SOMO 1
Hes. 21:4-9
Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia. Watu wakamnungβunikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu.
Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnungβunikia Mungu, na wewe; utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa. Basi, Musa akawaombea watu. Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo, ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.
Neno la Bwana⦠Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 102:1-2, 15-20 (K) 1
(K) Ee Bwana, usikie kuomba kwangu, kilio changu kikufikie.
Ee Bwana, usikie kuomba kwangu,
Kilio change kikufikie,
Usinifiche uso wako siku ya shida yangu,
Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi. (K)
Kisha mataifa wataliogopa jina la Bwana,
Na wafalme wote wa dunia utukufu wako;
Bwana atakapokuwa ameijenga Sayuni,
Atakapoonekana katika utukufu wake,
Atakapoyaelekea maombi yake aliye mkiwa,
Asiyadharau maombi yao. (K)
Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo,
Na watu watakaoumbwa watamsifu Bwana.
Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu,
Toka mbinguni Bwana ameiangalia nchi,
Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa,
Na kuwafungua walioandikiwa kufa. (K)
SHANGILIO
Yn. 8:12
Β
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, yeye anifuataye, atakuwa na nuru ya uzima.
INJILI
Β
Yn. 8:21-30
Β
Yesu aliwaambia Mafarisayo: Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi hamwezi kuja.
Basi, Wayahudi wakasema, Je! Atajiua! Kwa kuwa asema, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja?
Akawaambia, Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu. Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.
Basi wakamwambia, U nani wewe? Yesu akawaambia, Hasa neno lilo hilo ninalowaambia. Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake ndiyo ninenayo katika ulimwengu.
Wala hawakutambua ya kuwa anawatajia Baba. Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo. Naye aliyenipeleka yu pamoja nami; hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.
Naye alipokuwa akisema hayo, wengi walimwamwini.
Neno la Bwana⦠Sifa kwako Ee Kristo.
Michael Onyango (Guest) on July 17, 2024
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Margaret Anyango (Guest) on April 16, 2024
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Anna Kibwana (Guest) on January 20, 2024
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Lucy Mahiga (Guest) on November 23, 2023
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Alice Mrema (Guest) on July 29, 2023
Imani inaweza kusogeza milima
Rose Mwinuka (Guest) on July 26, 2023
Neema na amani iwe nawe.
Nora Lowassa (Guest) on July 9, 2023
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Susan Wangari (Guest) on May 7, 2023
Mungu akubariki!
Irene Akoth (Guest) on February 5, 2023
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Betty Cheruiyot (Guest) on November 20, 2022
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Monica Adhiambo (Guest) on October 21, 2022
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Anna Malela (Guest) on September 28, 2022
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Nora Lowassa (Guest) on August 22, 2022
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Charles Wafula (Guest) on July 5, 2022
Tumaini ni nanga ya roho
Monica Nyalandu (Guest) on April 8, 2022
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Tabitha Okumu (Guest) on December 10, 2021
Rehema hushinda hukumu
Frank Macha (Guest) on November 11, 2021
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Robert Ndunguru (Guest) on August 2, 2021
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Nora Kidata (Guest) on July 6, 2021
Dumu katika Bwana.
John Lissu (Guest) on June 19, 2021
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Alice Mwikali (Guest) on May 29, 2021
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Samson Mahiga (Guest) on May 4, 2021
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Elizabeth Mrope (Guest) on April 19, 2021
Endelea kuwa na imani!
Rose Waithera (Guest) on April 1, 2021
Sifa kwa Bwana!
Jane Muthoni (Guest) on November 28, 2020
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Henry Mollel (Guest) on September 4, 2020
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Christopher Oloo (Guest) on May 8, 2020
Nguvu hutoka kwa Bwana
Andrew Mahiga (Guest) on April 7, 2020
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Francis Mrope (Guest) on September 8, 2019
Katika imani, yote yanawezekana
Raphael Okoth (Guest) on July 19, 2019
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Diana Mumbua (Guest) on May 28, 2019
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
David Kawawa (Guest) on April 29, 2019
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Christopher Oloo (Guest) on March 26, 2019
Neema ya Mungu inatosha kwako
Frank Macha (Guest) on January 24, 2019
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
John Mushi (Guest) on December 12, 2018
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Edward Lowassa (Guest) on July 19, 2018
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Hellen Nduta (Guest) on May 11, 2018
Mwamini katika mpango wake.
Grace Njuguna (Guest) on April 6, 2017
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Mariam Kawawa (Guest) on April 3, 2017
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Kenneth Murithi (Guest) on February 14, 2017
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Anna Sumari (Guest) on February 5, 2017
Nakuombea π
Patrick Mutua (Guest) on November 7, 2016
Baraka kwako na familia yako.
Henry Sokoine (Guest) on October 30, 2016
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Nicholas Wanjohi (Guest) on July 12, 2016
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Dorothy Nkya (Guest) on May 8, 2016
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Victor Sokoine (Guest) on May 2, 2016
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Peter Mwambui (Guest) on December 11, 2015
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Lydia Wanyama (Guest) on December 8, 2015
Rehema zake hudumu milele
Anna Sumari (Guest) on October 21, 2015
Mwamini Bwana; anajua njia
Esther Nyambura (Guest) on April 21, 2015
Mungu ni mwema, wakati wote!