Mahitaji
Daal (lentils) nyekundu au/na kijani - 1 Kikombe kikubwa
Bizari ya manjano ya unga - 1/2 Kijiko cha chai
Pili pili ya unga - 1/2 kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Maji ya ndimu - 3 Vijiko vya supu
Kitunguu - 1 kiasi
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 Kijiko cha chai
Bizari ya unga (cummin powder) - 1 Kijiko cha chai
Mafuta ya kukaangia - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Safisha daal kwa kutoa mawe ikiwa yapo, kisha osha na roweka dakika 15 hivi.
Kisha chemsha kwa kutia maji, bizari ya manjano, chumvi, pili pili ya unga na maji ya ndimu hadi iive na kuvurujika.
Halafu chukua kisufuria na kaanga kitungu, kisha thomu na mwisho tia bizari ya pilau.
Kisha mimina mchanganyiko wa kitunguu kwenye sufuria ya daal (iliyokwisha iiva)na uchanganye na iwache motoni kidogo itokote.
Ukipenda mimina mchanganyiko kwenye blenda na usage mpaka iwe laini.
Tia kwenye bakuli na itakuwa tayari kuliwa na wali na samaki ukipenda
No comments yet. Be the first to share your thoughts!