Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰

Maana kamili ya Kwaresma

β€’
Author/Editor: Melkisedeck Leon Shine, 2015-2017: AckySHINE.com
Featured Image
Neno kwaresma ni neno la kilatini liitwalo Quadragesima maana yake ni arobaini(40). Mpenzi msomaji, katika maisha ya kikristo kuna kipindi cha siku 40.majira haya ya kwaresma huanza siku ya jumatano ya majivu na kuishia jumapili ya pasaka siku ambayo wakristo wanakumbuka kufufuka kwa yesu kristo kutoka katika wafu.
Kwaresma ni kipindi maalum ambacho wakristo wanakumbuka maisha ya Yesu kristo hapa duniani hususan mateso, kufa na kufufuka kwake.
Ni kipindi cha kutafakari maana na umuhimu wa dhabihu ya YESU kristo katika ukombozi wa dunia na kumrudia Mungu. Aidha ni kipindi ambacho wakristo wanakumbushwa kufanya toba na kumrudia Mungu kwa mujibu wa maandiko matakatifu.
Ingawa kipindi cha kwaresma ni kipindi cha mafungo kwa wakristo, watu wengi na hasa wa dini nyingine hushindwa kutambua funga inayofanywa na wakristo katika kipindi hiki na hasa kwa sababu wakristo wengi huonekana wakiendelea kula na kunywa wakati wa kwaresma. Wakristo walio wengi pamoja na kufuata kielelezo cha Yesu kristo ambae alifunga siku arobaini (usiku na mchana) huzingatia maagizo ya YESU mwenyewe na nabii Isaya ambao kwa kiasi kikubwa hufafanua aina ya funga ambayo wakristo wanapaswa kuizingatia.
Mwenyezi Mungu alitoa maagizo ya namna ya kufunga kupitia kwa nabii isaya akisema hivi
"Walakini wanitafuta kila siku, hupenda kujua njia zangu ; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao. Hutaka kwangu sheria za haki, humkaribia Mungu. Husema, mbona tumefunga lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu lakini huangalii? Fahamuni siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu. Je, kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je, ni siku ya mtu kujitabisha nafsi yake? je ni kuinamisha kichwa kama unyasi na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? je utasema ni siku ya kufunga na ya kukubaliwa na BWANA? Je, saumu niliyoichagua sio ya namna hii? Kufunguo vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaachia huru walio onewa, na kwamba mvunje kila nira? Je, sio kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? umwonapo mtu aliye uchi umvike nguo, wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapo pambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia, utukufu wa BWANA (Mungu) utakufuata nyuma ukulinde. Ndipo utaita na BWANA ataitika, utalia nae atasema mimi hapa…" (Isaya 58: 2-9).
Mwenyezi Mungu alitoa maagizo haya baada ya kuona watu wengi wakipoteza muda mwingi na kujitabisha kuacha kula na kujitesa miili yao ili kumpendeza Mungu, huku wakisahau mambo muhimu zaidi ambayo Mungu anawataka wafanye ili kumpendeza. (Katika kipindi hicho wayahudi walikuwa wakifunga kwa kujitesa sana ikiwa ni pamoja na kuacha kula, kuvua nguo zao za thamani na kuvaa magunia, kujipaka majivu na wengine kujipiga na kujikata miili yao ili waone maumivu zaidi.
Aidha, watu walikuwa wakitumia kipindi cha kufunga kuuonesha umma jinsi walivyo wacha Mungu na hivyo kupewa heshima mtaani. Mtu asiyefunga alionekana mjinga, mtenda dhambi na asiyefaa katika jamii. Kufunga ilikuwa sehemu ya maisha na si suala la uhusiano binafsi kati ya mtu na Mungu).

Kwa vile Mwenyezi Mungu wetu ni wa upendo na huruma, alimtuma nabii isaya kuwaambia watu hao kuachana na funga hiyo isiyo na maana na badala yake kuelekeza nguvu zao katika mambo muhimu ambayo Mungu anaangalia katika kutathimini utu wa mtu. Mambo hayo ni upendo, huruma na kujitoa kama ilivyoelezwa hapo juu na kuachana uovu wa aina zote.. Kwa msingi huo, mtu mwenye upendo na anaejitoa kusaidia wengine ana thamani kubwa mbele za Mungu kuliko mtu anaeshinda njaa siku 300 za mwaka pasipo kuonesha upendo wa kweli kwa wengine.
Yesu kristo alipokuja ulimwenguni, alisisitiza maneno ya nabii Isaya kwa kutaka watu waache tabia ya funga za kujionesha kwa watu, na badala yake wajitahidi kumpendeza Mugu.
Yesu alisema "Tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye nyuso za kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amini nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na baba yako (Mungu) aliye sirini; na baba yako aonae sirini atakujazi" (Mathayo 6:16)
Kumbe tabia ya kujionesha mbele za watu kwamba tumefunga inamuudhi Mungu na kutufanya tukose thawabu. Mtu anaejionesha au kujisifu kwamba anafunga huambulia kusifiwa na watu wa kidunia ambao wanadhani mtu huyo ni mtakatifu sana, lakini kwa mujibu wa maandiko matakatifu mtu huyo anajisumbua na kupoteza muda wake bure kwani hakuna thawabu anayo pata kwa Mwenyezi Mungu.
Tumuombe Mungu sana atuongoze na kutusaidia katika kipindi hiki cha Kwaresma na baada ya hapo.Ni wajibu wetu kujitahidi kuachana na maovu yote, kufanya toba ya kweli na kumpokea Yesu katika mioyo yetu badala ya kumuabudu kwa midomo tu. Tunapaswa kukumbuka kuwa Mungu wetu ni yule yule kabla, wakati na baada ya kipindi cha Kwaresma na hivyo kipindi hiki kiwe kipindi cha kutukumbusha na kutuandaa kwa ajili ya wakati mrefu ujao baada ya Kwaresma.
AckySHINE Solutions
✨ Join AckySHINE for more features! ✨

Comments 50

Please log in or register to comment or reply.
πŸ‘₯ Mary Njeri Guest Jun 19, 2024
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
πŸ‘₯ Hellen Nduta Guest May 18, 2024
Neema ya Mungu inatosha kwako
πŸ‘₯ Henry Mollel Guest Apr 27, 2024
Mungu akubariki!
πŸ‘₯ Edith Cherotich Guest Oct 28, 2023
Tembea kwa imani, si kwa kuona
πŸ‘₯ Dorothy Mwakalindile Guest Oct 8, 2023
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
πŸ‘₯ Charles Mrope Guest Sep 22, 2023
Endelea kuwa na imani!
πŸ‘₯ Chris Okello Guest Aug 27, 2023
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
πŸ‘₯ Stephen Mushi Guest May 2, 2023
Dumu katika Bwana.
πŸ‘₯ Robert Okello Guest Feb 7, 2023
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
πŸ‘₯ David Ochieng Guest Jan 2, 2023
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
πŸ‘₯ David Ochieng Guest Dec 26, 2022
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
πŸ‘₯ John Kamande Guest Sep 3, 2022
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
πŸ‘₯ James Kimani Guest Aug 18, 2022
Neema na amani iwe nawe.
πŸ‘₯ Andrew Odhiambo Guest Jul 25, 2022
Imani inaweza kusogeza milima
πŸ‘₯ Emily Chepngeno Guest Jun 2, 2022
Wakati wa Mungu ni kamilifu
πŸ‘₯ Anna Mahiga Guest Apr 21, 2022
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
πŸ‘₯ Lucy Wangui Guest Dec 28, 2021
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
πŸ‘₯ Ruth Wanjiku Guest Sep 3, 2021
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
πŸ‘₯ George Mallya Guest Aug 15, 2021
Mwamini katika mpango wake.
πŸ‘₯ Lucy Kimotho Guest Feb 28, 2021
Mwamini Bwana; anajua njia
πŸ‘₯ John Lissu Guest Jan 1, 2021
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
πŸ‘₯ Esther Nyambura Guest Dec 20, 2020
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
πŸ‘₯ Dorothy Nkya Guest Jun 10, 2020
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
πŸ‘₯ John Malisa Guest Jun 6, 2020
Rehema zake hudumu milele
πŸ‘₯ Alice Mwikali Guest Jul 1, 2019
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
πŸ‘₯ Alice Mwikali Guest May 28, 2019
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
πŸ‘₯ Betty Akinyi Guest Feb 13, 2019
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
πŸ‘₯ David Musyoka Guest Dec 21, 2018
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
πŸ‘₯ Monica Nyalandu Guest Dec 4, 2018
Tumaini ni nanga ya roho
πŸ‘₯ Grace Njuguna Guest Sep 30, 2018
Rehema hushinda hukumu
πŸ‘₯ Ruth Mtangi Guest Jul 27, 2018
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
πŸ‘₯ Simon Kiprono Guest May 29, 2018
Mungu ni mwema, wakati wote!
πŸ‘₯ Joseph Mallya Guest Apr 23, 2018
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
πŸ‘₯ Edith Cherotich Guest Apr 1, 2018
Sifa kwa Bwana!
πŸ‘₯ Joy Wacera Guest Nov 26, 2017
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
πŸ‘₯ Dorothy Nkya Guest Oct 8, 2017
Nguvu hutoka kwa Bwana
πŸ‘₯ Nancy Kawawa Guest Aug 13, 2017
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
πŸ‘₯ Mariam Hassan Guest Jun 8, 2017
Katika imani, yote yanawezekana
πŸ‘₯ Susan Wangari Guest May 14, 2017
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
πŸ‘₯ Edward Chepkoech Guest Apr 2, 2017
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
πŸ‘₯ Lydia Wanyama Guest Dec 23, 2016
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
πŸ‘₯ Monica Nyalandu Guest Dec 12, 2016
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
πŸ‘₯ Lucy Kimotho Guest Sep 23, 2016
Kwa Mungu, yote yanawezekana
πŸ‘₯ Stephen Amollo Guest May 3, 2016
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
πŸ‘₯ Patrick Akech Guest Feb 22, 2016
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
πŸ‘₯ Joseph Kiwanga Guest Feb 5, 2016
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
πŸ‘₯ David Musyoka Guest Jan 24, 2016
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
πŸ‘₯ Benjamin Kibicho Guest Jan 24, 2016
Baraka kwako na familia yako.
πŸ‘₯ David Kawawa Guest Oct 7, 2015
Nakuombea πŸ™
πŸ‘₯ George Ndungu Guest Jul 18, 2015
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako

πŸ”— Related Posts

🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About