Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:34:40 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Ndizi mbichi - 10
Nyama - kilo 1
Nazi ya kopo - 1
Chumvi - 1 Kijiko cha chakula
Ndimu - 1
Bizari ya manjano - 1 Kijiko cha chai
Pili pili mbichi - 3
Nyanya (tomatoes) - 2
Kitunguu maji - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chakula
Namna ya Kutayarisha Na Kupika
Kata nyama vipande vipande na uisafishe. Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive. Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi. Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi. Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria. Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo. Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi. Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda. Weka pembeni zipoe. Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.
Jinsi ya kupika Pilau Ya Nyama Ya Ng'ombe Na Nyanya
Updated at: 2024-05-25 10:35:28 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viambaupishi
Mchele (Basmati) 3 vikombe
Nyama ya ngoβmbe 1Β kg
Pilipili boga 1 kubwa
Nyanya 2 kubwa
Vitunguu maji 2 vikubwa
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Tangawizi 1 kijiko cha chai
Ndimu 1
Mafuta ya kupikia Β½ kikombe
Mdalasini Β½ kijiko cha chai
Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai
Pilipili manga Β½ Kijiko cha chai
Hiliki Β½ Kijiko cha chai
Jinsi ya kuandaa na kupika
Loweka mchele wako katika chombo
Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi
Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi
katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni
Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia
Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto
Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya
Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi
Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke
Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza
Funika na punguza moto na uache uive taratibu
Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo Nyanya ya kopo 1/2 Kitunguu 1 Curry powder 1/2 kijiko cha chai Chumvi Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
Safisha samaki na kisha uwamarinate na kitunguu swaum, tangawizi, limao na chumvi kwa muda wa nusu saa. Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana kisha waweke pembeni. Chukua fry-pan kisha tia mafuta kidogo sana (kama 1/2 kijiko cha chai) kisha tia vitunguu maji na uvikaange kwa muda wa dakika 2 (kwani havitakiwi kuiva kabisa) kisha waweke samaki na uwachanganye na hivyo vitunguu. Kisha baada ya hapo tia giligilani iliyokatwa, kamulia limao na tia chumvi kidogo kisha geuzageuza ili kuchanganya vitu vyote na kisha ipua. Baada ya hapo menya na ukate viazi katika vipande vya wastani, na kisha uvichemshe kidogo na visiive kabisa. Baada ya hapo weka sufuria jikoni kwenye moto wa wastani na utie mafuta kidogo (kama vijiko 2 vya chakula) na kisha tia viazi na uanze kuvipika kwa kuvigeuzageuza mpaka viive na kuwa rangi ya brown kisha tia chumvi kidogo, curry powder na giligilani iliyokatwa.Vipike kwa muda wa dakika mbili kisha viipue. Na baada ya hapo malizia kwa kupika asparagus. Kwanza zioshe kisha zikate kati. Baada ya hapo weka mafuta kidogo kama 1/2 kijiko katika fry-pan yakisha pata moto tia kitunguu swaum, asparagus na chumvi.Zipike kwa kuzigeuzageuza kwa muda wa dakika 5 na hapo zitakuwa zimeshaiva na tayari kwa kuliwa pamoja na samaki na viazi. Unaweza kuvisevu kwa ketchup.
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - 10-12
Nyama ngβombe - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 2
Nyanya/tungule - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7
Tangawizi mbichi - 1 kipande
Ndimu - 2 kamua
Chumvi - kiasi
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi - 3 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi. Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive. Menya ndizi ukatekate Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga. Tia tangawizi na thomu ilobakia. Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake. Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 6 Vikombe
Sukari ya kusaga 2 vikombe
Siagi 500 gm
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Kastadi Β½kikombe
MAPISHI
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli. Tia unga na baking powder na Kastadi. Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray). Pika (bake) katika oven moto wa 350Β° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:34:44 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Blue band vijiko vikubwa 2 Maziwa vikombe 2 Royco kijiko kikubwa 1-2 Pilipili manga (unga) kijiko cha 1 Chumvi kiasi Maji lita 2-3 Boga kipande Β½ Viazi mviringo 2 Vitunguu 2 Karoti 2 Nyanya 2
Hatua
β’ Menya boga, viazi, karoti, nyanya na kwaruza weka kwenya sufuria kubwa. β’ Menya, osha na katakata vitunguu kisha ongeza kwenye mboga. β’ Ongeza maji na chumvi chemshwa mpaka vilainike. β’ Pekecha ikiwa jikoni na moto kidogo β’ Ongeza blue band, maziwa royco na pilipili manga ukikoroga kwa dakika 5. β’ Onja chumvi na pakua kama supu. Uwezekano Tumia siagi badala ya margarine.
Jinsi ya kutengeneza Slesi Za Chokoleti Na Karameli
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 1 Magi (vikombe vya chai)
Sukari ya browni - Β½ Magi
Siagi iliyoyayushwa - 125Β g
Nazi iliyokunwa - Β½ Magi
MJAZO WA KARMEL (Caramel filling)
Syrup - 1/3 kikombe cha chai
Siagi iliyoyayushwa - 125Β g
Maziwa matamu ya mgando - 2 vikopo (condensed milk)
MJAZO WA CHOKOLETI (Chocolate filling)
Chokoleti - 185Β g (dark chocolate)
Mafuta - 3 Vijiko vya chai
MAANDALIZI
Changanya unga, sukari, siagi na nazi iliyokunwa kwenye bakuli mpaka unga ushikamane. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30Β cm au (8 in kwa 12 in) unaweza kuweka karatasi ya kuchomea chini ukipenda. Choma kwenye moto 325ΛC kwa muda wa dakika 15 mpaka 18 au mpaka ibadilike kuwa rangi ya browni. Kwenye sufuria ndogo tia syrup siagi na maziwa matamu ya mgando na changanya kwa moto mdogo mpaka uwe mzito kasha mimina juu ya keki uliyochoma na choma tena kwa muda wa dakika 20 mpaka karameli iwe rangi ya dhahabu. Kwenye sufuria ndogo nyingine tia vipande vya chokoleti na mafuta na ukoroge kwa moto mdogo mpaka iyayuke kisha wacha ipoe kidogo mimina juu ya mjazo wa karameli kisha weka kwenye friji mpaka ishikamane. Kata vipande weka kwenye sahani tiyari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:34:55 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIPIMO:
Unga wa Visheti
Unga 4 Vikombe vya chai
Siagi 1 Kikombe cha chai
Hiliki Β½ Kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.
2. Changanya vizuri isiwe na madonge.
3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
4. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.
5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .
6. Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili
7. Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.
8. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.
Shira:
Sukari 2 Vikombe vya chai
Maji 1 Kikombe cha chai
Vanilla Β½ Kijiko cha chai
(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.
Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Makongoro (miguu ya ng'ombe) kiasi Limao 1 kubwa Kitunguu swaum Tangawizi Chumvi Pilipili
Matayarisho
Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.
Note: Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.