Kwanza Mungu aliumba nini?
Kwanza Mungu aliumba Malaika (Kol 1:16)
Malaika ni viumbe gani?
Malaika ni viumbe vya Mungu vilivyo roho tu wenye akili na utashi. (Zab 91:11, Ebr 1:7, Ufu 12:7-9)
Mungu aliumba Malaika katika hali gani?
Mungu aliumba Malaika katika hali njema na heri kubwa.
Malaika wote walidumu katika hali njema na ya heri?
Siyo, Malaika wengine walikosa kwa kumkaidi Mungu, Wakatupwa Motoni.
Ndio Mashetani ambao Mkubwa wao ni Lusiferi. (Yoh 8:44, Uf 12:7-9)
Kwa nini Mungu ameumba Malaika?
Mungu ameumba Malaika ili wamtukuze, wafurahi naye Mbinguni, na wawe matarishi wake kwa wanadamu. (Tob 12:12, Lk 16:22)
Malaika wema kazi yao ni nini?
Malaika wema kazi yao ni kutuombea, kutumwa na Mungu kwetu, na wanatulinda kama Malaika wetu Walinzi. (Ebr 13:2)
Kila Mwanadamu anaye Malaika wake wa kumlinda?
Ndiyo, Kila Mwanadamu anaye Malaika wake wa kumlinda ndiye Malaika Mlinzi. (Mt. 18:10)
Malaika Walinzi wanatutendea nini?
Malaika walinzi hutupenda, hutuongoza, na kutulinda roho na mwilini (Zab 90:11)
Je Malaika wote ni sawa?
Hapana. Malaika wote sio sawa, maana kuna;
1. Malaika wakuu
2. Malaika wanaomtumikia Mungu Mbinguni yaani Makerubi na Maserafi
3. Malaika Walinzi
Malaika wakuu wako watatu ambao ni?
Malaika wakuu wako watatu: Mikaeli, Raphaeli na Gabrieli (Dn 10:13, Tobiti 12:15, Lk 1:26)
Makao ya shetani ni wapi na anatamani nini?
1. Mashetani kazi yao ni kuteswa Motoni
2. Hutaka kutudhuru roho na mwili na kutupoteza milele (1 Petro 5:8, Yoh 8:44)
Kisha kuumba Malaika Mungu aliumba nini?
Kisha kuumba Malaika Mungu aliumba Mbingu na dunia, na viumbe vingine vingi vyenye kuonekana mimea na watu. (Mwanzo 1;31)
Viumbe vyenye hiari ni vipi?
Malaika na watu ndio viumbe pekee vyenye hiari ya kuchagua wenyewe wachangie mpango wa Mungu au la.
โNazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi, chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wakoโ (Kumb 30:19-20).
Malaika na watu wanaweza kuchagua hata nini?
Malaika na watu wanaweza kuchagua hata wawe wema au wabaya milele.
โKulikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguniโ (Ufu 12:7-8).
Chaguo letu binadamu linafanyika siku kwa siku kwa kuchukua misimamo mizuri au mipotovu kuhusu dini na maadili.
โMwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzimaโ (Yoh 5:39-40).
Malaika wakoje?
Malaika ni roho tupu walioumbwa na Mungu ili wamtukuze milele, wamlinde kila mtu na kumtumikia Bwana Yesu katika kutuokoa.
โAngalieni, msidharau mmojawapo wadogo hawa, kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguniโ (Math 18:10).
Je, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu peke yetu?
Hapana, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu kwa kuvutwa na mashetani, yaani malaika waliokataa moja kwa moja kumtumikia; baada ya dhambi ya asili hao wanatutumia sisi pia tuangushane na wenzetu.
Lakini Mungu aliwahi kumuambia Shetani:
โNitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako, na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisiginoโ (Mwa 3:15).
โHata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamkeโ (Gal 4:4).
Joseph Kawawa (Guest) on December 9, 2023
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Anthony Kariuki (Guest) on October 10, 2023
Rehema hushinda hukumu
Paul Ndomba (Guest) on April 21, 2023
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Anna Malela (Guest) on March 19, 2023
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Elizabeth Mtei (Guest) on April 19, 2022
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Alex Nakitare (Guest) on March 23, 2022
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
David Ochieng (Guest) on January 17, 2022
Dumu katika Bwana.
Edwin Ndambuki (Guest) on December 8, 2021
Nakuombea ๐
Rose Kiwanga (Guest) on December 6, 2021
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Dorothy Majaliwa (Guest) on October 9, 2021
Katika imani, yote yanawezekana
Grace Mushi (Guest) on February 22, 2021
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Joseph Mallya (Guest) on November 23, 2020
Endelea kuwa na imani!
Alice Mwikali (Guest) on October 25, 2020
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Christopher Oloo (Guest) on September 3, 2020
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Kenneth Murithi (Guest) on July 20, 2020
Neema na amani iwe nawe.
Grace Mushi (Guest) on June 7, 2020
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Victor Malima (Guest) on April 23, 2020
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Edward Chepkoech (Guest) on November 18, 2019
Mungu akubariki!
Nicholas Wanjohi (Guest) on September 11, 2019
Rehema zake hudumu milele
Anna Sumari (Guest) on September 6, 2019
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Faith Kariuki (Guest) on August 16, 2019
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Alex Nakitare (Guest) on June 2, 2019
Neema ya Mungu inatosha kwako
Bernard Oduor (Guest) on April 17, 2019
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Henry Sokoine (Guest) on April 10, 2019
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Brian Karanja (Guest) on April 6, 2019
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Grace Mligo (Guest) on April 3, 2019
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Lydia Mutheu (Guest) on March 27, 2019
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Agnes Njeri (Guest) on March 25, 2019
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Raphael Okoth (Guest) on February 5, 2019
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Ruth Kibona (Guest) on October 26, 2018
Nguvu hutoka kwa Bwana
Lucy Wangui (Guest) on June 6, 2018
Tumaini ni nanga ya roho
Elizabeth Malima (Guest) on March 19, 2018
Mungu ni mwema, wakati wote!
Frank Sokoine (Guest) on February 19, 2018
Imani inaweza kusogeza milima
Elizabeth Mtei (Guest) on February 14, 2018
Mwamini Bwana; anajua njia
Catherine Mkumbo (Guest) on December 22, 2017
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Anna Kibwana (Guest) on August 31, 2017
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Daniel Obura (Guest) on July 21, 2017
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Joyce Aoko (Guest) on May 10, 2017
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Edwin Ndambuki (Guest) on February 21, 2017
Mwamini katika mpango wake.
Alex Nakitare (Guest) on February 12, 2017
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Robert Ndunguru (Guest) on January 14, 2017
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Lucy Mushi (Guest) on December 8, 2016
Baraka kwako na familia yako.
Grace Wairimu (Guest) on December 3, 2016
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Mercy Atieno (Guest) on October 11, 2016
Sifa kwa Bwana!
James Kawawa (Guest) on June 1, 2016
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Diana Mumbua (Guest) on April 11, 2016
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Victor Kamau (Guest) on March 22, 2016
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Monica Nyalandu (Guest) on January 20, 2016
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Mercy Atieno (Guest) on September 23, 2015
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Catherine Naliaka (Guest) on August 27, 2015
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia