Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Dagaa wabichi (Fresh anchovies packet 1) Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo) Matembele ya kukaushwa (dried sweet potato leaves, handful) Nyanya ya kopo (tin tomato 1) Kitunguu maji (onion 2) Limao (lemon 1/4) Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop) Chumvi (salt 1/2 ya kijiko cha chai) Mafuta (vegetable oil) Hoho (green pepper 1) Kitunguu swaum (garlic 5 cloves) Tangawizi (ginger 1 kijiko cha chai) Binzari ya curry (Curry powder 1/2 kijiko cha chai)
Matayarisho
Safisha dagaa kwa kutoa vichwa na utumbo kisha waoshe na uwakaushe na kitchen towel na uwaweke pembeni. Baada ya hapo katakata, vitunguu na hoho kisha weka pembeni. Baada ya hapo weka sufuria jikoni na utie mafuta yakisha pata moto tia dagaa na uwakaange mpaka wawe wa brown, kisha tia kitunguu swaum,curry powder na tangawizi, kaanga kidogo kisha malizia kwa kutia vitunguu maji, hoho,pilipili,chumvi na ukamulie limao. Kaanga kwa muda wa dakika 3-4 na hakikisha vitunguu na hoho haviivi sana na hapo dagaa watakuwa tayari.
Baada ya hapo yaoshe na uyaloweka matembele (kama ni makavu) kwa muda wa dakika 15, Kisha yatoe na uyaweke kwenye sufuria pamoja na kitunguu, nyanya, chumvi ,kamulia limao kidogo, pilipili na maji kiasi. acha matembele yachemke kwa muda wa dakika 20 na uhakikishe yameiva kwa kuwa laini. Baada ya hapo yapike mpaka maji yote yakauke na mafuta yatok na hapo matembele yatakuwa tayari.
Ukisha maliza kupika dagaa na matembele andaa chungu cha ugali. Kwanza unatakiwa kuchemsha maji ya moto, kisha koroga pembeni unga kiasi katika maji ya baridi na utie kwenye maji yanayochemka, Fanya kama unatengeneza uji, uji wa ugali ukishachemka tia unga na uanze kuusonga mpaka ugali uive. Ukisha iva pakua na usevu na mboga tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo tunaangalia mapishi ya fish finger ( sijui kama unaweza kusema kidole cha samaki)!, Ni mlo mzuri hasa kuliwa kama kitafunio au mboga ya pembeni.
Mahitaji
500g Fileti ya samaki 120g Chenga za mkate 100g Unga wa ngano Mayai 2 Ndimu 1 Kitunguu saumu 1 Kotmiri Mafuta ya kupikia
Matayarisho
Menya vitunguu saumu kisha visage
Katakata fileti kwa muundo wa mraba (kama vidole) kisha paka mchanganyiko wa vitunguu saumu
Kata ndimu na kamulia kwenye fillet yako
Weka chenga za mkate kwenye bakuli kisha uchanganye chumvi kiasi na kata kata kotmiri majani 3 na uchanganye pamoja.
Kwenye bakuli lingine weka mayai na uyapigepige yawe kama uji mzito
Weka unga kwenye bakuli jingine.
Chukua kipande cha fillet kiweke unga kidogo kisha kizamishe kwenye yai na baada ya hapo kizamishe kwenye mchanganyiko wa chenga za mkate. Fanya hivyo kwa vipande vyote.
Weka mafuta kwenye kikaago na subiri yachemke kisha weka fillet zako vizuri na zikaange pande zote hadi zimekuwa rangi ya brown ( hakikisha moto sio mkali sana).
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Tende zilizotolewa kokwa - 1 Kilo
Cornflakes - 1 ½ kikombe
Lozi Zilokatwa katwa - 1 kikombe
Siagi - ¼ kilo
MANDALIZI
Mimina tende na siagi kwenye sufuria bandika motoni moto mdogo mdogo mpaka zilainike. Kwa muda wa dakika 10. Isonge kidogo kwa mwiko au kuikoroga ichanganyike vizuri. Changanya Cornflakes na lozi kwenye tende mpaka zichanganyika vizuri. Pakaza treya au sinia mafuta au siagi kidogo. Mimina mchanganyiko wa tende, zitandaze vizuri na ukate vipande saizi unayopenda. Zikiwa tayari kuliwa kwa kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:22:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour) ( 1/4 kilo) Yai (egg 1) Sukari (sugar 1/4 kikombe cha chai) Chumvi (salt 1/4 kijiko cha chai) Hiliki (ground cardamon 1/4 kijiko cha chai) Maji kiasi Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Tia unga kwenye bakuli, kisha weka sukari, chumvi, hiliki na maji kiasi. Kisha koroga mpaka mchanganyiko wako uwe mzito. Baada ya hapo tia yai na ukoroge tena. hakikisha mchanganyiko hauwi mzito sana au mwepesi sana.Baada ya hapo onja kama kila kitu kimekolea. Injika chuma cha kupikia chapati (fry-pan) jikoni katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia nusu kijiko cha chakula cha mafuta katika fry-pan na kisha yatandaze. Hakikisha chuma kinapata moto na weka upawa mmoja wa unga wa chapati na uutandaze mpaka uwe flat. Baada ya hapo subiri mpaka chapati ikauke juu na kisha igeuze upande wa pili tia mafuta kijiko 1 kikubwa cha chakula kwa upande wa chini na wa juu kisha uanze kuikandamiza kwa juu na kijiko ili iweze kuiva vizuri kwa chini. Ikisha kuwa ya rangi ya brown igeuze na upike upande wa pili kiasi kisha iipue na uiweke kwenye sahani yenye kitchen towel ili kukausha mafuta. Rudia hii process kwa unga wote uliobakia. Na chapati zitakuwa tayari
Jinsi ya kutengeneza Wali Wa Dengu Kwa Samaki Wa Kukaanga
Updated at: 2024-05-25 10:37:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa basmati - 3 Vikombe
Dengu - 2 vikombe
Viazi - 3 vikubwa
Kitunguu - 2 kubwa
Nyanya - 2
Pilipili mbichi kubwa - 3
Pilipilimanga - ½ kijiko cha chai
Garama Masala (bizari mchanganyiko) -1 kijiko cha chai
Supu ya vidonge (stock cubes) - 2 vidonge
Chumvi - kiasi
Mafuta - ¼ kikombe
Zaafarani - 1 kijiko cha chai
Samaki wa kukaanga
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Dengu kama sio za tayari kwenye kopo, roweka na zichemshe hadi ziwive
Maandalizi ya Masala Ya Dengu:
Zaafarani – iroweke katika maji ya dafu dafu (warm) ya chini ya robo kikombe weka kando. Osha mchele, roweka. Menya viazi na vitunguu, katakata vitunguu, na nyanya , weka kando. Katakata viazi vipande vidogo vidogo kwa umbo la mchemraba (cubes). Katika sufuria tia mafuta yakipata moto, tia viazi ukaange kidogo kwa moto mdogo mdogo hadi kukaribia kuwiva, toa weka kando. Kaanga vitunguu hadi vigeuka rangi ya hudhurungi isiyokoza (light brown) kisha tia nyanya ukaange kidogo. Tia vidonge vya supu (stock cubes) uvivuruge katika mchanganyiko, katakata pilipili mbichi kwa urefu tia, uendelee kukakaanga. Tia bizari, chumvi. Zima moto, changanya dengu na viazi katika mchanganyiko huo.
Mapishi ya Wali:
Chemsha mchele kama kawaida ya kupika wali mweupe, kiini kiwe kimewiva nusu yake. Chuja maji kisha changanya katika mchanganyiko wa dengu. Nyunyizia zaafarani, uchanganye wali na mchanganyiko kidogo tu. Funika acha uive katika mtoto mdogo mdogo au tia katika oveni hadi uive kama kawaida ya kupika wali. Pakua katiha sahani na tolea na samaki yoyote wa kukaanga.
Jinsi ya kutengeneza Cookies Za Tende Na Tangawizi
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga vikombe vikombe 4
Baking soda 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi 400 gms
Sukari ½ kikombe
Tende chambua ukatekate ifikie ¾ kikombe
Tangawizi ya unga vijiko 2 vya chai
Vanilla 1 kijiko cha chai
Yai 1
Maziwa mazito vijiko 2 vya kulia.
MAANDALIZI
Changanya siagi na sukari katika mashine usage mpaka iwe laini nyororo. Tia yai uchanganye vizuri Tia tende na vanilla, tangawizi uchanganye vizuri. changanya unga na baking soda kisha, mimina kidogo kidogo huku unachanganya kwa kijiko cha ubao (mwiko). Unga ukiwa mzito ongeza vijiko 2 vya maziwa. Fanya viduara upange katika treya uliyopakaza siagi kisha uchome (bake) katika over moto mdogo wa kiasi dakika 15 vigeuke rangi viwive. Epua vikiwa tayari
Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Bilinganya 2 za wastani Nyanya kubwa 1 Kitunguu maji 1 kikubwa Swaum 1/2 kijiko cha chai Limao 1/4 Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai Parpika 1/4 kijiko cha chai Pilipili mtama 1/4 kijiko cha chai Curry powder1/4 kijiko cha chai Chumvi kiasi Coriander Olive oil
Matayarisho
Katakata bilinganya slice nyembamba kisha ziweke pembeni. Baada ya hapo kaanga kitunguu maji mpaka kiwe cha brown kisha tia swaum na spice zote, zikaange kidogo kisha tia nyanya na chumvi kiasi. Pika nyanya mpaka iive na itengane na mafuta. Baada ya hapo tia mabilinganya na ukamulie limao kisha punguza moto na uyafunike na mfuniko usioruhusu kutoa mvuke ili yaivie na huo mvuke. Baada ya hapo yaonje kama yameiva na malizia kwa kutia fresh coriander na baada ya hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa. kwa kawaida mi hupendaga kuyalia na wali na maharage badala ya kachumari kwahiyo nakuwa naitumia hiyo kama kachumbari
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Slice za mkate 6 Mayai 3 Chumvi Olive oil
Matayarisho
Vunja mayai yote katika sahani kisha tia chumvi kidogo sana na uyapige mpaka chumvi ichanganyike. Kisha chukua frying pan na utie vimafuta kidogo na uweke jikoni. Mafuta yakishapata moto kiasi,chovya slice za mkate katika hayo mayai na uzipike pande zote zikishaiva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili kukausha mafuta.Na baada ya hapo mikate yako itakuwa tayari kwa kuliwa na chai.