SOMO 1
Hos. 5:15-6:6
Bwana asema: Katika taabu yao watanitafuta kwa bidii:
Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu. Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tuataishi mbele zake. Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua Bwana; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyeshayo nchi.
Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema. Kwa sababu hiyo nimewakata-kata kwa vinya vya manabii; nimewaua kwa maneno ya kinywa change na hukumu yangu itatokea kama mwanga. Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
Neno la Bwana⦠Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 51:1-2, 16-19 (K) Hos. 6:6
(K) Ninavyotaka ni fadhili, si sadaka.
Ee Mungu, unirehemu,
Sawasawa na fadhili zako.
Kiasi cha wingi wa rehema zako,
Uyafute makosa yangu.
Unioshe kabisa na uovu wangu,
Unitakase dhambi zangu. (K)
Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa,
Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.
Dhabihu za MUngu ni roho iliyovunjika;
Moyo uliovunjika na kupondeka,
Ee Mungu, hutaudharau. (K)
Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako,
Uzijenge kuta za Yerusalemu.
Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki,
Na sadaka za kuteketezwa, na kafara. (K)
SHANGILIO
Eze. 18:3
Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa yote, asema Bwana, jifanyieni moy mpya na roho mpya.
INJILI
Lk. 18:9-14
Yesu aliwaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyangβanyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mpato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Neno la Bwana⦠Sifa kwako Ee Kristo.
Anna Mahiga (Guest) on September 26, 2023
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Henry Sokoine (Guest) on November 19, 2022
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Faith Kariuki (Guest) on July 2, 2022
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Andrew Mchome (Guest) on July 7, 2021
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Janet Wambura (Guest) on October 17, 2020
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Jane Muthui (Guest) on September 22, 2020
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
Charles Mboje (Guest) on June 25, 2020
Dumu katika Bwana.
Frank Sokoine (Guest) on May 19, 2020
Endelea kuwa na imani!
George Ndungu (Guest) on May 3, 2020
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
David Kawawa (Guest) on May 2, 2020
Nakuombea π
Janet Sumari (Guest) on April 17, 2020
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Mariam Hassan (Guest) on February 16, 2020
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Josephine Nekesa (Guest) on January 27, 2020
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Joyce Aoko (Guest) on November 24, 2019
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Peter Mugendi (Guest) on November 14, 2019
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Moses Kipkemboi (Guest) on November 10, 2019
Nguvu hutoka kwa Bwana
Alice Wanjiru (Guest) on September 7, 2019
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Peter Otieno (Guest) on September 3, 2019
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Alice Mwikali (Guest) on August 25, 2019
Rehema zake hudumu milele
Linda Karimi (Guest) on July 10, 2019
Baraka kwako na familia yako.
Dorothy Majaliwa (Guest) on March 27, 2019
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Janet Sumari (Guest) on March 14, 2019
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Nancy Akumu (Guest) on February 9, 2019
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Patrick Kidata (Guest) on January 26, 2019
Katika imani, yote yanawezekana
James Malima (Guest) on January 15, 2019
Mungu akubariki!
David Chacha (Guest) on January 5, 2019
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Robert Ndunguru (Guest) on January 4, 2019
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Paul Kamau (Guest) on January 3, 2019
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Grace Minja (Guest) on October 9, 2018
Neema na amani iwe nawe.
Charles Mrope (Guest) on October 2, 2018
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Janet Mbithe (Guest) on June 13, 2018
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Martin Otieno (Guest) on June 2, 2018
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Lydia Wanyama (Guest) on March 31, 2018
Sifa kwa Bwana!
Moses Mwita (Guest) on December 7, 2017
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Ann Wambui (Guest) on February 11, 2017
Neema ya Mungu inatosha kwako
Ruth Wanjiku (Guest) on January 17, 2017
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Joseph Mallya (Guest) on December 9, 2016
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
George Ndungu (Guest) on October 30, 2016
Mungu ni mwema, wakati wote!
Ruth Mtangi (Guest) on October 7, 2016
Tumaini ni nanga ya roho
Agnes Lowassa (Guest) on October 2, 2016
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Michael Onyango (Guest) on September 5, 2016
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Anna Mchome (Guest) on June 9, 2016
Rehema hushinda hukumu
George Ndungu (Guest) on June 4, 2016
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Andrew Mchome (Guest) on April 26, 2016
Mwamini Bwana; anajua njia
Agnes Njeri (Guest) on February 22, 2016
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Mercy Atieno (Guest) on January 10, 2016
Mwamini katika mpango wake.
Daniel Obura (Guest) on December 11, 2015
Imani inaweza kusogeza milima
Jane Muthoni (Guest) on November 9, 2015
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Violet Mumo (Guest) on November 1, 2015
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Lucy Mahiga (Guest) on April 12, 2015
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako