SOMO 1 - Kut. 3:1-8a, 13-15
Basi, Musa alikuwa akilichunga kunda la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpka mlima wa Mungu, hata Horebu. Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei. Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa. Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu. Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali.Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake nβnani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, Mimi niko ambaye niko, akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; Mimi niko amenituma kwenu. Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.Neno la Bwanaβ¦ Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI - Zab. 103:1-4, 6-8, 11 (K) 8
(K) Bwana amejaa huruma na neema.Ee nafsi yangu umhimidi Bwana.Naam, vyote vilivyo ndani yanguVilihimidi jina lake takatifu.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,Wala usizisahau fadhili zake zote.
(K)Akusamehe maovu yako yote,Akuponya magonywa yako yote,Aukomboa uhai wako na kaburi,Akutia taji ya fadhili na rehema.
(K)
Bwana ndiye afanyaye mambo ya haki,Na hukumu kwa wote wanaoonewa.Alimjulisha Musa njia zake.Wana wa Israeli matendo yake. (K)
Bwana amejaa huruma na neema,Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,Kadiri ileile rehema zake ni kuu kwa wamchao. (K)
SOMO 2 - 1 Kor. 10:1-6, 10-12
Ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa wawe na Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.Wala msinungβunike kama wengine wao walivyonungβunika, wakaharibiwa na mharabu.Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.Neno la Bwanaβ¦ Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO - Zab. 95:8
Msifanye migumu mioyo yenu; Lakini msikie sauti yake Bwana.
INJILI - Lk. 13:1-9
Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha Yesu habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichangaya damu yao na dhabihu zao. Akawajibu akawaambia.Je! Mwadahni ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamb awao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.Neno la Bwana⦠Sifa kwako Ee Kristo.
Rose Lowassa (Guest) on January 6, 2024
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Janet Wambura (Guest) on September 5, 2023
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Nancy Akumu (Guest) on August 21, 2023
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Elizabeth Mtei (Guest) on May 9, 2023
Nakuombea π
Janet Mbithe (Guest) on January 13, 2023
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
James Malima (Guest) on December 14, 2022
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Alice Mrema (Guest) on September 15, 2022
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Jane Muthui (Guest) on July 27, 2022
Endelea kuwa na imani!
Anthony Kariuki (Guest) on April 26, 2022
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Nancy Komba (Guest) on April 11, 2022
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Anna Mchome (Guest) on February 11, 2022
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Jackson Makori (Guest) on February 7, 2022
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
George Ndungu (Guest) on January 8, 2022
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Betty Kimaro (Guest) on December 19, 2021
Neema na amani iwe nawe.
Mercy Atieno (Guest) on July 9, 2021
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
James Kimani (Guest) on May 23, 2021
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Andrew Odhiambo (Guest) on May 16, 2021
Mungu ni mwema, wakati wote!
Ruth Wanjiku (Guest) on April 11, 2021
Rehema hushinda hukumu
Jane Malecela (Guest) on November 16, 2020
Neema ya Mungu inatosha kwako
Elizabeth Malima (Guest) on August 30, 2020
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
David Sokoine (Guest) on June 24, 2020
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Richard Mulwa (Guest) on March 7, 2020
Sifa kwa Bwana!
Hellen Nduta (Guest) on December 29, 2019
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Esther Cheruiyot (Guest) on November 18, 2019
Rehema zake hudumu milele
George Wanjala (Guest) on September 16, 2019
Baraka kwako na familia yako.
Mary Kendi (Guest) on August 12, 2019
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
George Ndungu (Guest) on June 17, 2019
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Benjamin Kibicho (Guest) on April 13, 2019
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Frank Sokoine (Guest) on April 10, 2019
Mwamini katika mpango wake.
Joseph Mallya (Guest) on February 15, 2019
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Michael Onyango (Guest) on November 30, 2018
Tumaini ni nanga ya roho
Margaret Mahiga (Guest) on June 24, 2018
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Lucy Kimotho (Guest) on January 3, 2018
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Nora Kidata (Guest) on November 30, 2017
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Irene Makena (Guest) on November 30, 2017
Imani inaweza kusogeza milima
Andrew Mahiga (Guest) on October 13, 2017
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Anna Sumari (Guest) on August 28, 2017
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Lydia Mzindakaya (Guest) on August 22, 2017
Katika imani, yote yanawezekana
John Malisa (Guest) on December 10, 2016
Mungu akubariki!
Mary Kidata (Guest) on September 12, 2016
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Joyce Aoko (Guest) on June 11, 2016
Dumu katika Bwana.
Sharon Kibiru (Guest) on May 25, 2016
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Emily Chepngeno (Guest) on November 6, 2015
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
John Malisa (Guest) on November 6, 2015
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Nancy Kawawa (Guest) on September 24, 2015
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Lucy Mushi (Guest) on September 14, 2015
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Edward Lowassa (Guest) on August 16, 2015
Mwamini Bwana; anajua njia
Moses Mwita (Guest) on July 24, 2015
Nguvu hutoka kwa Bwana
Monica Adhiambo (Guest) on June 12, 2015
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Carol Nyakio (Guest) on April 17, 2015
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha