Siku moja jioni katika mji flani, kulikuwa na basi likisafiri kutoka mji huo kuelekea mji mwingine. Lilikuwa ni basi kubwa na limejaa abiria. Wakati wakiendelea na safari, ghafla, mvua kubwa iliyoambatana na radi ikaanza kunyesha. Dereva hakuogopa, wala abiria, wakaendelea na safari. Mara wakati wanaenda, radi ikaanza kufuatilia gari. Kila wakienda, radi inapiga karibu na basi kana kwamba inalifuata basi. Likisimama, radi inapiga pembezoni mwa basi.
Dereva kuona hivyo, akasimamisha gari mita 5 kutoka kwenye mtiβ¦ Akawaambia abiria, "Humu ndani ya basi, kuna mtu ambaye leo ni siku yake ya kufa, tena kufa kwa radi. Ili tusife wote, nataka kila abiria ashuke akaguse mti ili anayepigwa na radi, apigwe wengine wasife kwa ajili yake. "Abiria wakitetemeka, wakaanza kushuka mmoja mmoja. Unaenda unagusa mti , kisha unarudi kwenye basi. Abiria wote pamoja na dereva mmoja mmoja, wakaenda, wakagusa mti na kurudi bila dhara lolote! Akawa kabaki abiria mmoja tu, ambaye alikuwa hajagusa mti. Abiria wote kwa macho ya hasira wakamwambia akaguse mti. Akawa anaogopa kufa. Akagoma. Wakamlazimisha kwa nguvu sana na kumtoa njeβ¦β¦. β¦β¦.. Yule abiria akiwa amefumba macho, akaenda akagusa mti. Hamadi bin Vuu! Radi kali sana ikalipiga basi, abiria na wote waliokuwamo, wakafa palepale. Kumbe uwepo wake ndio ulikuwa unazuia abiria wengine wasidhurike na radi.
MAFUNZO
1. Unapofanikiwa, huwezi jua uwepo wa nani umefanikisha mafanikio yako, usichukue sifa zote peke yako. Wapatie na wengine bila kumsahau MUNGU.
2. Unaweza kujiona huna thamani sehemu ulipo, iwe kwenye kundi la WhatsApp, darasani, kazini, kwenye basi, barabarani bila kujua kama uwepo wako ni wa muhimu sana kwa ustawi wa wengine.
3. Usimtenge wala kumnyanyasa mtu au jirani yako, huwezi jua uwepo wake ni kwa ajili gani.
Anna Mchome (Guest) on July 8, 2024
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Joyce Aoko (Guest) on May 4, 2024
Dumu katika Bwana.
Miriam Mchome (Guest) on March 11, 2024
Endelea kuwa na imani!
Kevin Maina (Guest) on February 29, 2024
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Samuel Were (Guest) on October 30, 2023
Neema ya Mungu inatosha kwako
Esther Nyambura (Guest) on October 22, 2023
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Nancy Kabura (Guest) on September 18, 2023
Mungu akubariki!
James Mduma (Guest) on September 9, 2023
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Charles Mrope (Guest) on August 29, 2023
Rehema zake hudumu milele
Grace Njuguna (Guest) on August 22, 2023
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Charles Mboje (Guest) on May 29, 2023
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Agnes Lowassa (Guest) on October 30, 2022
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Margaret Anyango (Guest) on September 4, 2022
Tumaini ni nanga ya roho
Sarah Achieng (Guest) on May 25, 2022
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Agnes Njeri (Guest) on April 28, 2022
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Elizabeth Mrope (Guest) on April 11, 2022
Imani inaweza kusogeza milima
Stephen Malecela (Guest) on September 30, 2021
Neema na amani iwe nawe.
Patrick Mutua (Guest) on June 16, 2021
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
John Lissu (Guest) on June 13, 2021
Nguvu hutoka kwa Bwana
Janet Wambura (Guest) on December 9, 2020
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Chris Okello (Guest) on December 3, 2020
Mwamini Bwana; anajua njia
Hellen Nduta (Guest) on November 29, 2020
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Rose Kiwanga (Guest) on November 16, 2020
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Janet Sumaye (Guest) on August 5, 2020
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Grace Minja (Guest) on May 24, 2020
Mungu ni mwema, wakati wote!
John Malisa (Guest) on December 7, 2019
Baraka kwako na familia yako.
Bernard Oduor (Guest) on July 10, 2019
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Joseph Kitine (Guest) on July 8, 2019
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Lydia Wanyama (Guest) on June 22, 2019
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Michael Mboya (Guest) on May 17, 2019
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Elizabeth Mrema (Guest) on April 27, 2019
Rehema hushinda hukumu
Kevin Maina (Guest) on January 25, 2019
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Lydia Mahiga (Guest) on September 5, 2018
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Janet Mbithe (Guest) on May 24, 2018
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
David Musyoka (Guest) on November 10, 2017
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
David Ochieng (Guest) on August 9, 2017
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Janet Wambura (Guest) on August 7, 2017
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Lucy Mushi (Guest) on April 21, 2017
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Samuel Omondi (Guest) on April 21, 2017
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
David Nyerere (Guest) on November 20, 2016
Katika imani, yote yanawezekana
Josephine Nekesa (Guest) on November 12, 2016
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Anna Malela (Guest) on September 29, 2016
Nakuombea π
Janet Mwikali (Guest) on July 2, 2016
Sifa kwa Bwana!
Paul Ndomba (Guest) on June 16, 2016
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Linda Karimi (Guest) on November 29, 2015
Mwamini katika mpango wake.
Monica Lissu (Guest) on October 16, 2015
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Nancy Akumu (Guest) on October 13, 2015
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
John Lissu (Guest) on September 13, 2015
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Nancy Kawawa (Guest) on August 16, 2015
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Susan Wangari (Guest) on June 19, 2015
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu