Kwa vijana mara nyingine siyo rahisi kufahamu afanye nini mara anapopata ashiki (hamu) ya kutaka kujamii ana. Unaweza ukajaribu kujisahaulisha kwa kufanya mambo mengine kama kucheza michezo kujifu-nza, kujisomea, kuwasaidia wazazi kazi za nyumbani au kuungana na vijana wen-zako katika shughuli za vikundi katika jamii . Vijana wengine huoga maji ya baridi kuondoa ashiki.
Kujisikia hamu ya kutaka kujamii ana au uume kudinda haimaanishi kwamba ni lazima ujamii ane. Kujamii ana ni njia mojawapo tu ya kuonyesha mapenzi. Kuna njia nyingine ambazo hutumika, kwa mfano kubusu, kuongea, kushikana mikono, kukumbatiana na kushikanashikana.
Njia nyingine ya kutumia kumaliza hamu ni kupiga punyeto. Kupiga punyeto ni kitendo cha msichana kushikashika na kusugua taratibu kinembe chake mpaka anafikia mshindo au kitendo cha mvulana kusuguasugua uume wake mpaka akojoe manii . Watu wengi wanaopiga punyeto hufanya hivyo wakiwa peke yao. Kupiga punyeto hakuna madhara yoyote ya kiafya wala kiakili.
Kwa vyovyote vile, kama huwezi kabisa kuacha kujamii ana, hakikisha mapenzi yawe salama. Mapenzi salama ni yale yanayofanyika bila wasiwasi wa kupata mimba zisizotarajiwa, magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizo ya VVU na UKIMWI. Kwa upande mwingine, mapenzi salama yanaweza kuwa ni vitendo vya kumaliza hamu bila kuhusisha sehemu za siri za mwanamke na mwanaume kukutana. Kwa upande mwingine mapenzi ya uume kuingizwa ukeni yanakuwa pia salama i iwapo tahadhari imechukuliwa kwa maana kwamba kondomu i litumika.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!