Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Tambi (vermiceli Roasted) Mifuko 2
Siagi - 4 Vijiko vya supu
Maziwa (condensed) 300Ml
Lozi zilizokatwakatwa - 1 kikombe
Zabibu kavu - 1 Kikombe
Arki (essence) - 1 Kijiko cha supu
MAPISHI
Weka karai kwenye moto kiasi Tia siagi Tia tambi uzikaange usiachie mkoni mpaka ziwe rangu ya dhahabu. Weka lozi na zabibu huku unakoroga Tia maziwa na huku unakoroga usiachie mkono. Tia arki Epua karai, tumia kijiko cha chai kwa kuchotea na utie kwenye kikombe cha kahawa nusu usikijaze. Kipindue kwenye sahani utoe kileja. Fanya hivyo mpaka umalize vyote.
Updated at: 2024-05-25 10:37:38 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Majimbi (Eddoes) kiasi 6 au 7
Nyama ng’ombe ½ kilos
Tangawizi ilosagwa 1 kijiko cha kulia
Haldi (bizari manjano/turmeric) ½ kijiko cha chai
Tui zito la nazi vikombe 2
Chumvi kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Safisha nyama kisha weka chumvi, bizari ya manjano, tangawizi mbichi, ukaushe kwanza katika sufuria kwa kukaanga kaanga. Ikianza kukauka, weka maji funika uchemshe iwive. Menya majimbi ukate kate na uweke katika sufuria nyengine. Mimina supu na nyama katika majimbi uchemshe yawive majimbi. Mwisho weka tui zito la nazi uchanganye vizuri kisha weka katika moto kidogo tu bila kufunika yakiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:23:00 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour) vikombe 2 na1/2 Sukari (sugar) 1/2 kikombe Hamira (yeast) 1/2 kijiko cha chai Hiliki (cardamon powder) 1/4 kijiko cha chai Tui la nazi (coconut milk) kiasi Baking powder 1/4 kijiko cha chai Siagi (butter)1 kijiko cha chakula Mafuta ya kukaagia
Matayarisho
Changanya unga na vitu vyote kasoro tui la nazi na mafuta ya kukaangia. Ukisha changanyika vizuri tia tui la nazi na uanze kuukanda mpaka uwe mlaini. Baada ya hapo usukume na ukate mandazi katika shape uipendayo, Kisha uyawe katika sehemu yenye joto (warm place) ili yapate kuumuka. Yakisha uumuka yakaange katika mafuta mpaka yaive kisha ipua na uyaache yapoe tayari kwa kuliwa. (Mafuta ya kukaangia yasiwe yamoto sana kwani yatayababua mandazi na hivyo ndani hayataiva vizuri.
Updated at: 2024-05-25 10:34:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo wapendwa nitaenda kuzungumzia mapishi ya mchuzi wa kuku (chicken curry).
Mahitaji
Kuku mzima Nyanya kubwa 3 Karoti mbili Pilipili hoho Kotmiri Tangawizi Kitunguu maji Kitunguu saumu kidogo Ndimu Mafuta ya kupikia Chumvi (pilipili ukipenda)
Matayarisho
1. Menya vitunguu saumu na tangawizi na uvitwange pamoja. 2. Katakata kuku vipande vidogo kisha ukamulie ndimu na kupaka mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu (kiasi tu). 3. Katakata vitunguu maji na pilipili hoho uweke pembeni. 4. Grind (Kwangua) kwenye grater nyanya na karoti pia uweke pembeni. 5.Katakata kotmiri vipande vidogo uweke pembeni. 6. Andaa kikaango na jiko.
Mapishi
1. Bandika kikaango jikoni na mafuta kiasi, yakishachemka weka vitunguu maji na kaanga hadi vimelainika na kuiva (hakikisha haviungui). 2. Weka pilipili hoho na karoti na endelea kukoroga hadi vyote viive na kulainika, Kisha weka chumvi. 3. Sasa weka vipande vya nyama koroga na funikia kwa dakika 3, kisha weka nyanya zako ulizo grind na koroga ili zichanganyike vizuri, vikishachanganyika weka kotmiri na pilipili kama utapenda. Acha vichemke kwa dakika 5. Hakikisha moto sio mkali sana. 4. Angalia kama nyama zimeiva vizuri kisha epua mchuzi wako. 5. Pakua kwenye bakuli na katakata kotmiri uweke kwa juu. Unaweza kula kwa ugali, wali, ndizi rost au chipsi.
Updated at: 2024-05-25 10:37:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Mashonanguo mkono 1 Tui la nazi kikombe 1 Karanga zilizosagwa kikombe ½ Mafuta vijiko vikubwa 4 Kitunguu 1 Nyanya ndogo 2 Chumvi kiasi
Hatua
• Chambua mashona nguo mateke, osha na katakata. • Menya osha na katakata kitunguu. • Osha, menya na katakata nyanya. • Kaanga karanga, ondoa maganda na saga zilainike. • Kuna nazi na chuja tui. • Kanga kitunguu, weka nyanya na koroga mpaka zilainike. • Weka mashona nguo na chumvi kisha koroga sawa sawa, funikiakwa dakika 5 -10. • Changanya tui la nazi na karanga, ongeza kwenye hizo mboga ukikoroga kwa dakika 5, punguza moto ili ziive taratibu. • Onja chumvi na pakua kama kitoweo. Uwezekano Changanya mnavu, mgagani, mashonanguo kidogo ki¬dogo au mboga nyingme. Tumia maziwa au krimu badala ya tui la nazi. Weka nyama au dagaa au samaki au mayai badala ya - karanga.
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 4 Vikombe vya chai Sukari ya laini (icing sugar) - 1 Kikombe cha chai Baking powder - 2 Vijiko vya chai Mayai - 2 Siagi au margarine - 1 Kikombe cha chai Vanilla -1 Kijiko cha chai Maziwa ya kuchanganyia - kiasi Tende iliyotolewa koko - 1 Kikombe ufuta (sasame) kiasi 1/4 kikombe
MAANDALIZI
Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika mashine. Kisha tia mayai, vanilla na halafu maziwa kidogo kidogo hadi mchanganyiko ushikamane. Gawanya madonge mawili na usukume kama chapati, lakini sio nyembamba sana. Tandaza tende robo ya duara na unyunyize ufuta duara zima: kisha kunja hadi mwisho na ukate kate, kisha upange katika trei ya kuvumbika. Vumbika (bake) moto wa 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi vigeuke rangi na viwive. Zikisha iiva ziache zipowe na zitakuwa tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
· Osha mikono yako kwa sabuni kabla na baada ya kutayarisha chakula · Tumia vyombo safi na sehemu safi kwa kutayarisha na kula chakula · Viporo vipashwe moto vizuri kabla ya kula · Chemsha maji ya kunywa na kuyaacha jikoni dakika kumi baada ya kuchemka
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 1 kilo
Kuku - 1
Vitunguu - 3
Viazi/mbatata - 5
Jira/bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 1 kijiti
Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
Hiliki - 3 chembe
Karafuu - 5 chembe
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kupikia - ½ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote.. Menya viazi, katakata vipande vya kiasi. Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau. Tia bizari zote isipokuwa hiliki. Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo. Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi. Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.
Updated at: 2024-05-25 10:37:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Boga la kiasi - nusu yake
Tui zito la nazi 1 ½ gilasi
Sukari ½ kikombe
Hiliki ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Menya boga kisha katakata vipande vya kiasi. Weka katika sufuri tia maji kiasi ya kuchemshia na kuwiva bila ya kubakia maji mengi. Changanya tui na sukari na hiliki kisha mimina juu ya boga wacha katika moto dakika chache tu bila ya kufunika. Epua mimina katika chombo likiwa tayari.