Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna nyama za aina mbili, nazo ni nyama nyeupe na nyama nyekundu.
Nyama nyeupe
Hizi ni nyama zitokanazo na samaki, kuku, ndege wa aina zote, bata, wadudu
Nyama nyekundu
Hutokana na ngβombe, mbuzi, kondoo,nguruwe na wanyama wa porini.
Nyama ina virutubishi vingi muhimu kwa afya ya binadamu kama protini, vitamini na madini. Madini ya chuma yanayopatikana kwenye nyama ni rahisi sana kusharabiwa (kufyonzwa) mwilini na ni muhimu kwa kuongeza wekundu wa damu. Uwezo wa miili ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuyeyusha chakula na kusharabu (kufyonza) virutubishi hupungua. Utumiaji wa nyama nyekundu kwa wingi unaweza kuwaletea matatizo hasa katika uyeyushwaji tumboni kwani nyama nyekundu si rahisi kuyeyushwa ukilinganisha na nyama nyeupe.
Hata hivyo katika nchi yetu watu walio wengi wanatumia nyama kwa kiasi kidogo sana na mara chache. Si vyema watu hawa waache kabisa nyama nyekundu. Jambo la muhimu ni kutumia njia mbalimbali ili kuifanya nyama hii iyeyushwe kwa urahisi tumboni.
Namna ya kusaidia uyeyushwaji ni pamoja n a : -
β’ Kutafuna vizuri au kutumia nyama ya kusaga (kwa wanaoipata). β’ Kupika nyama na viungo vinavyosaidia kulainisha kama vile papai bichi, limao, vitunguu saumu n.k. β’ Kula nyama pamoja na papai
Kwa hiyo, kwa anayepata nyama nyekundu kwa wingi, kupunguza kiasi cha nyama hiyo na kuongeza kiasi cha nyama nyeupe. Na kwa yule asiyepata nyama nyeupe, apatapo nyama nyekundu asiache kutumia kwani ina umuhimu mwilini mwake.
Vidokezo 10 vya Vitafunio vya Afya kwa Watoto Wagumu Kula
π Je, unatambua jinsi vitafunio vya afya vinavyoweza kuwabadilisha watoto wagumu kula? β¨π π Bofya hapa na ujifunze vidokezo 10 vya kushangaza ambavyo vitawafanya wapenzi wako wa chakula wakula kwa furaha! ππ₯¦ π Pata habari kamili kwenye makala yetu iliyobeba siri za kuwa na watoto wanaopenda kula! ππͺ #Afya #VitafunioVyaAfya #WatotoWagumuKula
Updated at: 2024-05-25 10:22:24 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vidokezo 10 vya Vitafunio vya Afya kwa Watoto Wagumu Kula
Kama mzazi au mlezi, mara nyingine inaweza kuwa changamoto kubwa kuwapa watoto wako vitafunio vyenye afya, hasa pale ambapo wana tabia ya kuchagua vyakula visivyo na lishe. Lakini usijali! Kama AckySHINE, nina vidokezo 10 vya vitafunio vya afya ambavyo vitawafurahisha watoto wako na kuwapa lishe bora wanayohitaji. Soma ili kugundua!
Matunda yenye rangi:
Matunda kama vile tufaa, ndizi, au zabibu ni vitafunio bora kwa watoto. Wanaweza kula matunda haya kama yalivyo au kutengeneza saladi ya matunda yenye rangi mbalimbali kwa kuongeza limau kidogo ili kuongeza ladha. πππ
Karanga:
Karanga kama vile njugu, karanga za pekee au karanga za kawaida zina protini nyingi na mafuta yenye afya. Unaweza kuzitoa kama vitafunio vya kati au kuzichanganya na matunda yaliyokatwa ndogo kwa kitafunio bora zaidi. π₯
Jibini:
Jibini ni chanzo kizuri cha protini na madini ya kalsiamu. Unaweza kuwapa watoto wako vipande vidogo vya jibini pamoja na matunda au karanga kama vitafunio vyenye afya. π§
Yoghurt:
Yoghurt yenye asili ya maziwa ni chanzo bora cha protini na kalsiamu. Unaweza kuongeza asali au matunda yaliyokatwa ndani yake ili kuongeza ladha na kufanya iwe vitafunio bora zaidi. π₯
Mtindi:
Mtindi ni chanzo kingine bora cha protini na kalsiamu. Unaweza kuongeza matunda yaliyokatwa kidogo au karanga zilizokatwa ndani ya mtindi ili kuongeza ladha na virutubisho vyenye afya. π
