Ee Yesu Mfungwa wa Upendo wa Mungu,/ ninapofikiri Upendo wako na jinsi ulivyojitolea kwa ajili yangu,/ nashindwa kuelewa./ Unaficha Ukuu wako usiofahamika/ na kujidhihirisha kwa ajili yangu mimi mnyonge./ Ee Mfalme wa utukufu,/ unaficha uzuri wako,/ lakini jicho la moyo wangu/ linapenya pazia na kuona Majeshi ya Malaika/ wakikuimbia kwa heshima bila kukoma/ na nguvu zote mbinguni zikikusifu bila mwisho zikisema:/ βMtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu..β/
Ni nani awezaye kufahamu Upendo wako/ na huruma yako isiyo na kipimo kwa ajili yetu!/ Ee Mfungwa wa Upendo,/ nafungia moyo wangu masikini/ kwenye Tabarnakulo hii/ ili niweze kukuabudu usiku na mchana bila mwisho./ Najua hakuna kizuizi/ na hata kama naonekana kukaa mbali,/ lakini moyo wangu u pamoja nawe/ katika ibada hii./ Hakuna kinachoweza kuzuia upendo wangu kwako./ Kwangu hakuna kizuizi chochote./
Ee Utatu Mtakatifu,/ Mungu Mmoja usiyegawanyika,/ utukuzwe kwa zawadi yako hii kuu/ na agano hili la huruma!/
Nakuabudu,/ Bwana na Muumba uliyefichika katika Sakramenti Takatifu!/ Ee Bwana,/ nakuabudu kwa kazi zote za mikono yako/ zinazonifunulia Hekima yako kuu,/ Wema wako na Huruma yako kuu./ Uzuri uliousambaza hapa/ Uzuri ulio nao Wewe mwenyewe/ ambaye U Uzuri usioelezeka;/ na ingawaje umejificha na kusitiri uzuri wako,/ jicho langu,/ kwa mwanga wa imani linafika kwako,/ na roho yangu inapata kumtambua Muumba wake/ aliye Uzuri usiopimika,/ ulio juu ya kila uzuri,/ na moyo wangu unazama kabisa katika sala ya kukuabudu./
Bwana wangu na Muumba wangu,/ wema wako wanitia moyo wa kuongea nawe,/ Huruma yako huondoa kiambaza/ kitenganishacho Muumba na kiumbe./ Furaha ya moyo wangu,/ ee Mungu, ni kuongea na Wewe./ Yote ambayo moyo wangu unayatamni nayapata kwako./ Hapa ndipo mwanga wako unaponiangaza akili yangu/ na kuiwezesha kukujua Wewe zaidi na zaidi/ β ndipo mikondo ya neema inapoutiririkia moyo wangu,/ ndipo roho yangu inapochota uzima wa milele./ Ee Bwana na Muumba wangu,/ licha ya mapaji yote haya,/ unajitoa mwenyewe kwangu,/ ili uweze kujiunganisha na kiumbe dhaifu na maskini./
Ee Kristu,/ nafurahi sana nionapo kwamba unapendwa/ na kwamba sifa na utukufu wako vinaongezwa/ hasa ya Huruma yako./ Ee Kristu,/ sitaacha kamwe kuutukuza wema wako na huruma yako,/ hadi dakika ya mwisho ya maisha yangu./ Kwa kila tone la damu yangu/ na kwa kila pigo la moyo wangu/ naitukuza Huruma yako./ Natamani kugeuzwa kabisa/ na kuwa utenzi wa utukufu wako./ Naomba siku ya kufa kwangu/ popote nitakapokuwa nimelala,/ pigo la mwisho la moyo wangu/ liwe utenzi mpendevu/ usifuo Huruma yako isiyo na kipimo./ Amina
(Na Mt. Faustina Kowalska).
Nora Kidata (Guest) on September 3, 2018
πβ€οΈβ¨ Asante Mungu kwa kila kitu
Janet Mwikali (Guest) on August 29, 2018
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Hellen Nduta (Guest) on August 13, 2018
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Peter Mugendi (Guest) on May 3, 2018
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Victor Malima (Guest) on February 27, 2018
ππ Namuomba Mungu akupiganie
Anna Malela (Guest) on December 10, 2017
Neema ya Mungu inatosha kwako
George Mallya (Guest) on November 16, 2017
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Irene Makena (Guest) on July 16, 2017
Mwamini katika mpango wake.
Peter Mugendi (Guest) on June 7, 2017
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Sarah Karani (Guest) on March 20, 2017
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Nicholas Wanjohi (Guest) on February 4, 2017
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Catherine Naliaka (Guest) on January 2, 2017
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Joseph Kitine (Guest) on November 15, 2016
ππ Neema za Mungu zisikose
Mary Njeri (Guest) on October 15, 2016
ππ Mungu wetu asifiwe
Mercy Atieno (Guest) on July 23, 2016
πβ¨π Mungu atajibu maombi yako
Nancy Akumu (Guest) on May 11, 2016
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Anthony Kariuki (Guest) on May 9, 2016
πππ
Nancy Kabura (Guest) on April 26, 2016
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Margaret Anyango (Guest) on February 9, 2016
πβ€οΈπ Tumshukuru Mungu kwa yote
Mary Njeri (Guest) on December 15, 2015
Sifa kwa Bwana!
John Mwangi (Guest) on November 1, 2015
Nakuombea π
Diana Mumbua (Guest) on July 8, 2015
πβ€οΈ Mungu ni mkombozi
Peter Mbise (Guest) on May 1, 2015
πβ€οΈπ Baraka za Mungu ziwe nawe