Muumbaji wa penseli alipomaliza kuiumba penseli yake aliiambia mambo muhimu ya kuzingatia ili iweze kuwa penseli bora kabla hajaituma kuingia kazini kwa matumizi.
βKuna vitu sita unatakiwa uvitambue, β Aliiambia penseli,
βKabla sijakutuma kwenda kutumika, unatakiwa uviweke akilini vitu hivyo na usivisahau kamwe. Vitakusaidia siku zote na utakuwa penseli bora maisha yako yote.β
Alisema muumbaji wa penseli.
βMoja,β alianza kuvitaja,βutakuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi, lakini kama utakubali na utaruhusu kuongozwa na mkono wa mtumiaji wakoβ
βMbiliβ aliendelea kutoa nasaha, βutapata maumivu makali kutokana na kuchongwa mara kwa mara. Lakini vumilia kwani itakusaidia kuwa penseli bora na kuandika vizuri.β
βTatu, utakuwa na uwezo wa kusahihisha makosa utakayo yafanya.β
βNne, kitu pekee cha muhimu katika maisha yako ni kile kilicho ndani yako kwa sababu ndicho chenye uwezo wa kuandika.β
βTanoβ alisisitiza mtengenezaji penseli, βkwenye kila sehemu utakayotumika, utaacha alama yako. Hata ikiwa ni kwenye sehemu ngumu au mbaya kiasi gani, ni lazima alama yako ibaki.
βNa sitaβ, alimalizia muumbaji yule wa penseli, βipo siku utaisha na kupotea. Hivyo usiwe na hofu wala woga wala hudhuni uikaribiapo siku hiyo na ukaogopa kutimiza wajibu wako kwa kuhofia kuisha. Ukiogopa kuisha hautotumika na umuhimu wako hautonekana kwani hautatimiza wajibu uliombiwa kuufanyaβ
Penseli ilielewa na kuahidi kukumbuka na ikaingia sokoni ikiwa na dhamira yake moyoni.
Sasa tutumie mfano huo wa penseli katika maisha yetu halisi. Ukivikumbuka vitu hivyo sita ilivyopewa penseli, utaweza kuwa mtu bora kabisa kwenye maisha yako yote.
Moja, una uwezo wa kufanya mambo mengi na makubwa, kama utajiweka kwenye mikono ya Mungu.
Mbili, utakutana na magumu mengi ya kuumiza, lakini hayo ndiyo yatakufanya uwe mtu imara na bora, usiyakimbie.
Tatu, una uwezo wa kurekebisha makosa yote uliyoyafanya. Usijilaumu.
Nne, sehemu yako ya muhimu ni ile iliyo ndani yako kwani ndiyo inayoandika maisha yako. Ilinde.
Tano, kila sehemu utakayopita, acha alama yako kwa kufanya mazuri yatakayokufanya ukumbukwe daima, bila kujali mazingira. Timiza wajibu wako kwa kiwango cha juu.
Sita, tambua kuwa ipo siku utakufa. Usiwe na hofu yoyote juu ya kifo kwani ukiogopa kifo hutafanya lolote hapa duniani.
Tumia mfano huu wa penseli upate ujasiri wa kutambua kuwa wewe ni mtu muhimu hapa duniani na umeumbwa kwa madhumuni maalumu na umepewa uwezo mkubwa sana na Muumba wako! Ni wewe pekee mwenye uwezo wa kutimiza dhamira uliyotumwa na Muumba.
UBARIKIWE SANA.
Grace Minja (Guest) on April 16, 2024
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
James Kimani (Guest) on July 25, 2023
Rehema hushinda hukumu
Violet Mumo (Guest) on July 10, 2023
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Edward Lowassa (Guest) on June 20, 2023
Nakuombea π
Joyce Mussa (Guest) on December 25, 2022
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
David Sokoine (Guest) on April 13, 2022
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Henry Mollel (Guest) on October 19, 2021
Mwamini Bwana; anajua njia
Andrew Mahiga (Guest) on October 7, 2021
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Peter Mwambui (Guest) on August 6, 2021
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
John Lissu (Guest) on June 1, 2021
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Diana Mumbua (Guest) on April 22, 2021
Endelea kuwa na imani!
Nancy Kabura (Guest) on April 11, 2021
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Richard Mulwa (Guest) on September 17, 2020
Mungu ni mwema, wakati wote!
Edward Lowassa (Guest) on July 2, 2020
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
James Mduma (Guest) on July 1, 2020
Mwamini katika mpango wake.
Martin Otieno (Guest) on June 26, 2020
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Rose Amukowa (Guest) on February 22, 2020
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Samson Tibaijuka (Guest) on January 11, 2020
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Martin Otieno (Guest) on January 9, 2020
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Richard Mulwa (Guest) on November 25, 2019
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Charles Mboje (Guest) on July 25, 2019
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Raphael Okoth (Guest) on May 16, 2019
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Sarah Karani (Guest) on May 6, 2019
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Lydia Mzindakaya (Guest) on February 2, 2019
Dumu katika Bwana.
Benjamin Masanja (Guest) on January 19, 2019
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
John Malisa (Guest) on December 2, 2018
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Samuel Omondi (Guest) on September 12, 2018
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Thomas Mwakalindile (Guest) on August 11, 2018
Baraka kwako na familia yako.
Elizabeth Malima (Guest) on May 21, 2018
Neema na amani iwe nawe.
Simon Kiprono (Guest) on January 25, 2018
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Alice Jebet (Guest) on November 20, 2017
Katika imani, yote yanawezekana
John Lissu (Guest) on October 30, 2017
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Jane Muthoni (Guest) on September 23, 2017
Sifa kwa Bwana!
Andrew Mahiga (Guest) on June 3, 2017
Rehema zake hudumu milele
Diana Mumbua (Guest) on February 24, 2017
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Michael Onyango (Guest) on November 29, 2016
Mungu akubariki!
Betty Kimaro (Guest) on September 29, 2016
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Paul Kamau (Guest) on September 23, 2016
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Joseph Kitine (Guest) on June 8, 2016
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
John Lissu (Guest) on June 4, 2016
Neema ya Mungu inatosha kwako
Irene Akoth (Guest) on May 15, 2016
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Peter Mugendi (Guest) on May 6, 2016
Nguvu hutoka kwa Bwana
Betty Kimaro (Guest) on March 17, 2016
Tumaini ni nanga ya roho
Nicholas Wanjohi (Guest) on February 28, 2016
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Grace Wairimu (Guest) on January 10, 2016
Imani inaweza kusogeza milima
Samuel Were (Guest) on November 5, 2015
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Nicholas Wanjohi (Guest) on August 10, 2015
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Chris Okello (Guest) on May 7, 2015
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Esther Cheruiyot (Guest) on May 6, 2015
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Moses Kipkemboi (Guest) on April 14, 2015
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima