SOMO 1 - Kumb. 4:1, 5-9
Musa aliwaambia makutano: Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu niwafundishazo, ili mmzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wa baba zenu.Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama Bwana, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwmingiayo ili kuimiliki. Zishikeni basi,5 mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikiaโต amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili. Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo? Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo.
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako.
Neno la Bwanaโฆ Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI - Zab. 147:12-13, 15-16, 19-20 (K) 12(K)
Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.Msifu Bwana, Ee Yerusalemu;
Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.Maana ameyakaza mapingo ya malango yako,Amewabariki wanao ndani yako. (K)
Huipeleka amri yake juu ya nchi,Neno lake lapiga mbio sana.
Ndiye atoaye theluji kama sufu,Huimwaga barafu yake kama majivu. (K)
Humhubiri Yakobo neno lake,Na Israeli amri zake na hukumu zake.
Hakulitendea taifa lolote mambo kama hayo,Wala hukumu zake hawakuzijua. (K)
SHANGILIO
Mbegu neno la Mungu, mpanzi lakini ni Kristu; Yeyote ampataye, ataishi milele.
INJILI - Mt. 5:17-19
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Msidhani kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka hata yote yatimie. Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme mbinguni.
Neno la Bwanaโฆ Sifa kwako Ee Kristo.
Rose Waithera (Guest) on February 6, 2024
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Alex Nyamweya (Guest) on November 26, 2023
Rehema hushinda hukumu
Francis Njeru (Guest) on November 23, 2023
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Nancy Kabura (Guest) on October 13, 2023
Baraka kwako na familia yako.
Catherine Mkumbo (Guest) on December 24, 2022
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Elijah Mutua (Guest) on July 7, 2022
Nakuombea ๐
Charles Mchome (Guest) on May 14, 2022
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Victor Sokoine (Guest) on April 5, 2022
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Richard Mulwa (Guest) on July 20, 2021
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Esther Nyambura (Guest) on July 11, 2021
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Charles Wafula (Guest) on June 29, 2021
Neema ya Mungu inatosha kwako
John Mwangi (Guest) on June 24, 2021
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Diana Mallya (Guest) on June 12, 2021
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Elizabeth Malima (Guest) on April 8, 2021
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Ann Awino (Guest) on February 21, 2021
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
John Mushi (Guest) on February 6, 2021
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Bernard Oduor (Guest) on January 20, 2021
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Esther Nyambura (Guest) on December 17, 2020
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Vincent Mwangangi (Guest) on December 8, 2020
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Simon Kiprono (Guest) on August 10, 2020
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Frank Macha (Guest) on June 25, 2020
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Andrew Mahiga (Guest) on May 25, 2020
Mungu ni mwema, wakati wote!
Victor Kimario (Guest) on April 16, 2020
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Esther Cheruiyot (Guest) on February 7, 2020
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Josephine Nekesa (Guest) on January 31, 2020
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
John Malisa (Guest) on January 10, 2020
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Francis Mrope (Guest) on December 25, 2019
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Joseph Njoroge (Guest) on December 24, 2019
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Patrick Kidata (Guest) on October 21, 2019
Neema na amani iwe nawe.
Charles Wafula (Guest) on June 18, 2019
Mwamini katika mpango wake.
Esther Nyambura (Guest) on April 10, 2019
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Wilson Ombati (Guest) on October 3, 2018
Tumaini ni nanga ya roho
Alice Mrema (Guest) on September 18, 2018
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Fredrick Mutiso (Guest) on August 5, 2018
Endelea kuwa na imani!
George Ndungu (Guest) on June 14, 2018
Imani inaweza kusogeza milima
Josephine Nekesa (Guest) on May 9, 2018
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Agnes Sumaye (Guest) on May 5, 2018
Dumu katika Bwana.
Nancy Komba (Guest) on December 11, 2017
Mungu akubariki!
Peter Mwambui (Guest) on December 3, 2017
Sifa kwa Bwana!
Ann Awino (Guest) on November 24, 2017
Mwamini Bwana; anajua njia
Ruth Kibona (Guest) on November 3, 2017
Nguvu hutoka kwa Bwana
Anna Mahiga (Guest) on September 28, 2017
Wakati wa Mungu ni kamilifu
George Wanjala (Guest) on August 16, 2017
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Rose Amukowa (Guest) on February 28, 2017
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Nancy Kabura (Guest) on May 21, 2016
Katika imani, yote yanawezekana
Nancy Kawawa (Guest) on February 9, 2016
Rehema zake hudumu milele
Anna Mchome (Guest) on November 29, 2015
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Thomas Mwakalindile (Guest) on August 24, 2015
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Agnes Sumaye (Guest) on July 17, 2015
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Nicholas Wanjohi (Guest) on June 18, 2015
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao