Sidebar with Floating Button
AckySHINE Katoliki
โ˜ฐ
AckyShine

Maswali na Majibu kuhusu Sanamu katika Kanisa Katoliki

Featured Image

Je sanamu zimekatazwa?


Sanamu hazijakatazwa, ila tunaziheshimu kwa sababu zinatukumbusha Mungu na Watakatifu. (Kut 25:18-22).

18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku. 20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. Kutoka 25 :18-22.

Vile vile Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli Wachonge sanamu ya nyoka na yeyote atakayeumwa na nyoka akiiangalia atapona.







Mfano wa sanamu takatifu ni zipi?


Sanamu ya Bikira Maria, Mtoto Yesu, Mt. Yosefu, Moyo wa Yesu na za Watakatifu.







Ni nini maana ya kuabudu sanamu?


Kuabudu sanamu ni kukipa kiumbe chochote heshima au upendo anaostahili Mungu peke yake.







Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?


Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)

Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;

"18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.ย (Kutoka 25 :18-22.)"

Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?

Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.

"BWANA akamwambia Mose, โ€œTengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.โ€™โ€™ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi."ย (Hesabu 21:8-9).

Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.

Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.

Sanamu au picha sio haramu bali maana ya hiyo sanamu au picha ndio inaiharamisha.


Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.

Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.

Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.

Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.

Kumbukaย kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwaย "Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake", kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.

Tofauti ya Sanamu za Kikatoliki na za kipagani ni Kwamba,


Sanamu za Kipagani:ย Sanamu hizi huchukuliwa kama Mungu na huabudiwa na kutolewa Sadaka kama Mungu Mwenyewe.


Sanamu za Kikatoliki:ย Sanamu hizi huchukuliwa kama ishara ya kile inachokiwakilisha, haiabudiwi kamwe bali inaheshimiwa tuu.


Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.ย (Kutoka 25 :22).ย Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.

Jifunze kupitia Sanduku la Agano na Msalaba wa Yesu


Kwenye Agano la kale:ย Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hichoย Kutoka 25:10-22.ย Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.

Kwenye Agano jipya:ย Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.

FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.

Kwa nini tunasali mbele ya Picha/Sanamu na Hasa kufanya Ishara ya msalaba?


Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.

Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.

Kwa nini watu wanabusu picha na sanamu?


Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.







Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vina maana gani?


Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vinamaanisha tu sifa fulani: k.mf. macho ujuzi wake, mikono uwezo wake, mabawa ulinzi wake, n.k. โ€œRoho haina mwili na mifupaโ€ (Lk 24:39).







Je, ni halali kuheshimu sanamu?


Ndiyo, ni halali kuheshimu sanamu kama viwakilishi vya Yesu, Mama yake na watakatifu wake, ambao zinaleta sura zao.

Kwa msingi huo walimsihi Yesu โ€œwaguse hata pindo la vazi lake tu. Na wote waliogusa wakaponywa kabisaโ€ (Math 14:36).

โ€œMimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote il msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristoโ€ (Gal 6:14).

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Grace Mligo (Guest) on July 14, 2024

Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi

Francis Mtangi (Guest) on July 3, 2024

Tembea kwa imani, si kwa kuona

David Nyerere (Guest) on May 12, 2024

Katika imani, yote yanawezekana

Mariam Hassan (Guest) on March 17, 2024

Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu

Joyce Mussa (Guest) on December 30, 2023

Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia

Christopher Oloo (Guest) on November 10, 2023

Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia

Catherine Naliaka (Guest) on November 7, 2023

Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni

Robert Ndunguru (Guest) on June 6, 2023

Mwamini Bwana; anajua njia

Miriam Mchome (Guest) on May 31, 2023

Mungu ni mwema, wakati wote!

Ann Wambui (Guest) on May 19, 2023

Hauko peke yako; Mungu yuko nawe

John Mwangi (Guest) on April 26, 2023

Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako

Irene Makena (Guest) on April 2, 2023

Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu

Alex Nakitare (Guest) on March 5, 2023

Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia

Sarah Karani (Guest) on March 4, 2023

Mwamini katika mpango wake.

James Malima (Guest) on February 6, 2023

Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote

John Malisa (Guest) on September 25, 2022

Bwana yuko karibu na wote wanaomwita

Bernard Oduor (Guest) on August 5, 2022

Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake

Anthony Kariuki (Guest) on November 27, 2021

Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha

Christopher Oloo (Guest) on October 3, 2021

Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika

Charles Mchome (Guest) on September 20, 2021

Ahadi za Mungu ni za kweli daima

Francis Mtangi (Guest) on August 24, 2021

Mungu akubariki!

Isaac Kiptoo (Guest) on August 18, 2021

Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao

Faith Kariuki (Guest) on June 15, 2021

Endelea kuwa na imani!

Michael Mboya (Guest) on May 24, 2021

Upendo wa Mungu haukosei kamwe.

Peter Mwambui (Guest) on October 29, 2020

Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha

Thomas Mtaki (Guest) on August 26, 2020

Rehema zake hudumu milele

John Mushi (Guest) on July 31, 2020

Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini

Irene Makena (Guest) on March 9, 2020

Nakuombea ๐Ÿ™

Elizabeth Malima (Guest) on December 1, 2019

Nguvu hutoka kwa Bwana

Alex Nakitare (Guest) on October 19, 2019

Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi

Joseph Kiwanga (Guest) on July 4, 2019

Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe

Monica Nyalandu (Guest) on June 6, 2019

Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi

Monica Adhiambo (Guest) on December 25, 2017

Neema na amani iwe nawe.

Chris Okello (Guest) on October 13, 2017

Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia

Miriam Mchome (Guest) on March 31, 2017

Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima

Stephen Kangethe (Guest) on March 28, 2017

Sifa kwa Bwana!

Ann Awino (Guest) on November 22, 2016

Kwa Mungu, yote yanawezekana

Nancy Kawawa (Guest) on September 22, 2016

Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine

Sarah Achieng (Guest) on August 30, 2016

Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako

Irene Akoth (Guest) on August 14, 2016

Rehema hushinda hukumu

Grace Majaliwa (Guest) on August 5, 2016

Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe

Nora Lowassa (Guest) on June 21, 2016

Dumu katika Bwana.

Anna Kibwana (Guest) on May 22, 2016

Wakati wa Mungu ni kamilifu

Nancy Kabura (Guest) on April 1, 2016

Baraka kwako na familia yako.

Joseph Njoroge (Guest) on March 6, 2016

Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi

Agnes Njeri (Guest) on January 3, 2016

Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida

Joseph Njoroge (Guest) on December 21, 2015

Tumaini ni nanga ya roho

Edwin Ndambuki (Guest) on July 23, 2015

Imani inaweza kusogeza milima

Andrew Mchome (Guest) on July 22, 2015

Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu

Betty Cheruiyot (Guest) on July 3, 2015

Neema ya Mungu inatosha kwako

Related Posts

Amri ya Kwanza ya Mungu: Mambo Muhimu ya Kuzingatia

Amri ya Kwanza ya Mungu: Mambo Muhimu ya Kuzingatia

Katika amri ya kwanza ya Mungu tumeamriwa nini?... Read More

Je, Kanisa Katoliki linatambua na kufundisha umuhimu wa kuishi imani katika matendo mema?

Je, Kanisa Katoliki linatambua na kufundisha umuhimu wa kuishi imani katika matendo mema?

Je, Kanisa Katoliki linatambua na kufundisha umuhimu wa kuishi imani katika matendo mema? Jibu ni... Read More

Maswali na Majibu kuhusu Malaika

Maswali na Majibu kuhusu Malaika

Read More

Mambo ya Msingi kufahamu kuhusu Ndoa ya Kikatoliki

Mambo ya Msingi kufahamu kuhusu Ndoa ya Kikatoliki

Read More
Je, Kanisa Katoliki linawahimiza waamini kuheshimu na kutii viongozi wa kidini na maaskofu?

Je, Kanisa Katoliki linawahimiza waamini kuheshimu na kutii viongozi wa kidini na maaskofu?

Je, Kanisa Katoliki linawahimiza waamini kuheshimu na kutii viongozi wa kidini na maaskofu? Jibu ... Read More

Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wa sala katika maisha ya Kikristo?

Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wa sala katika maisha ya Kikristo?

Sala ni sehemu muhimu katika maisha ya Kikristo. Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wa... Read More
Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu Maandiko Matakatifu?

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu Maandiko Matakatifu?

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu Maandiko Matakatifu?

Kanisa Katoliki linaamini kwa... Read More

Amri za Kanisa: Mambo ya Muhimu kujua na Kuzingatia

Amri za Kanisa: Mambo ya Muhimu kujua na Kuzingatia

Amri za Kanisa ni zipi?

Katika Amri ya Sita na Tisa Mungu ametuamuru nini?Read More

Maswali na Majibu kuhusu Biblia

Maswali na Majibu kuhusu Biblia

Read More