Sandvihi za mboga:
Badala ya kutumia mkate wa kawaida, tumia mkate wa ngano nzima au mkate wa mboga kama karoti au matango. Weka mboga zingine kama nyanya au pilipili kwenye sandvihi na uwape watoto wako. Ni vitafunio vyenye lishe bora na rahisi kuandaa. π₯ͺ
Ndizi za kukaanga:
Ndizi za kukaanga ni vitafunio vya afya na tamu ambavyo watoto wengi hupenda. Unaweza kuzikaanga kwa mafuta ya mizeituni au jibini kidogo ili kuongeza ladha. π
Kabeji:
Kabeji ni mboga yenye lishe na inayoambatana vizuri na vitafunio vingine. Unaweza kutoa vipande vidogo vya kabeji pamoja na dipu ya jibini au mtindi. π₯¬
Barafu ya matunda:
Kufanya barafu ya matunda ni njia nzuri ya kuwapa watoto wako kitafunio cha baridi na kitamu. Changanya matunda yaliyosagwa na maji, weka kwenye tray ya barafu na weka kwenye friji hadi itenge. Ni kitafunio bora cha majira ya joto! π§
Chapati za nafaka:
Badala ya kutumia unga wa ngano, tumia unga wa nafaka kama vile unga wa mtama au ulezi. Chapati za nafaka ni vitafunio bora vyenye lishe na rahisi kuandaa. Unaweza kuzitumia kama sahani ya kando au kuzikata vipande vidogo na kuwapa watoto wako. πΎ
Hivyo basi, kama AckySHINE ninaamini kwamba vitafunio vyenye afya ni muhimu sana kwa watoto wetu. Kwa kufuata vidokezo hivi, unaweza kuwapa watoto wako vitafunio vyenye lishe bora na kuwajenga kwenye tabia ya kula afya. Kumbuka, kuwapa watoto wako vitafunio vyenye afya ni njia bora ya kuwaweka na afya bora na kuwapa nguvu ya kukua na kufanikiwa!
Je, una maoni gani kuhusu vidokezo hivi? Je, umewahi kujaribu vitafunio hivi na kama ndivyo, ni vitafunio vipi ulivyopenda zaidi? Asante kwa kusoma na natarajia kusikia maoni yako! π
1) Weka karai kwenye moto kiasi
2) Tia siagi
3) Tia tambi uzikaange usiachie mkoni mpaka ziwe rangu ya dhahabu.
4) Weka lozi na zabibu huku unakoroga
5) Tia maziwa na huku unakoroga usiachie mkono.
6) Tia arki
7) Epua karai, tumia kijiko cha chai kwa kuchotea na utie kwenye kikombe cha kahawa nusu usikijaze.
8) Kipindue kwenye sahani utoe kileja.
9) Fanya hivyo mpaka umalize vyote.
Jinsi ya kutengeneza Wali Wa Dengu Kwa Samaki Wa Kukaanga
Updated at: 2024-05-25 10:37:33 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa basmati - 3 Vikombe
Dengu - 2 vikombe
Viazi - 3 vikubwa
Kitunguu - 2 kubwa
Nyanya - 2
Pilipili mbichi kubwa - 3
Pilipilimanga - Β½ kijiko cha chai
Garama Masala (bizari mchanganyiko) -1 kijiko cha chai
Supu ya vidonge (stock cubes) - 2 vidonge
Chumvi - kiasi
Mafuta - ΒΌ kikombe
Zaafarani - 1 kijiko cha chai
Samaki wa kukaanga
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Dengu kama sio za tayari kwenye kopo, roweka na zichemshe hadi ziwive
Maandalizi ya Masala Ya Dengu:
Zaafarani β iroweke katika maji ya dafu dafu (warm) ya chini ya robo kikombe weka kando. Osha mchele, roweka. Menya viazi na vitunguu, katakata vitunguu, na nyanya , weka kando. Katakata viazi vipande vidogo vidogo kwa umbo la mchemraba (cubes). Katika sufuria tia mafuta yakipata moto, tia viazi ukaange kidogo kwa moto mdogo mdogo hadi kukaribia kuwiva, toa weka kando. Kaanga vitunguu hadi vigeuka rangi ya hudhurungi isiyokoza (light brown) kisha tia nyanya ukaange kidogo. Tia vidonge vya supu (stock cubes) uvivuruge katika mchanganyiko, katakata pilipili mbichi kwa urefu tia, uendelee kukakaanga. Tia bizari, chumvi. Zima moto, changanya dengu na viazi katika mchanganyiko huo.
