Ndiyo, kuna hatari kubwa ya kuambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI wakati wa kujamii ana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni.
Ngozi ya ndani ya sehemu ya haja kubwa ni laini sana na uwezekano wa kupata michubuko wakati wa kujamii ana ni mkubwa, kwa sababu hakuna majimaji kama ukeni yanoyorahisisha uume kuingia. Kwahiyo virusi vya UKIMWI ni rahisi sana kuingia mwilini mwa mwanamke kupitia kwenye michubuko hii ..
Pia ngono kwa njia ya mdomoni ( βkula koni, chumvi chumvi , kulamba ukeni) hatari sana kama mwanamke ana vidonda au michubuko mdomoni na mwanaume au vidonda au michubuko uumeni, wanaweza kuambukizana.
Watu wote wanashauriwa kutumia kondomu i ili kuzuia maambukizi.

Je, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI vinaambukiza kwa kujamiiana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni?

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!