Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 2 Vikombe
Cocoa ya unga - 1 Kijiko cha supu
Sukari ya hudhurungi - 1 Kikombe
Siagi - ΒΎ Kikombe
Yai - 1
Molasses - ΒΌ Kikombe
Baking soda - 2 vijiko vya chai
Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai
Tangawizi mbichi - 1 kijiko cha supu
Karafuu ya unga - Β½ kijiko cha chai
Chumvi Β½ kijiko cha chai
Vanilla Β½ kijiko cha chai
MAANDALIZI
Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando. Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti. Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili. Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri. Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike. Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri. Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.) Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka
Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.
Oka katika oven 350ΒΊF kwa muda wa dakika 15.
Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi. Panga kwenye sahani tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:02 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour) 1/4 Kitunguu kikubwa (chopped/slice onion) 1 Yai (egg) 1 Chumvi (salt) Mafuta (cooking oil)
Matayarisho
Tia unga, chumvi na maji kiasi katika bakuli kisha koroga mpaka madonge yote yaondoke. Baada ya hapo tia yai na vitunguu kisha koroga tena mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. baada ya hapo choma chapati zako kama kawaida (jinsi ya kuchoma unaweza kuangalia kwenye recipe yangu ya chapati za maji katika older posts) na baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Tambi (spaghetti 1/2 ya packet) Mafuta (vegetable oil) Sukari (sugar 1/2 kikombe cha chai) Hiliki (cardamon 1/2 kijiko cha chai) Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai) Tui la nazi (coconut oil 1 kikombe cha chai) Maji kiasi
Matayarisho
Tia mafuta kiasi kwenye sufuria kisha ibandike jikoni (katika moto wa wastani) yakisha pata moto kiasi tia tambi na uanze kuzikaanga kwa kuzigeuzageuza kila mara mpaka zitakapokuwa za yangi ya light brown. baada ya hapo ipua na umwage mafuta ya kwenye tambi (bakiza kidogo sana kwani usipofanya hivyo tambi zitakuwa na mafuta sana) Baada ya hapo zirudishe jikoni na kisha utie hiliki, chumvi, sukari, tui la nazi na maji kiasi. Zifunike kisha ziache zichemke mpaka maji yakauke. Baada ya hapo zigeuze na uzipike mpaka ziive. Nahapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:47 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vitumbua ni aina ya vitafunwa vya chai ambavyo hutengenezwa kwa kutumia unga wa mchele. Kiasili vitumbua ni chakula ambacho hupendelewa sana na watu wa pwani. Na mara nyingi wamekuwa wakipika kwa kuchanganya na nazi ili kuvifanya view na ladha nzuri zaidi
Mahitaji:
Unga wa mchele Β½ kg Sukari vijiko 4 vya mezani Tui bubu la nazi Mafuta ya kupikia Unga wa hiliki Β½ kijiko cha chai Hamira kijiko 1 cha chai Chuma cha vitumbua
Maandalizi:
Chukua unga wa mchele na weka kwenye bakuli au sufuria ya kilo moja Weka hamira kisha weka sukari kisha miminia tui katika mchanganyiko wako Weka hiliki koroga hadi view uji mzito Acha uji huo kwa muda wa saa moja hadi uumuke, mara nyingi kuumuka kunategemea na hali ya hewa, Baada ya hapo weka mafuta kijiko kimoja cha chakula kila kishimo acha yapate moto Kisha kaanga virumbua vyako
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kambale 2 Nazi kopo 1 Nyanya kopo 1 Vitunguu 2 Curry powder 1 kijiko cha chai Turmaric 1/2 kijiko cha chai Binzari nyembamba ya unga 1/2 kijiko cha chai Swaum/ tangawizi 1 kijiko cha chakula Giligilani kiasi Limao 1/2 Chumvi Olive oil
Matayarisho
Loweka samaki katika maji ya moto kwa muda wa muda wa nusu saa.Baada ya hapo Saga pamoja nyanya, vitunguu, swaum na tangawizi kisha vibandike jikoni na uvipike mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta. Pika mpaka nyanya zitengane na mafuta kisha tia spice zote.Zipike kwa muda mdogo kisha tia tui la nazi, maji kiasi, samaki, pilipili nzima, chumvi na kamulia limao. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na samaki pia wawe wameiva na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo ipua kisha tia giligilani iliyokatwa na mchuzi utakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuulia kwa chochote kile upendacho. Mi hupendaga kuulia na ugali mlaiiini au na wali pia.
Jinsi ya kutengeneza Biskuti Ya Keki Kavu (Shortcake)
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 2 Magi (vikombe vya chai)
Sukari iliyosagwa - 2/3 Magi (kikombe cha chai)
Siagi - 220Β g
Unga wa mchele - Β½ Magi
Yai -1
Vanilla - 1 kijiko cha chai
MAANDALIZI
Changanya vitu vyote hivyo kwenye bakuli mpaka unga ushikamane. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30Β cm au (8 in kwa 12 in) Choma kwenye moto 325ΛC kwa muda wa saa nzima au mpaka ibadilike kuwa rangi ya dhahabu. Epua acha ipoe kisha kata vipande kama mstatili, weak kwenye sahani tayari kunywewa na chai.
NYONGEZA
Kwa unga huo huo unaweza kutengeneza vibiskuti vya duara duara.