Mapishi ya Wali:
Chemsha mchele kama kawaida ya kupika wali mweupe, kiini kiwe kimewiva nusu yake. Chuja maji kisha changanya katika mchanganyiko wa dengu. Nyunyizia zaafarani, uchanganye wali na mchanganyiko kidogo tu. Funika acha uive katika mtoto mdogo mdogo au tia katika oveni hadi uive kama kawaida ya kupika wali. Pakua katiha sahani na tolea na samaki yoyote wa kukaanga.
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mackerel 2 Kitunguu swaum na tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha cha kula Pilipili iliyo katwakatwa (chopped scotch bonnet ) 1/2 Limao (lemon) 1/2 Chumvi (salt) kiasi Curry powder 1/2 kijiko cha chai Coriander powder 1/2 kijiko cha chai Mafuta 1 kijiko cha chai
Matayarisho
Safisha samaki kisha wakaushe maji ( ukipenda unaweza kuwakata kati au ukawapika wazima) Baada ya hapo wakate mistari kila upande ( ili spaces ziweze kuingia ndani) kisha waweke kwenye bakuli na utie spice zote. Wachanganye vizuri kisha waweke frijini na uwaache wamarinate kwa muda wa masaa 3. Baada ya hapo washa oven kisha wapakaze mafuta na uwafunge kwenye foil na uwatie kwenye oven kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo fungua foil na uwaache kwenye oven kwa muda wa dakika 10 ili wapate kukauka kidogo. Na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuwala kwa kitu chochote upendacho.
Updated at: 2024-05-25 10:34:48 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo tunaangalia mapishi ya fish finger ( sijui kama unaweza kusema kidole cha samaki)!, Ni mlo mzuri hasa kuliwa kama kitafunio au mboga ya pembeni.
Mahitaji
500g Fileti ya samaki 120g Chenga za mkate 100g Unga wa ngano Mayai 2 Ndimu 1 Kitunguu saumu 1 Kotmiri Mafuta ya kupikia
Matayarisho
Menya vitunguu saumu kisha visage
Katakata fileti kwa muundo wa mraba (kama vidole) kisha paka mchanganyiko wa vitunguu saumu
Kata ndimu na kamulia kwenye fillet yako
Weka chenga za mkate kwenye bakuli kisha uchanganye chumvi kiasi na kata kata kotmiri majani 3 na uchanganye pamoja.
Kwenye bakuli lingine weka mayai na uyapigepige yawe kama uji mzito
Weka unga kwenye bakuli jingine.
Chukua kipande cha fillet kiweke unga kidogo kisha kizamishe kwenye yai na baada ya hapo kizamishe kwenye mchanganyiko wa chenga za mkate. Fanya hivyo kwa vipande vyote.
Weka mafuta kwenye kikaago na subiri yachemke kisha weka fillet zako vizuri na zikaange pande zote hadi zimekuwa rangi ya brown ( hakikisha moto sio mkali sana).
Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Bilinganya 2 za wastani Nyanya kubwa 1 Kitunguu maji 1 kikubwa Swaum 1/2 kijiko cha chai Limao 1/4 Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai Parpika 1/4 kijiko cha chai Pilipili mtama 1/4 kijiko cha chai Curry powder1/4 kijiko cha chai Chumvi kiasi Coriander Olive oil
Matayarisho
Katakata bilinganya slice nyembamba kisha ziweke pembeni. Baada ya hapo kaanga kitunguu maji mpaka kiwe cha brown kisha tia swaum na spice zote, zikaange kidogo kisha tia nyanya na chumvi kiasi. Pika nyanya mpaka iive na itengane na mafuta. Baada ya hapo tia mabilinganya na ukamulie limao kisha punguza moto na uyafunike na mfuniko usioruhusu kutoa mvuke ili yaivie na huo mvuke. Baada ya hapo yaonje kama yameiva na malizia kwa kutia fresh coriander na baada ya hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa. kwa kawaida mi hupendaga kuyalia na wali na maharage badala ya kachumari kwahiyo nakuwa naitumia hiyo kama kachumbari
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Maziwa ya unga - 2 vikombe
Sukari - 3 vikombe
Maji - 3 vikombe
Unga wa ngano - Β½ kikombe
Mafuta - Β½ kikombe
Iliki - kiasi
MAPISHI
Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri Kisha mimina mafuta koroga Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza. Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 1 kilo
Kuku - 1
Vitunguu - 3
Viazi/mbatata - 5
Jira/bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 1 kijiti
Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
Hiliki - 3 chembe
Karafuu - 5 chembe
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kupikia - Β½ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote.. Menya viazi, katakata vipande vya kiasi. Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau. Tia bizari zote isipokuwa hiliki. Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo. Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi. Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.