Zaburi 101:3
βSitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.β
Watu wengi wameanguka katika mtego huu wa Ibilisi na kujikuta wakifanya mambo ya "AIBU" wanapokuwa sehemu zao za Siri iwe ni chumbani au bafuni.
1. MAANA YA PICHA ZA NGONO
Neno PICHA ni kivuli cha mtu, watu, kitu n.k. PICHA si kitu halisi bali ni kivuli chake. Unaweza ukapewa PICHA ya mtu lakini usifahamu urefu wake au ni mfupi kiasi gani lakini sura yake ukawa umeiweka katika kumbukumbu yako. NGONO ni kitendo cha mtu, watu kufanya kitendo cha kujamiana (Tendo la Ndoa) na pia ni ile hali ya kuwa uchi wa mnyama. Kuangalia picha za ngono ni kitendo cha kuangalia watu wakifanya Matendo ya kujamiana iwe kwa njia ya asili, kinyume na maumbile au kufanya na wanayama. Kitendo hicho huleta kuchochea tamaa ya miili kiasi ambacho watu wengine hufanya mambo ya "AIBU" katika nyumba zao (Warumi 1:24-28). PICHA za NGONO zimeenea kila mahali kwa sasa, kwenye simu yako unaweza ukakutana na "uchafu" wa namna hiyo. Wahindi wao picha za ngono huziita "kachumbali" na unaweza ukamkuta Mhindi amekaa na familia yake anaangalia "kachumbali" wanadai inanogesha utamu wanapofika kitandani. Huko ni kujidanganya Mungu hakumletea Adamu PICHA ya NGONO bali alimletea mke ambaye watashirikiana naye kwenye Tendo Takatifu (Mwanzo 2:18, 21-25). Wakati mmoja Mfalme Daudi wakati watu wake wa vita wamekwenda vitani yeye akawa yuko ghorofani anaangalia "PICHA LIVE" ya NGONO mwanamke alikuwa akioga matokeo yake yakawa ni kufanya kitendo chenyewe na kuamua kumuua mume wa Bathsheba (2Samweli 11:2-27).βIkawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?ββ¦β¦β¦..
Kile kitendo cha Daudi "kuona" lilikuwa kosa kubwa la kiufundi katika akili yake likamchanganya. Ndivyo ilivyo kwa PICHA ZA NGONO lazima ukiangalia upate "UKICHAA" wa muda ukajikuta umeng'ang'ania sabuni au ndizi ukiwa unapiga punyeto. Ni aibu sana sana mtu mwenye heshima zako kama wewe labda wewe ni meneja, mkurugenzi, mtu mwenye Elimu yako ya maana unakutwa unaangaika sabuni, godoro au toy la jinsia ya kiume.
2. JE! KUANGALIA PICHA ZA NGONO NI DHAMBI?
Kuangalia picha za ngono "NI DHAMBI" kwa herufi kubwa. Katika Sheria ya Musa ilikuwa mtu anahesabika kuwa ametenda dhambi pale ambapo atakutwa akifanya kitendo hicho au kukiwa na mashahidi wawili au watatu atatakiwa kuhukumiwa sawasawa na Sheria husika. Kwenye dhambi ya uzinzi mtu alitakiwa apigwe mawe hadi afe sivyo kwa Sheria ya Kristo yenyewe inazungumzia juu ya kitendo cha "kutamani" tu unahesabika kuwa umefanyika DHAMBI (Mathayo 6:27-29, Waebrania 10:28). Tamaa mbaya ni dhambi kama dhambi nyinginezo. Kwa kawaida tamaa huja na ile tamaa huchukua mimba na baadaye huzaa dhambi (Yakobo 1:13-16). Kitendo cha kuangalia picha za ngono hupofusha "FIKRA" nzuri za mtu alizonazo. Mawazo machafu uanza kutawala katika ubongo wako hadi "USHUSHE" huo mzigo ulioko kwenye viungo vyako vya uzazi. Ahaaa ni hatari aiseeee. Wewe unayengalia picha za ngono Kama ndiyo starehe yako unaiharibi nafsi yako "unakuwa zezeta wa akili" Biblia inasema "taa ya Mwili jicho na jicho lako likiwa safi mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu mwili wako wote utakuwa na giza.."(Mathayo 6:22-23). Kwa wale wanandoa ni "MWIKO" kutumia picha za ngono ili kunogesha kufanya Tendo la Ndoa. Wewe mume unaye hapo "chombo" unakiona "live" na kimethibitishwa na Mungu mwenyewe sasa hiyo mipicha ya nini? Kila kiungo Mungu alikiweka kwa ajili ya kusudi maalum kama ni mdomo kwa ajili ya kuongea na kupitisha chakula na si kunyonya sehemu za Siri za mwenzi wako. Mungu ameweka sehemu ya "haja kubwa" kwa ajili ya kutolea uchafu uliotengenezwa na tumbo na si kiungo kingine kiende kukoroga "zege" hilo huo ni uchafu(Ufunuo 22:10-15).Warumi 1:26:27
βHivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.β
3. JINSI YA KUSHINDA DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO
PICHA ZA NGONO zinavutia sana kuziangalia ila zina maangamizo makubwa sana katika maisha yako. Lazima ufikie mahali kukata shauri ndani ya Moyo wako kuambatana na Mungu. Kusudi kubwa la shetani kuachilia mambo yake ya NGONO kwenye mitandao ili apate wafuasi wengi zaidi. Hakuna kitu unachoweza kukifanya katika simu za Android wengine wasikitambue. Kila unalolipitia na kuliangalia kwa Siri siku ya siku litaletwa hukumuni na Mungu mwenyewe (Warumi 2:16, Mhubiri 12:14)USHAURI WAKIVITENDO:
I) Yatie Nuru macho yako - Zaburi 13:3, 19:8 - Yaruhusu macho yako yaingiziwe nuru na Yesu. Chukua muda wa kutosha kuingiza PICHA zinazomhusu Mungu zaidi. Angalia wahubiri mbalimbali.II) Tazama mambo ya Adili(mema) - Zaburi 17:2-3 - Kuna nguvu kubwa sana tunapokuwa tunaangalia mambo mema. Vipindi vizuri vya neno la Mungu. PICHA zinazojenga siyo zinazoharibu fikra zetu.
III) Kumuomba Mungu afumbue macho yako - Zaburi 119:18, 146:8- Maombi ni muhimu ili kufanya macho yako kuona kusudi la Mungu na Kutambua uwepo wa shetani katika PICHA ZA NGONO.
IV) Weka maneno ya Mungu Mbele za macho yako - Mithali 4:20-21
Wakati wote soma neno la Mungu kupitia kifaa chochote cha ki-electronic ili uweze kumjua Mungu zaidi.
V) Macho yako yatazame Mbele - Mithali 4:25-27
Kutazama Mbele maana yake uwe na maono. Maono ni PICHA au TASWIRA ya Mbele ya maisha yako. Yeremia aliulizwa unaona nini naye akasema "anaona ufito wa mlozi" anaona kitu kizuri (Yeremia 1:11-12).
VI) Pendezwa na njia za Mungu - Mithali 23:26
Kuanzia sasa anza kupendezwa na njia za Mungu katika maisha yako. Acha kuzifuata njia zako katika kuufurahisha mwili wako wa PICHA zisizofaa.
VII) Tafuta watumishi wa Mungu ili wakufundishe - Isaya 48:17, 30:20-21
Kuna mambo ambayo yanatupa shida katika maisha yetu ni vizuri kuwaona waalimu ili watusaidie jinsi ya kutoka katika mtego huo.
VIII) Omba rehema na neema ya Yesu - Waebrania 4:16
Tunahitaji neema ya Mungu ili kushinda Hali hiyo ya kupenda KUANGALIA PICHA ZA NGONO na pia kufunguliwa kutoka katika vifungo hivyo vya pepo wa tamaa na mahaba.
Mungu atakubariki ukipeleka ujumbe huu kwa wengine
Mary Sokoine (Guest) on May 7, 2024
Nguvu hutoka kwa Bwana
Elizabeth Mrope (Guest) on April 27, 2024
Sifa kwa Bwana!
Joyce Nkya (Guest) on February 21, 2024
Dumu katika Bwana.
Rose Mwinuka (Guest) on January 28, 2024
Mwamini katika mpango wake.
Edwin Ndambuki (Guest) on December 23, 2023
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Moses Kipkemboi (Guest) on November 1, 2023
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Charles Mchome (Guest) on October 21, 2023
Rehema hushinda hukumu
Irene Akoth (Guest) on August 11, 2023
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
George Ndungu (Guest) on December 31, 2022
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Dorothy Nkya (Guest) on December 3, 2022
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Jane Muthoni (Guest) on August 17, 2022
Katika imani, yote yanawezekana
Diana Mumbua (Guest) on April 9, 2022
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
George Mallya (Guest) on March 28, 2022
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Paul Ndomba (Guest) on March 14, 2022
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Joseph Mallya (Guest) on December 14, 2021
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
George Wanjala (Guest) on October 30, 2021
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Ruth Wanjiku (Guest) on October 20, 2021
Nakuombea π
Irene Akoth (Guest) on October 7, 2021
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Jacob Kiplangat (Guest) on April 1, 2021
Endelea kuwa na imani!
Lydia Mutheu (Guest) on March 26, 2021
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Mary Kendi (Guest) on January 22, 2021
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Tabitha Okumu (Guest) on January 18, 2021
Imani inaweza kusogeza milima
Chris Okello (Guest) on November 30, 2020
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Emily Chepngeno (Guest) on November 23, 2020
Mwamini Bwana; anajua njia
George Mallya (Guest) on November 10, 2020
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Mary Sokoine (Guest) on August 25, 2020
Mungu ni mwema, wakati wote!
Jane Muthui (Guest) on December 24, 2019
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
James Kawawa (Guest) on November 7, 2019
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Peter Tibaijuka (Guest) on December 23, 2018
Rehema zake hudumu milele
Thomas Mwakalindile (Guest) on November 30, 2018
Neema ya Mungu inatosha kwako
Mary Sokoine (Guest) on September 8, 2018
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Grace Njuguna (Guest) on May 19, 2018
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Irene Makena (Guest) on January 22, 2018
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Lydia Mahiga (Guest) on November 10, 2017
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Edwin Ndambuki (Guest) on October 12, 2017
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Charles Mboje (Guest) on July 25, 2017
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
James Mduma (Guest) on June 23, 2017
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Simon Kiprono (Guest) on May 21, 2017
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Janet Mbithe (Guest) on April 13, 2017
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Samson Tibaijuka (Guest) on October 18, 2016
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Chris Okello (Guest) on September 28, 2016
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Wilson Ombati (Guest) on August 18, 2016
Neema na amani iwe nawe.
Anna Sumari (Guest) on August 3, 2016
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Violet Mumo (Guest) on July 21, 2016
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Stephen Amollo (Guest) on June 30, 2016
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Samuel Were (Guest) on May 24, 2016
Mungu akubariki!
Lucy Kimotho (Guest) on March 19, 2016
Tumaini ni nanga ya roho
Stephen Kikwete (Guest) on July 7, 2015
Baraka kwako na familia yako.
Hellen Nduta (Guest) on May 13, 2015
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Victor Kimario (Guest) on April 7, 2015
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu