Kifungu cha 14 cha Katiba ya Tanzania kinaeleza kwa ufasaha
kuwa: βKila mtu ana haki ya kuishi na kulindwa utu wake katika
jamii kwa misingi ya sheria.β Hata Rais Kikwete katika hotuba
zake kwa Taifa za kila mwezi amewahi kukemea mauaji haya
mwaka 2008 kwa kusema; β mauaji haya ni aibu na fedheha
kubwa kwa jamii yetuβ pia βukatili usio na sababuβ na akaendelea
kusema, βni lazima yakomeshwe mara moja.β
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na taasisi na asasi za
kijamii wanaendelea kutoa mafunzo, taarifa na mazingira
yatakayowawezesha Albino kuishi maisha bora na yenye
mafanikio katika jamii.

Je, serikali imechukua hatua gani kudhibiti hali hii ya mauaji ya Albino? Tutaishi vipi?

Comments
Please log in or register to leave a comment or reply.
No comments yet. Be the first to share your thoughts!