SOMO I
Isa. 22:19-23
Bwana, Bwana wa majeshi, asema hivi: Nami nitakusukuma na kukutoa katika mahali pako, naye atakushusha utoke hapa usimamapo. Na itakuwa katika siku ile nitamwita mtumishi wangu Eliakimu, mwana wa Hilkia; nami nitamvika vazi lako, nitamtia nguvu kwa mshipi wako, nami nitamkabidhi yeye mamlaka yako; naye atakuwa baba kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa nvumba ya Yuda. Na ufunguo wa nvumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga. Nami nitamkaza kanta msumari mahali palipo imara; naye atakuwa kiti cha utukufu kwa nyumba ya baba yake.
Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
WIMBO WA KATIKATIΒ
Zab. 138: 1-3, 6, 9 (K) 9
(K) Ee Bwana, fadhili zako ni za milele,Β
Usiziache kazi za mikono yako.
Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu. (K)
Nitalishukuru jina lako,
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa maana umeikuza ahadi yako,
Kuliko jina lako lote.
Siku ile niliyokuita ulinitikia,
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu. (K)
Ingawa Bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu,Β
Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.
Ee Bwana, fadhili zako ni za milele;
Usiziache kazi za mikono yako. (K)
SOMO 2Β
Rum 11: 33-36
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.
Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
SHANGILIO
Mt 11: 25
Aleluya, aleluya,
Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi,Β
kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye
hekima na akili. ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya
INJILIΒ
Ml 16:13-20
Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipo, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? Wakasema, Wengine hunena Yohane Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. Akawaa- mbia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Yesu akajibu, akamwambia. Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikufunulia hili, bali Baba vangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. Ndipo alipowakataza sana wanafunziΒ wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba yeye ndiye Kristo.
Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
Β
Kevin Maina (Guest) on June 2, 2024
Neema na amani iwe nawe.
Grace Mligo (Guest) on February 22, 2024
Nakuombea π
Stephen Malecela (Guest) on December 19, 2023
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
James Malima (Guest) on August 18, 2023
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Nicholas Wanjohi (Guest) on July 17, 2023
Mungu ni mwema, wakati wote!
Grace Mligo (Guest) on January 21, 2023
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Vincent Mwangangi (Guest) on December 17, 2022
Rehema zake hudumu milele
Edwin Ndambuki (Guest) on July 2, 2022
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
David Kawawa (Guest) on May 22, 2022
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Philip Nyaga (Guest) on December 1, 2021
Nguvu hutoka kwa Bwana
Lucy Mushi (Guest) on March 8, 2021
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Lucy Mahiga (Guest) on February 1, 2021
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Margaret Mahiga (Guest) on January 7, 2021
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Charles Mboje (Guest) on January 1, 2021
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Emily Chepngeno (Guest) on December 23, 2020
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Philip Nyaga (Guest) on November 27, 2020
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Stephen Malecela (Guest) on November 1, 2020
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Alice Mrema (Guest) on August 15, 2020
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Henry Sokoine (Guest) on May 13, 2020
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Anna Kibwana (Guest) on April 30, 2020
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Jane Malecela (Guest) on April 17, 2020
Tumaini ni nanga ya roho
George Mallya (Guest) on February 4, 2020
Katika imani, yote yanawezekana
Henry Mollel (Guest) on January 12, 2020
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Patrick Mutua (Guest) on January 12, 2020
Dumu katika Bwana.
John Malisa (Guest) on December 28, 2019
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Stephen Malecela (Guest) on November 13, 2019
Endelea kuwa na imani!
Daniel Obura (Guest) on November 2, 2019
Mwamini Bwana; anajua njia
Joseph Njoroge (Guest) on February 24, 2019
Sifa kwa Bwana!
George Wanjala (Guest) on February 7, 2019
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Victor Kamau (Guest) on December 2, 2018
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Charles Mchome (Guest) on August 28, 2018
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Edward Chepkoech (Guest) on July 28, 2018
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Nora Lowassa (Guest) on March 14, 2018
Imani inaweza kusogeza milima
Margaret Mahiga (Guest) on November 7, 2017
Baraka kwako na familia yako.
Paul Kamau (Guest) on October 8, 2017
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Bernard Oduor (Guest) on September 17, 2017
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Patrick Kidata (Guest) on June 29, 2017
Mungu akubariki!
Anna Malela (Guest) on April 16, 2017
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Diana Mallya (Guest) on February 19, 2017
Neema ya Mungu inatosha kwako
Monica Nyalandu (Guest) on February 18, 2017
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Margaret Mahiga (Guest) on January 11, 2017
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Victor Mwalimu (Guest) on May 31, 2016
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Margaret Mahiga (Guest) on March 2, 2016
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Sarah Achieng (Guest) on February 11, 2016
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Fredrick Mutiso (Guest) on December 11, 2015
Rehema hushinda hukumu
David Kawawa (Guest) on December 1, 2015
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Samson Tibaijuka (Guest) on November 8, 2015
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Robert Ndunguru (Guest) on April 25, 2015
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Joyce Aoko (Guest) on April 14, 2015
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Anna Kibwana (Guest) on April 4, 2015
Mwamini katika mpango wake.