Mungu akurehemu.
Unaweza kuwa umemaliza masomo yako na umefaulu vizuri, lakini kila unapoomba kazi huitwi hata kwenye usaili, na ukiitwa hupati kazi, miaka inazidi kwenda. Unaamua kwenda kwenye maombi. Kila siku unafanya maombi lakini bado hufanikiwi. Unajiuliza tatizo liko wapi. Unaji-asses na kuona hakuna tatizo mahali. Kumbe huna "kamba nyekundu"
Au unaweza kuwa una biashara yako lakini haifanikiwi. Hupati wateja. Umehitahidi kwa kila hali lakini bado huoni faida. Unadhani tatizo labda Mungu amekuacha. Unaamua kuwa mtu wa maombi. Unazunguka makanisa mbalimbali kuonbewa lakini bado haufanikiwi. Kumbe huna "kamba nyekundu".
"Kamba nyekundu" imekuwa siri ya mafanikio ya watu wengi bila kujalisha mahusiano yao kiroho na Mungu. Bila kujalisha kama ni wakristo au si wakristo. Kamba nyekundu imewasaidia hata wenye dhambi kubarikiwa. Rahabu alikua kahaba lakini yeye na ndugu zake waliokolewa kwa sababu ya "kamba nyekundu".
Je kamba nyekundu ni nini? Kamba nyekundu ni mfumo wako wa maisha; jinsi unavyoishi na unayowatendea watu wengine, hasa "wateule" wa Mungu.
Kuna wakati Mungu huamua kukubariki si kwa sababu wewe ni mwema sana, bali kwa sababu kuna watu wema wanaoomba kwa ajili yako. Inawezekana tangu uanze kuomba, maombi yako hayajawahi kufika kwa Mungu lakini unabarikiwa, kwa sababu ya kamba nyekundu.
Kuna watu ambao ni "wateule" wa Mungu, kwahiyo kadri unavyowatendea mema hao watu baraka zinakuja kwako "automatically" hata kama wewe si mkristo. Rahabu aliwatendendea mema wapelelezi wa Israel baraka zikaenda kwake "automatically" bila kujalisha kwamba alikua kahaba.
Yatima, wajane, maskini, wazee, wagonjwa na wengine wenye uhitaji ni wateule wa Mungu. Kwahiyo ukiwatendea mema watu hawa baraka zinakuja kwako hata kama wewe ni mwenye dhambi.
Kwa mfano kama kuna watoto yatima unawasomesha, au kuna wajane unawasaidia mahitaji yao, au wagonjwa unawasaidia matibabu, si rahisi Mungu kuondoa mkono wake wa baraka kwako hata kama wewe ni mwenye dhambi. Mungu akiondoa baraka kwako watu wake watateseka.
Wale yatima, wajane, wagonjwa ambao wewe ni msaada kwao kila wakiomba Mungu huongeza baraka kwako ili uzidi kuwahudumia. Inawezekana maombi yako hayafikagi kwa Mungu lakini unabarikiwa kwa sababu ya maombi ya hao unawaosaidia.
Kuna wakati Mungu anaweza kuamua kuzipiga dhoruba biashara za wenzako, lakini ya kwako ikasimama imara. Si kwa sababu wewe ni mwema sana, bali kwa sababu kuna watu wanamlilia Mungu kwa ajili yako. Kuna wanategemea ada za shule kwenye hiyo biashara yako. Kuna watu wanategemea pesa za matibabu kwenye biashara yako. Kwa hiyo Mungu akiyumbisha biashara yako atakua anawaumiza watu hao. So ili asiwaumize anaamua kukuaacha. Hiyo ni kamba nyekundu.!
Kuna wakati wenzio wakifanya makosa madogo kazini wanafukuzwa kazi, lakini unajishangaa wewe umefanya makosa makubwa na hufukuzwi. Si kwa sababu una bahati sana. Ni kamba nyekundu. Kuna watu walioko nyuma yako ambao ni wateule wa Mungu. Kuna yatima wanategemea kulipiwa ada kwa mshahara wako, kuna wagonjwa wanategemea kusaidiwa hela za matibabu kwenye mshahara wako, kuna wajane wanategemea hela ya kuishi kutoka kwako. Kwahiyo Mungu akikuadhibu anakua amewaadhibu na wao. Kwahiyo ili wapone inabidi akulinde hata kama umefanya kosa kazini. Unashangaa tu kesi imeisha hata kwa namna ambayo hujui. Hiyo ni kamba nyekundu.!
Kuna mtu ambaye ni maskini wa kutupwa hana hata uwezo wa kununua sukari. Lakini anamuomba Mungu kwa imani kuwa ampe sukari aweze kunywa chai kila siku. Kwa kuwa huyo maskini huwa anapata sukari kutoka kwako, Mungu atazidi kukubariki ili uendelee kumhudumia huyo maskini. Hiyo ni Kamba nyekundu.!
Kamba nyekundu ilimuokoa Rahabu na ndugu zake licha ya kwamba alikua kahaba. Jiulize wewe una kamba nyekundu? Je kuna watu wako nyuma yako ambao Mungu akiwaangalia anakubariki, anakuokoa hata kama upo kwenye hatari?
Kama unamsomesha mwanao shule ya "mamilioni" kwa mwaka wakati mtoto wa jirani yako hana hata uniform za kuendea shule, au unatumia "mamilioni" kwa pombe na starehe wakati kuna wagonjwa wanaokufa kwa kukosa panadol, siku Mungu akitaka kukuadhibu hajiulizi mara mbili maana huna "kamba nyekundu" nyuma yako.
Lakini yule anayesaidia wenye uhitaji, kama yatima, wagonjwa, wazee, wajane,walemavu, au maskini atazidi kubarikiwa tu hata kama ni mwenye dhambi, maana anayo kamba nyekundu.
Hii ni kwa sababu Mungu akitaka kumuadhibu, kabla hajamtizama yeye anatizama kwanza yatima walioko nyuma yake anaowasaidia, anatizama wagonjwa wanaomtegemea kwa matibabu, anatizama wajane. Anaona akimuadhibu, atakuwa ameadhibu na hao wanaomtegemea. Kwa hiyo anaamua kumuacha.
Hii ina maana kuwa baraka na utakatifu ni vitu viwili tofauti. Unaweza usiwe mtakatifu lakini Mungu akakubariki na akakulinda. Unaweza kubarikiwa si kwa sababu unastahili, bali kwa sababu kuna "wanaostahili" wapo nyuma yako wakikupigania kwa baba yao (Yehova). Ndio maana kuna watu wengi wasio Wakristo wanabarikiwa kila siku hata kama hawamjui Mungu. Ni kwa sababu wana "kamba nyekundu".
Malisa G.J
Moses Kipkemboi (Guest) on June 4, 2024
Mungu akubariki!
Robert Okello (Guest) on May 10, 2024
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Nora Kidata (Guest) on January 19, 2024
Nguvu hutoka kwa Bwana
Mary Kendi (Guest) on July 15, 2023
Katika imani, yote yanawezekana
Peter Mbise (Guest) on June 26, 2023
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Peter Tibaijuka (Guest) on June 1, 2023
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Janet Sumaye (Guest) on December 15, 2022
Mwamini katika mpango wake.
Joy Wacera (Guest) on December 8, 2022
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Rose Mwinuka (Guest) on June 6, 2022
Mungu ni mwema, wakati wote!
Raphael Okoth (Guest) on May 6, 2022
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Ruth Kibona (Guest) on February 22, 2022
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Dorothy Majaliwa (Guest) on March 28, 2021
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Samson Tibaijuka (Guest) on January 27, 2021
Rehema hushinda hukumu
Alice Mwikali (Guest) on December 31, 2020
Dumu katika Bwana.
Lucy Wangui (Guest) on December 14, 2020
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Mary Kidata (Guest) on September 17, 2020
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Grace Njuguna (Guest) on September 15, 2020
Nakuombea 🙏
Nancy Akumu (Guest) on June 8, 2020
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
David Chacha (Guest) on December 20, 2019
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Lucy Wangui (Guest) on December 10, 2019
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Esther Nyambura (Guest) on November 30, 2019
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Monica Lissu (Guest) on October 3, 2019
Endelea kuwa na imani!
Philip Nyaga (Guest) on September 24, 2019
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Paul Ndomba (Guest) on September 21, 2019
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Patrick Mutua (Guest) on August 1, 2019
Sifa kwa Bwana!
Nancy Kawawa (Guest) on June 11, 2019
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
James Malima (Guest) on March 31, 2019
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Diana Mallya (Guest) on March 6, 2019
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Wilson Ombati (Guest) on January 4, 2019
Mwamini Bwana; anajua njia
David Kawawa (Guest) on August 6, 2018
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
John Kamande (Guest) on August 6, 2018
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Moses Mwita (Guest) on June 10, 2018
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Dorothy Nkya (Guest) on May 21, 2018
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Andrew Mchome (Guest) on March 29, 2018
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Monica Lissu (Guest) on January 22, 2018
Neema na amani iwe nawe.
Joseph Njoroge (Guest) on September 22, 2017
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Jane Muthoni (Guest) on August 31, 2017
Baraka kwako na familia yako.
Janet Mwikali (Guest) on July 16, 2017
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Christopher Oloo (Guest) on April 12, 2017
Tumaini ni nanga ya roho
Samson Tibaijuka (Guest) on April 9, 2017
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Samuel Omondi (Guest) on March 5, 2017
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Stephen Kikwete (Guest) on October 19, 2016
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
David Chacha (Guest) on June 19, 2016
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Victor Sokoine (Guest) on May 5, 2016
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Hellen Nduta (Guest) on March 3, 2016
Rehema zake hudumu milele
Joyce Aoko (Guest) on January 31, 2016
Imani inaweza kusogeza milima
Raphael Okoth (Guest) on January 1, 2016
Neema ya Mungu inatosha kwako
Esther Nyambura (Guest) on October 15, 2015
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
George Tenga (Guest) on August 18, 2015
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Miriam Mchome (Guest) on May 15, 2015
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia