Sidebar with Floating Button
AckySHINE Katoliki
☰
AckyShine

Nafasi ya Bikira Maria Katika Kanisa Katoliki

Featured Image
Kanisa katoliki linamthamini Bikira Maria kama Mama wa Mungu, Mama wa Kristu, Mama wa Mkombozi pia Mama wa uhai kuna maneno kadhaa hutumika pia kufafanua zaidi hiyo heshima mfano HYPERDULIA zaidi ya…. Bikira Maria tunamheshimu zaidi ya watakatifu, PROTODULIA ikiwa na maana ya heshima kwa Bikira Maria zaidi ya Mt. Yoseph na pia LATRIA likiwa na maana ya heshima kwa Mungu peke yake kwani ndani yake kuna kunakuabudu pia!!!
🌻Bikira Maria anatuelekeza kwa mwanae kama alivyo waelekeza waliokuwa harusini kana lolote atakalo waambieni fanyeni Yoh.2:5
🌻Bikira Maria ni Mama wa uhai, mlei, muuguzi wa kwanza/ muhudumu wa kwanza alienda kwa haraka kuanzisha kliniki ndogo nyumbani mwa Zakaria amhudumie Elizabeti Mama wa Yohane Mbatizaji aliyekuwa mjamzito
🌻Tunasema Bikira Maria ni mzazi bora wa kuiga kwani alitetea uhai, Mama huyo hakutoa mimba japo misuko suko ilikuwa mingi Mfano maneno ya pembeni ya watu kwa vile mimba haikuwa ya Yoseph mumewe, hali mbaya ya uchumi na ukiangalia hivyo Familia takatifu ya Maria na Yosefu haikuwa na hali nzuri kifedha Lk. 2:22-24 Bikira Maria alivumilia hali hiyo kwani angetoa angemuua Mkombozi wetu, na sababu hizo ndizo hata dunia ya leo zina wafanya watu watoe mimba Ikiwa kutoa ni kuua na hatimaye tunapoteza
-Mama wa watoto wa kesho
-Baba wa watoto wa kesho
-Padre wa kesho
-Mtawa wa kesho
-Raisi wa kesho n.k
🌻Bikira Maria alikombolewa kwaajili ya mastahili ya mwanae tena kwa namna ya pekee sana, aliangaliwa na…..
-Baba kama Binti yake Mpenzi
-Mwana, mama mheshimiwa
-Roho Mtakatifu, hekalu lake
SWALI: Sisi nasi kama tunaamini heshima anayopaswa kupewa Bikira Maria ni sawa na kwamba pia sisi tunaelewa kwamba tumekombolewa kupitia yeye?
Nafasi ya Bikira Maria Katika Biblia ya kanisa katoliki
🌻Sisi kama wanakatoliki tunasema Bikira Maria ni Mama wa Mungu kweli kwa kzingatia mambo makuu mawili ambayo ni kama ifuatavyo:
1. Kwanza lazima Bikira Maria awe mama halisi wa Yesu
2. Pili ni kuwa Yesu aliyemzaa Ni Mungu.
1. BIKIRA MARIA NI MAMA HALISI WA YESU
🌻Sote tunapaswa kufahamu kama kweli BiKira Maria ni Mama halisi wa Yesu kupitia vifungu vifuatavyo na hii ndio nguzo pekee ya kujinasua katika makundi yasiyo amini kama Bikira Maria anastahili heshima twende pamoja sasa:
-Lk. 1:30-31 neno linasema
Malaika akamwambia ' usiogope Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu, tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume na jina lake utamwita Yesu kwahiyo ni dhahiri kwamba huyu ni mama halisi wa Yesu ambae sisi tunamuimba kila leo.
-Mt. 1:18 neno linasema:
kuzaliwa kwake Yesu Kristu kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu huu ni ushahidi tosha kuwa Bikira Maria ni Mama halisi wa Yesu kwani ndiye aliye pewa hadhi zaidi ya wanawake wote kuzaa kitakatifu Mwana wa Mungu.
-Rom 1:3 neno linasema hivi
yaani habari za mwanawe, aliye zaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili ikikumbuka wakati tunasali nasadiki kama sehemu ya kuikiri imani yetu kuna maneno huwa tunatamka kwamba akapata mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwake yeye Bikira Maria, akawa mwanadamu hivyo ni connection nzurii sana kwetu kuendelea kumheshimu Mama yetu Maria kwa kutuunganisha na Mungu kwa ubinadamu wetu!
-Nabii Isaya 7: 14 anatabili:
kwahiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara, tazama , Bikira atachukua mimba , atazaa mtoto mwanamume naye atamwita jina lake Imanueli(yaani Mungu pamoja nasi tazama maneno haya yalitabiliwa na Nabii huyu juu ya mama huyu Mtakatifu atakavyo tuletea ukombozi kwann tusimheshimu na kumtetea mpaka tunapotoshwa?
- Mate 1:14 neno linasema
hawa wote walikuwa wakidumu kwa Moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake na mariamu mama yake Yesu na ndugu zake wanawake wengine walihesabiwa pamoja lakini mama Maria anasemwa kwa upeke yake ktokana na uzito wake kupita wanawake wengine kwani ndiye mama wa Yesu Kristu ni heshima kubwa!!!
2. Yesu ni Mungu na Bikira Maria ni Mama wa Mungu
🌻katika sehemu ya jambo letu la pili ni kwamba je alichozaa Mama Maria ni Mungu? Kama ni muhimu kujua hilo hebu tuone uthibitisho wa hili kupitia baadhi ya vifungo bdani ya Biblia zetu ambazo pia wenzetu wanaopinga Habari ya mama yetu Maria waone twende pamoja:
-Yoh. 1:1-2 neno linasema
hapo mwanzo kulikuwako Neno naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu Huyo Mwanzo alikuwako kwa Mungu kwa maneno hayo na ukiendelea kusoma ukitafakari utaona anaezungumziwa na Yesu Kristu ambaye ndie nuru halisi ya ulimwengu ni ndie uzima wetu kwa Mungu na huyu Yesu basi alizaliwa na Bikira Maria hivyo alichozaa Maria ni Mungu kweli.
-Rom 9:6 neno linasema:
ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya Mwili, ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu mwenye kuhimidiwa milele. Amina hayo ni maneno yanayo tambulisha koo ya kibinadamu kwamba ndiko pamoja ubinadamu wetu amezaliwa Mungu soma injili ya mtakatifu Mathayo sura ya kwanza aya ya kwanza na kuendelea habari za ukoo wa Yesu naamini hapa Tmcs tunapasikia sana!!!
- Fil 1:6-7 neno linasema:
nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu nakuendelea……….. maneno hayo yanaonyesha kuwa Kristo ndie mambo yote katika kuupata uzima wa milele na huyu anae onekana ni mwisho wa yote amaezaliwa na Mwanamke Maria.
-Mitume nao walikiri kuwa Yesu ni Mungu mtu Yoh. 20:28
Tomaso akajibu, akamwambia Bwana wangu na Mungu wangu kutokana na matendo na kazi ya Yesu Kristu iliwafanya mitume waone kuwa ufalme wake sio wa dunia hii tu bali ni wa milele na kazi yake ni Takatifu na sio hapo tu kumbuka pia wale wanafunzi walio kuwa wanasema yatufaa sasa tujenge vibanda vitatu kimoja cha Musa na kingine cha Eliya mara sauti ikasikika ikisema huyu ni mwanangu mpendwa wangu msikieni yeye na mara akageuka sura maneno hayo ilikuwa ni uthibitisho juu ya umungu wa Yesu Kristu ambaye huyu alizaliwa na Bikira Maria.
- Lk. 1:35 neno linasema
Malaika akajibu akamwambia "Roho Mtakatifu atakujilia juu yako , na nguvu zake aliyejuu zitakufunika kama kivuli, kwasababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu mwana wa Mungu" haya maneno ni dhahiri yanatufundisha kwamba Bikira Maria alimzaa Mungu katika ubinadamu wake.
-Gal. 4:4 neno linasema:
huyu ni mwana wa Mungu, ni mwana wa mwanamke, huyo mwana wa Mungu, pia ni mwana wa Maria tuseme nn sasa tusiyumbishwe yumbishwe na maneno yasiyo na tija juu ya mama Maria kwani kupitia yeye tunakuwa salama katika Roho na Mwili
Maneno ya Busara
-Mt. Germanus alishwahi kusema *Maria mahali pa kuishi pa Mungu*
-Mt. Jerome alisema Maria Hekalu la mwili wa Bwna
-Martine Luther, hata baada ya kujiengua kutoka kanisa katoliki alikiri kuwa Bikira maria ni Mama wa Mungu akisema:
hakuna jambo kubwa zaidi ya hili kuwa Bikira Maria alipata kuwa Mama wa Mungu ambalo kwalo zinatoka zawadi(heri) kubwa na Nyingi ambazo amepewa inakuaje leo tusione umhimu wa heshima kwa mama huyu?
-Mt. Bernado alisema Maria alimpendeza Mungu kwa ubikira wake, na alichukua mimba kwa unyenyekevu wake
MWISHO: FUNDISHO MAISHANI
- Sote ambao tupo chini ya utawala wa Yesu Kristo tunawajibu wa kutetea uhai kwa nguvu zote tukipiga marufuku utoaji mimba kwa visingizio mbalimbali
- Eva alishindwa kumtii Mungu akaleta mauti lakini Bikira Maria alitii kubaki mwamnifu na kumtunza Kristu na hatimaye ameleta uhai na neema zote , akina dada na mama zetu igeni mfano wa Maria na Elizabeti katika malezi bora!!
-Sisi sote tuliowabatizwa tunapapaswa kuwa wanyenyekevu kama Maria na familia yao yote kwani unyenyekevu umejengwa juu ya upendo pia ni mama wa fadhila nyingi utii, uchaji, ibada, uvumilivu, kiasi, upole na amani.

Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?

Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.

Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;

1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu

Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, "Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe." 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, "Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho." 34 Maria akamjibu, "Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?" 35 Malaika akamjibu, "Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)

2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi

19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, "Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa." 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: "Ataitwa Mnazare." Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.

3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12

Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, "Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni." 49 Yeye akawajibu, "Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?" 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.

4. Kukosekana kwa neneo "Binamu" kwenye lugha ya Yesu

Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno "Binamu" kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?" (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.

5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja

Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.

6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake

Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?" (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, "Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba." (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.

7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye

26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: "Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao." 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: "Tazama, huyo ndiye mama yako." Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Simon Kiprono (Guest) on June 25, 2024

Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu

Anna Sumari (Guest) on March 26, 2024

Baraka kwako na familia yako.

Michael Onyango (Guest) on March 13, 2024

Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia

Joseph Kawawa (Guest) on March 11, 2024

Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia

John Mwangi (Guest) on February 9, 2024

Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao

Josephine Nekesa (Guest) on November 10, 2023

Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi

Stephen Kikwete (Guest) on October 23, 2023

Mungu ni mwema, wakati wote!

Jackson Makori (Guest) on September 24, 2023

Katika imani, yote yanawezekana

David Kawawa (Guest) on August 20, 2022

Neema ya Mungu inatosha kwako

Nancy Komba (Guest) on April 22, 2022

Rehema hushinda hukumu

Peter Mugendi (Guest) on April 17, 2022

Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi

John Kamande (Guest) on March 17, 2022

Ahadi za Mungu ni za kweli daima

Fredrick Mutiso (Guest) on January 29, 2022

Imani inaweza kusogeza milima

Victor Mwalimu (Guest) on January 17, 2022

Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe

Elizabeth Mtei (Guest) on October 12, 2021

Bwana yuko karibu na wote wanaomwita

James Kawawa (Guest) on September 14, 2021

Tumaini ni nanga ya roho

Alice Jebet (Guest) on August 31, 2021

Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha

Charles Mboje (Guest) on August 30, 2021

Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi

Esther Nyambura (Guest) on July 22, 2021

Neema na amani iwe nawe.

Edward Lowassa (Guest) on March 25, 2021

Mwamini katika mpango wake.

Betty Cheruiyot (Guest) on February 27, 2021

Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu

Grace Njuguna (Guest) on June 20, 2020

Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu

Dorothy Mwakalindile (Guest) on May 27, 2020

Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe

Alex Nakitare (Guest) on December 28, 2019

Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake

Betty Cheruiyot (Guest) on September 16, 2019

Sifa kwa Bwana!

Irene Makena (Guest) on May 1, 2019

Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni

Edward Chepkoech (Guest) on February 28, 2019

Hauko peke yako; Mungu yuko nawe

Agnes Lowassa (Guest) on January 28, 2019

Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia

Mary Sokoine (Guest) on November 23, 2018

Wakati wa Mungu ni kamilifu

Sarah Mbise (Guest) on November 16, 2018

Dumu katika Bwana.

Michael Mboya (Guest) on October 7, 2018

Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika

Edwin Ndambuki (Guest) on August 20, 2018

Nguvu hutoka kwa Bwana

Bernard Oduor (Guest) on July 21, 2018

Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi

David Musyoka (Guest) on June 5, 2018

Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako

Grace Njuguna (Guest) on November 28, 2017

Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote

Stephen Amollo (Guest) on October 19, 2017

Mwamini Bwana; anajua njia

Lydia Mutheu (Guest) on August 10, 2017

Tembea kwa imani, si kwa kuona

Mariam Kawawa (Guest) on May 22, 2017

Rehema zake hudumu milele

Lydia Mzindakaya (Guest) on December 4, 2016

Nakuombea πŸ™

Kenneth Murithi (Guest) on October 3, 2016

Kwa Mungu, yote yanawezekana

Joyce Nkya (Guest) on September 29, 2016

Mungu akubariki!

Henry Sokoine (Guest) on August 26, 2016

Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida

Peter Otieno (Guest) on August 22, 2016

Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako

Ruth Wanjiku (Guest) on June 10, 2016

Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia

Rose Mwinuka (Guest) on May 31, 2016

Upendo wa Mungu haukosei kamwe.

Francis Mrope (Guest) on May 29, 2016

Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima

Agnes Njeri (Guest) on May 5, 2016

Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine

Francis Mrope (Guest) on May 3, 2016

Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha

Wilson Ombati (Guest) on January 19, 2016

Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini

Mary Kidata (Guest) on April 27, 2015

Endelea kuwa na imani!

Related Posts

Kuomba Msamaha katika Huruma ya Mungu: Njia ya Uongofu

Kuomba Msamaha katika Huruma ya Mungu: Njia ya Uongofu

  1. Kuomba Msamaha ni Njia ya Uongofu

Katika maisha yetu, tunakosea wakati mwingi... Read More

Huruma ya Mungu: Faraja na Ufariji katika Majaribu

Huruma ya Mungu: Faraja na Ufariji katika Majaribu

Huruma ya Mungu: Faraja na Ufariji katika Majaribu

Huruma ya Mungu ni zawadi kubwa kutoka ... Read More

Huruma ya Mungu: Chemchemi ya Upendo Usiokwisha

Huruma ya Mungu: Chemchemi ya Upendo Usiokwisha

Huruma ya Mungu: Chemchemi ya Upendo Usiokwisha

  1. Kama Mkristo Katoliki, tunajua k... Read More

Ishara ya Msalaba

Ishara ya Msalaba

Read More
Kuishi katika Huruma ya Mungu: Njia ya Utakatifu na Ukarimu

Kuishi katika Huruma ya Mungu: Njia ya Utakatifu na Ukarimu

Kuishi katika Huruma ya Mungu: Njia ya Utakatifu na Ukarimu

  1. Kuishi katika huruma... Read More

Je, Kanisa Katoliki linawahimiza waamini kuishi maisha matakatifu na kuwa mashuhuda wa Injili?

Je, Kanisa Katoliki linawahimiza waamini kuishi maisha matakatifu na kuwa mashuhuda wa Injili?

Je, Kanisa Katoliki linawahimiza waamini kuishi maisha matakatifu na kuwa mashuhuda wa Injili? Ji... Read More

Je, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria?

Je, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria?

Je, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria?

Ndio, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria... Read More

Huruma ya Mungu: Ukarimu Usiokuwa na Kikomo

Huruma ya Mungu: Ukarimu Usiokuwa na Kikomo

Huruma ya Mungu: Ukarimu Usiokuwa na Kikomo

Katika maisha yetu ya kila siku, tunakabiliana... Read More

Ishi kama Penseli ili uwe mtu bora

Ishi kama Penseli ili uwe mtu bora

Muumbaji wa penseli alipomaliza kuiumba penseli yake aliiambia mambo muhimu ya kuzingatia ili iwe... Read More

Huruma ya Mungu: Chemchemi ya Upendo Usiokwisha

Huruma ya Mungu: Chemchemi ya Upendo Usiokwisha

Huruma ya Mungu ni chemchemi ya upendo usiokwisha. Tunaishi katika dunia ambayo imejaa shida na m... Read More

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu sakramenti ya Ndoa?

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu sakramenti ya Ndoa?

Sakramenti ya Ndoa ni muhimu sana katika Kanisa Katoliki. Kwa mujibu wa imani ya Kanisa, ndoa ni ... Read More

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu kuombea wafu?

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu kuombea wafu?

Ni jambo la kawaida kwa Kanisa Katoliki kuombea wafu. Kuombea wafu ni sehemu ya imani yetu kama W... Read More

πŸ“˜ About πŸ”’ Login πŸ“ Register πŸ“ž Contact