MAHITAJI
Wafer Powder/gram wafer (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) - vikombe 2
Maziwa ya Mgando Matamu ya Kopo - 2 vikombe
Nazi iliyokunwa - Β½ Kikombe
Chokoleti vipande vipande - 1 Kikombe
Njugu vipande vipande - Β½ Kikombe
Siagi - 227Β g
MAPISHI
Yeyusha siagi motoni kisha changanya na unga wa wafer acha kidogo motoni
Mimina katika treya unayochomea itandaze vizuri, kisha mimina maziwa juu yake pamoja na njugu vipande , nazi iliyokunwa na vipande vya chokoleti.
Choma (bake) kwenye oveni kwa moto wa 350ΒΊC kwa dakika 20.
Katakata tayari kwa kuliwa
No comments yet. Be the first to share your thoughts!